Pendekezo: Waziri anayeshughulikia Misaada ya Kigeni

Pendekezo: Waziri anayeshughulikia Misaada ya Kigeni

Misaada ya Kigeni ina sehemu Kubwa Sana katika uchumi wetu. Hii ni kweli kiasi kwamba bajeti yetu huwa inaandaliwa ikipigia hesabu misaada hii ya moja kwa moja ya bajeti. Wanaotupa misaada wana vyombo vyao vinavyosimamia na hata Mawaziri au Manaibu Waziri. Sote tunajua vyombo Kama USAID, DANIDA, SIDA, CIDA (imebadilisha Jina nadhani), na JICA nikitaja machache ni taasisi za nchi mbalimbali zinazosimamia misaada kwenda nchi nyingine.

Je, umefika wakati na sisi tuwe na chombo rasmi kinachoratibu na kusimamia misaada inayoingia na kutoka (Kama tuliyopeleka Msumbiji?)? Je, kwa vile misaada ya kigeni ni sekta rasmi na yenye mchango mkubwa unaostahili Waziri kamili hata Kama ni ndani ya Ofisi ya Rais? Je, kutakuwa na faida au hasara gani tukiwa na sera rasmi ya misaada ya kigeni na Waziri mwenye kusimamia sera hiyo?

Au tuendelee tu hivihivi(maintain the status quo) yaani bila kuwa na sera au mtu (point person) anayeweza kuulizwa na kujibu? Je, wizara ya Mambo ya Nchi za Nje inatosha baadhi ya wahisani wameweka International Development Kama cabinet level ministry.Tusiwaige?
Tuwakumbushe watawala wa Afrika kuwa kushika hatamu hakukufanyi ugeuke kuwa
1. injinia,
2. daktari bingwa,
3. mhasibu mbobezi,
4. mwanasayansi wa viwango vya NASA
5. au mtaalam zaidi!

Therefore your power doesn’t suddenly increase your knowledge or qualify you to be anything more than you were! Waache u-much-know na upumbavu, wawe humble!
 
Back
Top Bottom