Pengo la Mkapa ni kubwa sana wakati huu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,597
8,738
Magufuli hakuna mtu hata mmoja anaweza kukaa naye na kumueleza ukweli bila kuna na mahitaji binafsi.

Mzee Mwinyi: Anachojali ni mtoto wake kuwa rais zanzibar
Kikwete: Anajali mtoto na mke wake familia inatamaa haiwezi kupumzika😂. Mama Salma hawezi hata kutoa hoja masikini

Mkapa pekee ndiye alikuwa mtu anaweza kusema bila kuwa na agenda zake binafsi

Matatizo yajayo
1. Seif kule Zanzibar Magufuli atafanya nini? Mwaka huu fujo zitakuwepo waziwazi! . Tujue tu kwamba hata ukiweka polisi shughuli za maendeleo haziwezi kuendelea na polisi mitaani. Mkapa ndiyo anajua kuhusu Zanzibar na ndiyo kitu anajutia sana kwenda madaraka yake kama umesoma kitabu chake.

2. Lissu hawezi kuhogwa na kazi. Jaribio la Magufuli la kutaka kumpa kazi Lissu linaonyesha kutokujua kwamba Lissu ana wito na pesa sio shida kwake! Nafikiri Magu alikuwa hajui nguvu za huyu jamaa. Lissu anapedwa zaidi, ana kipaji zaidi, ni kijana zaidi. Hakuna kitu hata kimoja cha kipaji ambacho viongozi wa CCM wamemzidi. Lissu pekee anauwezo wa kufanya Tanzania iwe na kutofahamu. Bila Lissu kuridhika itakuwa ngumu maana kule Zanzibar na huku ni tatizo

Vilevile muda ni mdogo. Kampeni za wana CCM na makundi yataanza, makundi ya Mwinyi, Majaliwa, Jaffo na wapenda madaraka kama Mwigulu. Lakini kuna wakina Makamba na Kikwete wanaotaka mtu wao. Kikwete anataka mradi wa bagamoyo urudi na China imeendaa pesa nene sana kuchukua bandari na baadae kuifanya base ya jeshi lake.

Miaka mitano itakuwa michungu sana vilevile upinzani unaongezeka kichinichini na teknologia inafanya habari zifike kwa haraka kila mahali mradi wa kuzuia habari wa usalama wa taifa umeshindikana tayari. Pamoja na kubanwa Watanzania wengi wanapenda uhuru kuliko hata maendeleo.

Pengo la Mkapa ni kubwa maana ataenda kwa nani? Mtu pekee mwenye uwezo wa kumwambia Magufuli ukweli aliyebaki ni Karume lakini hawajazoeana kabisa
 
Back
Top Bottom