JIBU LANGU: mi naona kuwa unachanganya mambo. Kardinale na maaskofu walibariki waraka wa dini yao na si wa serikali. Naomba hili ulielewe. Waraka ule si wa waislamu wala wapagani. Ni waraka wa wakatoliki, sasa kama wewe si Mkatoliki waraka ule unakuhusuje? Mbona wakatoliki hawaujadili ila watu wasio wakatoliki wanauvalia njuga kama wao?
Na hapo ndio kwenye tatizo. Asasi ama uongozi wa kidini kutoa misimamo, maelekezao ama matamshi yanayohusu SIASA tena uhcaguzi wa viongozi wa kuwawakilisha watanzania wote kwa ujumla wao, wawe waislamu ama wakristo ni kuvunja, kukiuka ama kudharau misingi ya taifa letu na zaidi kuhatarisha mustakabali wa taifa letu haswa katika swala la maelewano, mepenzi na kuaminiana miongoni mwa watanzania....
Ahaaa! UFISADI! Je wewe unapenda Mafisadi? Kama unawapenda basi naona una kila sababu ya kuupinga waraka ule maana umegusa mioyo ya mafisadi zaidi. Kama si fisadi, naomba vilete vipengele vya waraka unavyovipinga ili tuvijadili!
Nakushauri usome hotuba ya Mwalimu Nyerere inayoitwa TUJISAHIHISHE aliyoitoa mwaka 1962 akihutubia bunge la Tanganyika. Hii tabia ya kukimbilia kuwatuhumu watu wanaoipingana ama kutofautiana na mitizamo na hoja zenu kuwa sio wazalendo, wana chuki na dini za wengine ama watu wengine, wajinga, wanafiki, mafisadi ama wanapenda au kutetea ufisadi, ni tabia mufilisi ambayo haisaidi taifa kuondokana na madhila na hatari tunazokumbana nazo. haina tofauti na wale wana CCM wanaofikiri kuwa watu wote wasiokubaliana na utawala wao ni wapinzani, wasio wazalendo, wana choyo, wana uchu wa madaraka, wakorofi n.k
Ni lazima TUJISAHIHISHEili tuweze kuondokana na huo Uozo tunaoushutumu. Ama sivyo tutafanikiwa kuondoa uozo mmoja na kuingiza UVUNDO mwengine.
Ninapinga zaidi mantiki, uhalali na mazingira ya utolewaji wa WARAKA na MUONGOZO zaidi ya yaliyomo ndani yake. Hata kama yaliyomo ndani yake yanaweza kuwa yanahitajika sana lakini kushindwa kuheshimu MISINGI YA UTAIFA WETU na kutambua mazingira ya kisiasa na kijamii tuliyo nayo sasa kunaondoa uhalali wote wa kilichoandikwa ndani ya ILANI cum WARAKA ama MUONGOZO ......
omarilyas
Halafu kardinale kama kiongozi yeyote yule wa dini yeyote anaweza kumshauri mheshimiwa Rais. Zaidi ya hayo kardinale ni mtanzania vile vile.
Ushauri wa kiungwana na wenye nia njema ya kujenga kati ya watu wawili wanaoheshimiana na ambao ni viongozi wa kitaifa hautolewi majukwaani na kwa kuanzisha movements....Pia ukumbuke kuwa Waraka haukuwa wazi kwa wote hadi pale waandishi wa habari walipoamua kutumia ujasusi kuupata na kuutoa magazetini. Nalijua hilo kwa undani wake.
Ni kweli Waraka unaipa changamoto serikali lakini pia unahatarisha amani na maelewano kati ya watanzania na hivyo kutishia usalama wa taifa kama ambavyo hao viongozi walio mafisadi wafanyavyo. Naamini kuna njia zingine makini za kutoa changamoto hilo ambalo linahitajika sana lakini sio katika njia za Waraka wala Muongozo..Ama kwa kutimia Makanisa ama Misikiti...Waraka unaipa changamoto ya serikali kupambana na mafisadi. Ila haupingi serikali. Ila kwa bahati mbaya, baadhi ya viongozi wa serikali ni mafisadi. Ndio maana wanasema waraka una malengo ya kisiasa zaidi ya kutoa elimu ya uchaguzi kwa wakatoliki.
Hakuna elimu ya urai isiyo na malengo ya kisiasa....tuache kudanganyana. Na wala sio dhambi kuwa na malengo ya kisiasa lakini ni muhimu kutekeleza malengo hayo bila ya kuvunja misingi na maadili ya UTAIFA wetu haswa pale inapohusisha suala la tofauti za kiimani ama nyinginezo za kijamii katika taifa ambalo halina asasi imara za kiutawala kama ilivyo hapa kwetu Tanzania.
omarilyas
Ndugu yangu Omarilyas uliandika: "Na hapo ndio kwenye tatizo. Asasi ama uongozi wa kidini kutoa misimamo, maelekezao ama matamshi yanayohusu SIASA tena uhcaguzi wa viongozi wa kuwawakilisha watanzania wote kwa ujumla wao, wawe waislamu ama wakristo ni kuvunja, kukiuka ama kudharau misingi ya taifa letu na zaidi kuhatarisha mustakabali wa taifa letu haswa katika swala la maelewano, mepenzi na kuaminiana miongoni mwa watanzania...."
Hoja yangu ni:
Mi nadhani bado hujaelewa kuwa waraka wa wakatoliki ni waraka kwa ajili ya wakatoliki kuwaelimisha kulingana na imani yao juu ya jamii yao kimwili, kiroho, kijamii, kisiasa, n.k. Waraka hauna malengo ya kumweka mtu madarakani bali unawakumbusha wakatoliki kuchagua viongozi wenye busara na wasio mafisadi. Maana imani za kikatoliki hazikubali ufisadi. Zinataka kuwaelimisha wananchi. Sasa ni jinsi gani waraka huu unahatarisha usalama wa taifa? Mambo ya wakatoliki ni ya wakatoliki, si ya waislamu, si ya wanasiasa, bali ni ya wakatoliki. Pingeni mpaka mchoke waraka ndo hivyo umeshatoka na wakatoliki tutatekeleza maagizo ya viongozi wetu. Maaskofu msichoke kupinga ufisadi, tunawaunga mkono. Hongereni sana! Tumsaidieni Rais Kikwete kupigana na mafisadi, hawatufai katika Tanzania yetu hii tunayoipenda. Wakatoliki tu Watanzania tunaipenda nchi yetu na hatujavuruga amani na hatuna mpango wa kuvuruga amani. Amina.
Ndugu yang Omarilyas umeandika: Nakushauri usome hotuba ya Mwalimu Nyerere inayoitwa TUJISAHIHISHE aliyoitoa mwaka 1962 akihutubia bunge la Tanganyika. Hii tabia ya kukimbilia kuwatuhumu watu wanaoipingana ama kutofautiana na mitizamo na hoja zenu kuwa sio wazalendo, wana chuki na dini za wengine ama watu wengine, wajinga, wanafiki, mafisadi ama wanapenda au kutetea ufisadi, ni tabia mufilisi ambayo haisaidi taifa kuondokana na madhila na hatari tunazokumbana nazo. haina tofauti na wale wana CCM wanaofikiri kuwa watu wote wasiokubaliana na utawala wao ni wapinzani, wasio wazalendo, wana choyo, wana uchu wa madaraka, wakorofi n.k
Hoja yangu:
Ndio mna chuki binafsi na wakatoliki. Mbona ule wa waislamu hamuupingi! Kulikoni! Kwani waraka wa wakatoliki unahatarisha vipi taifa. Mi sioni hatari yeyote. Waraka haujawataka watu waingie Msituni wala hauchochei uadui baina ya wananchi na dini zao. Unapinga tu matendo ya kifisadi. Naomba tusilete hoja za Baba wa Taifa ambazo ukizisoma haziingiliani kabisa na dialogue hii. Tumwacheni baba wa taifa apumzike mahali pema peponi amina. Kazi aliyoifanya ni kubwa, tumweshimuni na tumtoe katika suala hili maana nadhani si vizuri kumwingiza katika hoja zetu.
Ndugu ya Omarilyas umeandika: Ni lazima TUJISAHIHISHEili tuweze kuondokana na huo Uozo tunaoushutumu. Ama sivyo tutafanikiwa kuondoa uozo mmoja na kuingiza UVUNDO mwengine.
Ninapinga zaidi mantiki, uhalali na mazingira ya utolewaji wa WARAKA na MUONGOZO zaidi ya yaliyomo ndani yake. Hata kama yaliyomo ndani yake yanaweza kuwa yanahitajika sana lakini kushindwa kuheshimu MISINGI YA UTAIFA WETU na kutambua mazingira ya kisiasa na kijamii tuliyo nayo sasa kunaondoa uhalali wote wa kilichoandikwa ndani ya ILANI cum WARAKA ama MUONGOZO ......
Hoja yangu: Ok. wewe pinga tu waraka huu. Waraka ndo hivyo tena umeshatoka. Ni kama unapiga ngumi ukuta, utaishia kujiumiza mwenyewe. Sisi vita yetu ni juu ya mafisadi na si juu ya usalama wa taifa!
Waraka wenyewe naona jamaa wameamua kuuficha. Kwa hakika tuna usongo sana na mwongozo huo. Lakini kwa bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyeuleta. Tunawaomba maustadhi mliomo humu mtuletee huo mwongozo.
Pingeni mpaka mchoke waraka ndo hivyo umeshatoka na wakatoliki tutatekeleza maagizo ya viongozi wetu.
Ndio mna chuki binafsi na wakatoliki. Mbona ule wa waislamu hamuupingi! Kulikoni! Kwani waraka wa wakatoliki unahatarisha vipi taifa. Mi sioni hatari yeyote. Waraka haujawataka watu waingie Msituni wala hauchochei uadui baina ya wananchi na dini zao. Unapinga tu matendo ya kifisadi.
Ok. wewe pinga tu waraka huu. Waraka ndo hivyo tena umeshatoka. Ni kama unapiga ngumi ukuta, utaishia kujiumiza mwenyewe. Sisi vita yetu ni juu ya mafisadi na si juu ya usalama wa taifa!
Yeyote anayejidai kumheshimu Mwalimu Nyerere na hapohapo kuunga mkono ama kujaribu kujustify ILANI cum WARAKA WA WAKATOLIKI na ama MUONGOZO WA SHURA YA MAIMAMU ni ama hajui ni kwanini tunamuita Baba wa Taifa na au ni mnafiki mkubwa......Naomba tusilete hoja za Baba wa Taifa ambazo ukizisoma haziingiliani kabisa na dialogue hii. Tumwacheni baba wa taifa apumzike mahali pema peponi amina. Kazi aliyoifanya ni kubwa, tumweshimuni na tumtoe katika suala hili maana nadhani si vizuri kumwingiza katika hoja zetu.
kulingana na gazeti la majira la leo askofu wa jimbo kuu katoliki la dar es salaam, muadhama polycarp kardinali pengo ameibuka tena na kutangaza mapambano mapya dhidi ya mafisadi huku akidai nchi imeoza na kamwe kanisa halitakaa kimya na kulea hali hiyo.
- asema kamwe kanisa halitakubali kunyamaza.
- asema watapambana na ufisadi hadi mwisho.
- aapa kupambana na yeyote anayetetea uovu.
- asema katoliki haliandai mgombea urais mwaka 2010.
- adai anayeogopa waraka wa kanisa ni fisadi.
Ndugu yangu MZINGANYIKA, naona umeshindwa kabisa kujibu swali langu? Nilikuuliza wewe ni muumini wa dini gani? Na kwamba utoe ushaidi kuhusu yale uliyoyasema kuwa kanisa halitakiwi kupinga ufisadi. Umeshindwa kujieleza. !
Waraka wenyewe naona jamaa wameamua kuuficha. Kwa hakika tuna usongo sana na mwongozo huo. Lakini kwa bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyeuleta. Tunawaomba maustadhi mliomo humu mtuletee huo mwongozo.
Ukitaka ujadili vizuri point zako inabidi kwanza uelewe unachoongea. What is politics in first place? Maana wewe unatenganisha kabisa politics na maisha ya kila siku. Lazima ujue kuwa Siasa ndiyo tunaishi nayo kila siku, na ndiyo ina-shape our lives. Please go back to learn and come to discuss. Pengo, Kikwete, Myself and yourself are ruled by politics and our destiny detrermined by political affiliation a country moulds itself to. Kwa mfano Siasa ya ujamaa ili-affect vipi maisha yetu. Je sasa, maisha yetu yote yako impacted na hisi siasa. Hata dini inashape vile vile kwa sababu wale watu nao wanaomini hizo dini wako shaped na hizi political za uchwara! Wakeup please!!
Jina langu ni mzanganyika, sio mzinganyika ndugu.
Nimeleta makala ya Padri aliyeeleza wazi wazi kwamba mission ya Yesu haikujumuisha worldly affairs. Pia nimesema hakuna maamrisho ndani ya Biblia yanayowaamuru utekelezaji wa any code of conduct katika worldly affairs.
Biblia haina muongozo wa maswala ya kiulimwengu kwa sababu hiyo haikuwa mission ya Jesus. Mission yake ilikuwa in spirituality tu.
Umenielewa ama bado?
Ndio maana nilihoji Pengo anadhibitiwa na nini kwa sababu amezungumza mambo yaliyo nje ya Biblia.
Biblia haizungumzii maswala ya utawala na uongozi.Kama unaona maneno yangu si kweli jaribu kuleta code of leadership in the Bible kama utaiona.
Angezungumza kama Raia ingeeleweka ni raia kazungumza, yeye kazungumza kama kiongozi wa kanisa, sasa iweje kiongozi wa kanisa ahubiri mambo amabayo yako nje na yaliyo ndani ya kitabu chake kitakatifu?
Soma kitabu cha "100 most influencial persons in History' by MIcahel Harte, huyo ni mwandishi, mwanasheria, ni mtafiti na pia ameonesha wazi kwamba mission ya Jesus ilikuwa pure spiritual.
Sielewi kwa nini unapata taabu kuelewa kwamba kila mtu anatakiwa kuwa na scope ya anayoyafanya na kuyasema kutokana na capacity yake.Kwani hutambui kwamba viongozi wa dini wana mipaka?ama unaamini wanaweza kusema lolote kwa kivuli cha dini?
Kesho Shehe wa Kiislamu akianza kuhubiri mambo ambayo hayapo ndani ya Uislamu kwa kivuli cha dini itakuwaje?
Kwa nini dini yangu ikusumbue, wewe angalia hoja zangu and prove me wrong kama unaamini hoja zangu zina makosa ili nami nione wapi hoja yangu ina upungufu.
Sikusema imeandikwa maovu yasikemewe. Nimesema hakuna sehemu inayomuamuru muumini wa Biblia akemee maovu na ndio maana nimesema the one who can prove me wrong alete ushahidi.ia nimesema Paul ameamuru ndani ya Romans kwamba 'hakuna tena sheria ya righteousness'. Biblia pia inasema 'deeds are filthy rags' sasa kama wema na uadilifu ni filthy rags mbele ya Mungu kuna umuhimu na uhalali gani wa kuhubiri uadilifu?
Huwezi kuleta ushahidi wa kisichikuwepo, ushahidi huletwa kwa lililopo sio kwa kisichopo.
Kwenye thread nyingine kuna mchangiaji mwenye signature ya quotation ya Biblia ambaye pia amesema kwamba Yesu hakuhubiri worldly affairs. Anakiri kwamba the scope does not cover hayo ya Pengo na kuna dalili kwamba huyo ni muumini wa kitabu hichohicho.
Sasa wewe prove me wrong kwa kuleta amri ya kukemea maovu na kwamba aliyyoyakemea ni maovu kwa mujibu wa maandishi. Nipe maandishi yanayowapa waumini sifa za uongozi ili tuone kama hizo sifa katoa ndani ya kitabu ama maoni binafsi.
Kama hakuna Biblical writings zinazo support aliyoyasema kuna tofauti gani kati ya maneno yake na maneno ya Mrema, ama Slaa, ama Lowassa, ama Kingunge?