Pengo aonya uhusiano wa mapadri na wanasiasa Imeandikwa na Martha Mtangoo, Dodoma; Tarehe: 22nd August 2010 @ 22:30 Imesomwa na watu: 16; Jumla ya maoni: 0
MAPADRI nchini wameaswa kutodanganywa na wanasiasa wenye lengo la kujipatia mali.
Mwito huo ulitolewa jana mjini Dodoma na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo wakati wa kilele cha maadhimisho ya kongamano la mwaka wa upadri.
Askofu Mkuu huyo alisema Tanzania ina vyama vingi vya siasa na kuwataka mapadri wasitumie vyama hivyo vya siasa katika kuwasaidia maskini kwani ni hatari, ila wahubiri habari njema za ukombozi wa Yesu kristo.
Alibainisha kuwa endapo padri yeyote hapa nchini atajiunga na wanasiasa atakuwa hana akili.
Alifafanua kuwa ni vyema mapadri wasidanganyike wala kurubuniwa na wanasiasa kama ilivyokuwa kwa mapadri wa nchini Rwanda ambao walisababisha maafa mwaka 1994 na hivyo kuishia gerezani.
Alisema baadhi ya mapadri hao wa Rwanda walikubali kuburuzwa na wanasiasa hao kwa ajili ya kutaka kujipatia mali na hivyo kusababisha maafa kutokana na ujinga wao.
Alifafanua kuwa ni dhahiri kuwa mapadri hao chimbuko lao halikuwa la upadri kutokana na wao kukubali kudanganywa na wanasiasa hao wapumbavu hali ambayo imesababisha mapadri wote kudharauliwa na kuonekana hawana maana kwa ajili ya vitendo vyao viovu.
Mkuu Kanda2 umemaliza kila kitu alichosema Pengo ni kweli kabisa kwani bwana Slaa anataka kuleta machafuko.amefanya machafu yake kanisani anaona haitoshi na sasa anataka kuwagawa watanzania kwa kupitia Chadema. cha ajabu kule Karatu katafuta Padri mwingine ndiye kamkabidhi jimbo lake.kwanini asitafute mtu ambaye hana msimamamo wa madhehebu yake? Slaa sio muadilifu.asikilize ushauri wa Pengo.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kadinali Pengo, amewaonya viongozi wa dini na waandishi wa habari wasikubali kutumiwa na wanasiasa wapumbavu.
Alisema kama viongozi wa dini na waandishi wa habari hawataikwepa mitego ya wanasiasa hao hasa katika kipindi cha uchaguzi, taifa linaweza kutumbukia kwenye maafa makubwa kama yaliyotokea nchini Rwanda.
Onyo hilo alilitoa jana mjini hapa, alipokuwa akihubiri kwenye kilele cha kongamano la mwaka wa mapadri wa Kanisa Katoliki lililofanyika kwenye uwanja wa hijja wa Mbwanga.
Kongamano hilo ambalo lilifanyika kwa muda wa siku tatu katika Chuo Kikuu cha Dodoma na jana kilele chake kuadhimishwa katika uwanja huo wa Mbwanga liliwakutanisha mapadri na maaskofu wote wa kanisa hilo waliopo hapa nchini.
Pengo alisema kuwa si nchi ya Rwanda peke yake ndiyo yenye wanasiasa wapumbavu, hata Tanzania kuna wanasiasa wa aina hiyo wanaoweza kuwarubuni mapadri na kuwafanya washiriki katika matukio mbalimbali ya kisiasa ambayo yanaweza kuleta maafa kwa taifa.
Alibainisha kuwa wanasiasa wapumbavu waliwateka mapadri nchini Rwanda mwaka 1994 na kujihusisha katika mauaji ya halaiki nchini humo yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja.
Askofu Pengo alisema kutokana na kushiriki katika maovu hayo, baadhi ya mapadri walifungwa magerezani kutokana na tukio hilo la kinyama ambalo halimpendezi binadamu na Mungu.
Alisema kufungwa kwa baadhi ya mapadri hao ambao ni wenzao kusiwe sababu ya kuchafuka kwa mapadri wote duniani na kuonekana kuwa kazi yao haina maana.
Kadinali Pengo alisema kuwa kumekuwa na maneno ya kuwaondolea thamani mapadri na kutaka watu wasiwasikilize kwa kusema kuwa wao ni kati ya watu wanaoshiriki katika kuleta maafa na ndio maana mapadri wengine wamefungwa magerezani.
Mauaji hayo ya halaiki yaliyofanyika nchini Rwanda hayakuanzishwa na mapadri kwani mapadri hao walirubuniwa na wanasiasa wapumbavu ambao hata hapa nchini Tanzania wapo, cha msingi ni kujiepusha nao, alisema.
Askofu huyo alisema padri yeyote atakayejiunga na kushirikiana na wanasiasa atakuwa mpumbavu kama walivyo wanasiasa wapumbavu.
Aidha Pengo aliwataka viongozi wa dini kutovunjika moyo na kauli za kuwakejeli na badala yake waendelee kuhubiri habari njema kwa maskini na matajiri kwa kupiga kelele katika nyakati zinazofaa na zisizofaa.
Pengo alisema kuwa kazi ya mapadri na maaskofu ni kuhubiri Injili na habari njema kwa watu wote na si kushiriki katika masuala ya kisiasa ambayo wakati mwingine yamekuwa yakisababisha kuvunjika kwa amani ya nchi.
Alisema si lazima kiongozi wa dini kila anapohubiri apigiwe makofi ndipo atakuwa amefanya vizuri bali uzuri wa kazi yao unaweza kuonekana wakati wowote.
Alibainisha ni busara kwa mapadri na maaskofu kutotafuta matokeo ya haraka bali wawe na subira kwa kila jambo wanalolifanya.
Mapadri msidanganyike, endeleeni kuhubiri habari njema za wokovu kwa watu wote kwani msipopiga kelele nyie hata sauti iliayo nyikani itapiga kelele, alisema Pengo.
Naye Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma Yuda-Tadei Rwaich, amevitaka vyombo vya habari kutotumiwa na wanasiasa kupotosha jamii wakati huu wa kuelekea kipindi cha uchaguzi. Alisema kuwa vyombo vya habari wakati mwingine vimekuwa vikitumika kama chambo katika kupotosha jamii kutokana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa na wanasiasa hao kipindi chote na hasa nyakati hizo za uchaguzi. Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na mapadri na maaskofu kutoka katika nchi nzima ya Tanzania ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka lengo lake kuu katika mwaka huu wa mapadri ni kuwa mapadri kuwa ishara ya matumaini mapya katika ulimwengu wa leo
Dr. Slaa alishatoka huko. Kwake ni sawa kujishughulisha na siasa. Kardinali alikuwa akionya wale wanaotoa bado huduma ya kipadre kwamba wasijihusishe na siasa kwani kwa kufanya hivyo wataweza kuwagawa waamini ambao ni wanachama wa vyama mbalimbali. Wao ni wachungaji wa wote kuegemea chama fulani kutaleta mgawanyiko Kanisani kwa misingi ya itikadi. Kumbe wao wanatakiwa kuwa neutral.
Wewe ndo umeelewa mada. Mada hii ya Pengo. Sio Pengo tu, viongozi wa dini zote wanapaswa kuwaasa wachungaji wao, maimamu sijui na nani wanaohudumia kondoo wa Mungu watofautishe imani na siasa. Viongozi wa kiroho wakijiambatanisha na baadhi ya vyama watawagawa waamini wao pia, na hiyo itakuwa hatari.
CHAMA,
Kama Slaa aliukana upadre na akaozeshwa na Papa!! ajabu Papa amuozeshe Padre! any way lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa First lady wetu mtarajiwa yaani mama Slaa yeye ni kiongozi wa CCM huku mumewe ni CHADEMA!! sasa huenda tukawa na Rais CHADEMA na first lady CCM! hapo patamu maana ndio mseto wenyewe huo!
Una mawazo ya kizamani kweli. Kwanza jisahihishe umesikia wapi papa anaozesha????? Mawazo finyu. Fungua macho utoe ushamba wako. Miaka 50 iliyopita ungezungumza hivyo tusingekushangaa. Leo katika ulimwengu wa sanyansi na technolojia ya utandawazi uzungumzapo hivyo utaonekana mbumbumbu. Pili first lady mtarajiwa yupo chama cha mumewe. Hata asingekuwa mbona hakuna uhusiano wa ndoa yao na siasa? Kazi kwako.....
chama,
kama slaa aliukana upadre na akaozeshwa na papa!! Ajabu papa amuozeshe padre! Any way lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa first lady wetu mtarajiwa yaani mama slaa yeye ni kiongozi wa ccm huku mumewe ni chadema!! Sasa huenda tukawa na rais chadema na first lady ccm! Hapo patamu maana ndio mseto wenyewe huo!
Sina maana hiyo mkubwa haimaanishi kuwa kila kitu kilicho taaluma si wito ila kuna mambo ambayo ni wito na pia ni taaluma. Kimsingi usiingie zaidi katika wanasiasa ambao wanashindwa kuyatekeleza matakwa ya walimu, manesi na Matabibu na kusema kuwa ni wito na ukiwauliza kwanini siasa isiwe wito hawatakujibu na kubwa zaidi kuwa wito, shughuli yoyote inategemea na unavyodefine I mean from which perspective!
Kadinali Pengo ni alichoongea ni sahihi lakini amesahau kuwakumbusha mapdri wawe mstari wa mbele kukemea maovu kama vile rushwa, wizi na ubadhirifu. Lamsingi mashahe na mapadri wasijihusishe na siasa bali wanapaswa kukemea maovu; hasa ukitilia maanani wanasiasa wote wa Tanzania (ukiachia Ngombale Mwiru na Paul Sozigwa ) wana imani za kidini. Kadinali anatakiwa kuwa muwazi vinginevyo itaonekana anampiga vijembe Dr. Slaa kwa hofu iliyopo ya ukatoliki na mgombea Slaa. Bahati nzuri udini hauna nafasi kwenye siasa za Tanzania.
]Hacha[/B] uongo Dr. Slaa ana Phd ya Canon Law, PhD (JCD) Law (Doctor of Canon Law) nenda kafuatilie ujue hiyo canon law ina husu nini sio unatetea husichojua.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.