Wewe unayejidai una akili lakini unashindwa kuelewa kwa nini all of a sudden nchi imegawanyika kidini namna hii kwenye awamu hii kuliko wakati mwingine wowote! Nyerere pamoja na mapungufu yake yote aliwafanya watz kujiona kitu kimoja! Nilimsikia anayejiita Prof Lipumba kwamba kwa asili watz ni watu wa amani bila kujua kwamba amani iliyopo imetengenezwa na haijaja yenyewe!
Peleka udini wako huko uarabuni, elewa kuwa Tanzania haitakaa iwe nchi ya kiislam hata kama Kikwete akigeuza baraza zima liwe la waislam pekee.
Ama kweli tunakoelekea kubaya ... kama Omari naye amefikia pa kulinganisha waraka wa kikatoliki na kile alichofanya Ponda na wenzake wakati wa utawala wa Mkapa.
unapondea wanachoandika wenzako wakati na wewe unafanya kile kile tu walichofanya wenzako.
Huo ndio usongo mliokuwa nao wa kuwa JMK ni muIslam na anendesha mambo vizuri kama alivyoigeuza nchi Mwinyi, mkamuandama mkashindwa na sasa mnamuandama JMK, hamtoweza. Na mashule atajenga na mavyuo anajenga na ataendelea kujenga na waIslam watasoma sasa bila kuwa na sababu ya kuchaguana. Janja yake panya sisi kwisha tambuwa!
Kipi nilichofanya mimi? Nilipinga waraka kama ninavyopinga muongozo. Yote kwangu ni petrol kwenye moto unaofuka....
Ninchosema ni kuwa kama ilivyokuwa sawa kuwashughulikia kina Ponda then na pia ni sawa kuwashugulikia kina Pengo na Ponda sasa.....Wote wanacheza na misingi ya utaifa wetu whatever the justifications they have...Misingi ipo kwa ajili ya kutumika wakati wote haswa pale ambako tunadhani kuwa tuna haki ya kuivunja...
omarilyas
Huwezi kulinganisha alichofanya Pengo na kile cha Ponda. Ni vitu na mambo mawili tofauti. Hakuna kokote kule Pengo alipochochoe wakatoliki wafanye fujo dhidi ya serikali yao kama alivyokuwa akifanya Ponda wakati wa Mkapa.
Come on Omari, unajua hili vizuri sana.
Unaongea nini wewe? Una akili timamu kweli?
Hoja ya mimi ninayempinga Pengo ni kama ifuatavyo.
Pengo hakuzungumza kama raia wa kawaida kama wewe na mimi, amezungumza kama kiongozi wa dini.
Katika mazungumzo yake amekemea ufisadi-sasa ninakuuliza, katika Biblia wapi waumini wameamrishwa kukemea maasi na maovu?
Kuna faida gani ya kumsikiliza wakati Paulo ameshasema ndani ya Biblia kwamba sasa sheria haina nafasi mbele ya Mungu?Rejea aya nilizozileta.
Paulo amesema 'kupona (salvation)' hakutegemei vitendo wala utii wa amri Mungu, kupona mbele ya Mungu kunategea imani kwamba Mungu amekufa msalabani kwa ajili ya midhambi ya waumini, sasa hoja ya kufuata 'the law' inatoka wapi?
Of course common sense inasema corruption ina athari. Je, wewe uko tayari kukiri kwamba sheria za kikatoliki zinatungwa na common sense hata kama hazina support ya kitabu (Bible)?Kama ni hivyo, je hizo zitaitwa sheria za Mungu ama za binaadamu?Kama za kibanaadamu kwa nini zisiwe challenged?
Kama angekuwa Muislamu ningemuelewa kwa sababu kitabu cha Waislamu kinasema wazi kwamba Mungu hapendi ufisadi na mafisadi na pia waumini wa Kiislamu wanaambiwa wazi wazi wakatazane mabaya na kukumbushana mema.
Wapi ndani ya Biblia waumini wameamrishwa kukatazana mabaya? Tuanze na hapo ili tuone kama kweli kauli yake imekuwa motivated na Biblia ama maoni binafsi.
Tukikubali maoni binafsi yatangazwe hadhadhari na viongozi wa dini kwa kutumua kivuli cha dini ni sawa na kuwakubalia magaidi wafanye vitu vyao na kusingizia dini.
JK =
Richmond/Dowans
Buzwagi
EPA
Matumizi yasiyo na maelezo ikulu
Mikataba feki ya madini
Inflation ya kutisha
Na mengine kibao.
JK kafanya ufisadi mwenyewe na watu wakaujua na wakaanza kumsema. Hayo mengine ni ya kwako.
EPA ni madudu yaliyosukw, kukubaliwa na hata kutekelezwa wakati wa MKAPA na sio JK. Matumizi yasiyo na maelezo Ikulu ni ugonjwa wa miaka yote kwa marais wote. Mikataba feki ni mkataba wa BUZWAGI tu kati ya mikataba zaidi ya sita ya uchimbji mkubwa ndio umesainiwa wakati wa JK
Punguza muda unaoutumia kwenye al arabiya labda utaelewa anachokisema Pengo.
Huwezi kulinganisha alichofanya Pengo na kile cha Ponda. Ni vitu na mambo mawili tofauti. Hakuna kokote kule Pengo alipochochoe wakatoliki wafanye fujo dhidi ya serikali yao kama alivyokuwa akifanya Ponda wakati wa Mkapa.
Come on Omari, unajua hili vizuri sana.
Alichosema kinaeleweka na sikukihoji.
Nimehoji uhalali wa yeye kusema aliyoyasema.
Amri ipi ndani ya kitabu chake inachompa yeye uhalali wa kukemea maovu?
Kama una ushihidi bring it on badala ya kulaumu al arabiya.
Ninachokihofia kanisa katoliki linafadhiliwa na Mafias wanapesa nyingi na utajiri wa uchafu, Mungu aepushe wasije wakamhujumu rais wa nchi na nchi yenyewe. Pengo hakusita kuonyesha chuku na hasira yake kwa rais tumeshuhudia maneno yake makali ya utovu wa adabu na ufedhuli aliyoyatoa mbele ya rais Kikwete katika maziko ya askofu Mayalla kule Mwanza, alijuburi na kuonyesha kuwa anamdharau rais na kumfedhehesha mbele ya kadamnasi yeye na serikali yake kwa kuonyesha tu kutopigia magoti wito wa kanisa uliopewa jina la "waraka wa kanisa".
Tusubiri uchaguzi ujao tutaona vituko vya nuuni firauni kwa Pengo na watu wake wanajiita wapiganaji dhidi ya ufisadi wakati wakiwa ndani ya system ya kifisadi.
Mmeona wapi Ibilisi akamuongoza mtu katika ibada?
Well, kama unajua socialpolitics za Tanzania ni wazi utang'amua kuwa wanachokifanya kina Pengo ni hichohicho lakini kwa kutumia maneno ya kuvutia na sio ya ghadhabu na makali kama ya kina PONDA...
Wote ni sawa tu kwani kwao wao kuchanganya DINI na SIASA ni sawa pale inapoendana na matakwa na maslahi yao na ni Haramu pale wengine wanapotumia kuwalenga wale wanaowaona watu wao kama walivokuwa wakifanya kina Ponda kwa Mkapa....Kumbuka hiki tunachokiita hapa WARAKA ukweli ni kuwa kiliandikwa ni ILANI.......ni waandishi ndio wamekuza neno waraka kupunguza makali yake.....I know the story behind WARAKA na najua kuwa halikuwa wazo la PENGO lakini ameubariki kuwaunga mkono RADICALS wa upande wake ambao hawana tofauti na kina Ponda.....
omarilyas
haitaji kitabu cha kiarabu ili kukemea uovu
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. EPA ni madudu yaliyosukw, kukubaliwa na hata kutekelezwa wakati wa MKAPA na sio JK. Matumizi yasiyo na maelezo Ikulu ni ugonjwa wa miaka yote kwa marais wote. Mikataba feki ni mkataba wa BUZWAGI tu kati ya mikataba zaidi ya sita ya uchimbji mkubwa ndio umesainiwa wakati wa JK. Mingine yote ikiwemo ule wa unyama na aibu wa BULYANHULU ulikuwa wakati wa Mkapa.
Ni ujinga wa hali ya juu kuanza kutuhumu udhaifu wa URAIS kwa misingi ya kidini. Huu ni ujinga wa hali ya juu ambao unatufanya tuwe asusa za wanasiasa hovyohovyo kutupumbaza na kututumia kwa ajenda zao bila ya kuwapima kwa kutumia vigezo makini......
omarilyas
Kanisa halifadhiliwi na mafia. .... acha kashfa wewe au ndio mambo yale ya kusema misikiti inafadhiliwa na magaidi kama Osama?
Omari,
Ni ujinga wa hali ya juu kumtetea raisi kwa misingi ya kidini (nikitumia logic yako hapa).
Pesa za EPA zilisaidia uchaguzi wa ccm na KIkwete. Yeye hakukataa ingawa alijua kila kitu kinachoendelea.
Buzwagi ni ya Kikwete hilo kila mtu analijua.
Mikataba ya madini ingebadilishwa kama Kikwete angekuwa na nia ila kwa vile yeye ni fisadi kama walioisaini basi ameshindwa kufanya lolote kuibadili.
Pengo haitaji kitabu cha kiarabu ili kukemea uovu. Yeye kama mtanzania ana kila sababu ya kukemea ufisadi wa serikali ya Kikwete na mpango wa kutaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kiislam