Naileta hii unedited......
Pengo aonya uhusiano wa mapadri na wanasiasa
Imeandikwa na Martha Mtangoo, Dodoma; Tarehe: 22nd August 2010 @ 22:30 Imesomwa na watu: 16; Jumla ya maoni: 0
MAPADRI nchini wameaswa kutodanganywa na wanasiasa wenye lengo la kujipatia mali.
Mwito huo ulitolewa jana mjini Dodoma na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo wakati wa kilele cha maadhimisho ya kongamano la mwaka wa upadri.
Askofu Mkuu huyo alisema Tanzania ina vyama vingi vya siasa na kuwataka mapadri wasitumie vyama hivyo vya siasa katika kuwasaidia maskini kwani ni hatari, ila wahubiri habari njema za ukombozi wa Yesu kristo.
Alibainisha kuwa endapo padri yeyote hapa nchini atajiunga na wanasiasa atakuwa hana akili.
Alifafanua kuwa ni vyema mapadri wasidanganyike wala kurubuniwa na wanasiasa kama ilivyokuwa kwa mapadri wa nchini Rwanda ambao walisababisha maafa mwaka 1994 na hivyo kuishia gerezani.
Alisema baadhi ya mapadri hao wa Rwanda walikubali kuburuzwa na wanasiasa hao kwa ajili ya kutaka kujipatia mali na hivyo kusababisha maafa kutokana na ujinga wao.
Alifafanua kuwa ni dhahiri kuwa mapadri hao chimbuko lao halikuwa la upadri kutokana na wao kukubali kudanganywa na wanasiasa hao wapumbavu hali ambayo imesababisha mapadri wote kudharauliwa na kuonekana hawana maana kwa ajili ya vitendo vyao viovu.
Naomba kuwasilisha