Pendekezo: Waziri anayeshughulikia Misaada ya Kigeni

Pendekezo: Waziri anayeshughulikia Misaada ya Kigeni

Unasemaje?
JamiiForums285286567.jpg
 
Sasa wakati umefika kufanya hili liwe kweli.... Trade not Aid....
Hata kama ni biashara, utafanyaje kwa akili kama zenu CCM.

Mpaka leo tuna uchumi wa kikoloni, tunasafirisha malighafi na kununua finished goods mpaka sindano.

Wawekezaji wa maana aka Mabeberu hatuwataki, tunataka wachina ndio ndugu hawatukisoi wala kutukemea tukiua watu wetu.
Hao wachina wetu wanawekeza kwenye Mabonanza aka makorokoro
 
Mzee Mwanakijiji
Huu ni wakati wa kuchapa kazi tujenge nchi kwa pesa zetu za ndani.
Mabeberu hawatutakii mema. Mitano tena.
Acha Mara moja kujimwambafai ,uchape kazi na kujenga Nchi kwa pesa zako mwenyewe, Yapo mataifa yamesimama ila bado yanahitaji kushikwa mkono na mataifa mengine,Sasa wewe una nini mpaka uwe na kiburi? ndugu zangu wabondei ndo hapo wakwambiapo huna lolote, Yani mjenge nchi kwa pesa zenu wakati COVID 19 tu mnakimbilia misaada badala ya kutoa misaada. Acheni wakuu kupenda jitoa ufahamu.
 
Umejuaje biashara za ndani "zinazidi kufa"?
Najua haupo Tanzania. Ngoja nikushauri siku Njoo Tanzania, ukishuka airport nenda hadi quality centre, then ukitoka nenda mkuki tower , ukimaliza Njoo posta mtaa wa Samora tu tembelea mwanzo hadi mwisho fanya survey ya maduka na biashara ikoje.

Utakuwa umepata jibu ya ulichouliza
 
kwa wasiomjua M.M.Mwanakijiji alikuwaga mtetezi wa haki za binaadam na Demokrasia. Kumbe ilikuwa zuga tu ilikuwa ni vita dhidi ya Jakaya. Wakipigana na Slaa na kanisa katoliki. Sasa haki za binadamu zinazingatiwa mpaka zinamwagika ndiyo maana anazungumzia misaada.
 
kwa wasiomjua M.M.Mwanakijiji alikuwaga mtetezi wa haki za binaadam na demokrasia. Kumbe ilikuwa zuga tu ilikuwa ni vita dhidi ya Jakaya. Wakipigana na Slaa na kanisa katoliki. Sasa haki za binadamu zinazingatiwa mpaka zinamwagikia ndo maana anazungumzia misaada
Usimpake matope mwenzako.
 
Misaaada?

Sisi ni 'Dona Kantri' hatutaki misaada ya Mabeberu.

Hapo ulipo simama na tembea kifua mbele.
 
Wazo zuri na linatakiwa kufanyiwa kazi. Kwa wizara ya fedha wao wana- Commission mbali mbali kabisa zinazo shugulikia misaada muhimu..

Mfano: Commission for Billateral Aids, commission ya misaada mbali mbali.

Wazo zuri sana.
 
Back
Top Bottom