Pendekezo: Uchaguzi mkuu ukiahirishwa kambi rasmi ya upinzani bungeni waunde serikali ya mpito

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Kama uchaguzi wa Octoba 2015 utaahirishwa kwa sababu ya kutokamilika kwa zoezi la kuandikisha wapiga kura, pendekezo linatolewa hapa kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni (KUB), ambayo inaundwa na UKAWA waruhusiwe kupitia mchakato wa maridhiano ya kitaifa kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi mkuu.

Msingi wa pendekezo hili ni kwa vile hakuna sababu yoyote ya tume ya uchaguzi ya taifa kushindwa kumaliza kuandikisha wapiga kura kwa sababu kunasheria inayoitaka tume hiyo kuandikisha wapiga kura mara kwa mara kila baada a kipindi fulani. Kusubiri kuandikisha wapiga kura dakika ya mwisho karibia na uchaguzi kunatafsiriwa kama kushindwa kutimiza wajibu na hivyo UKAWA waokoe jahazi kwa kuongoza nchi kuelekea kukamilisha zoezi la uchaguzimkuu utakaokuwa umeahirishwa (msisitizo ni kuwa kama uchaguzi utaahirishwa kwa sababu ya kushindwa kukamilisha zoezi la kuandikisha wapiga kura kabla ya Octoba 2015).
 
Pendekezo hili litawafanya serikali na NEC yake kuwajibika ipasavyo kuandikisha wapiga kura kila baada ya uchaguzi mkuu.
 
sijaelewa yaani ccm akae pembeni kuangalia ukawa anavopaform au waunde mseto
 
Na imagine akina Nkuruzinza Watanzania itakuwaje.Na yale magari 700 ya polisi yqtapelekwa wapi?
 
Kiasi inaweza kuwapima waongeaji kama kweli ni wazalendo paletu wawapo ktk serikali je rushwa, ufisadi utakoma walau kwa kipindi kifupi? natamani iwe hivyo hata kwa miaka 2tu uzalendo uonekane kwa nafsi za watu
 
sijaelewa yaani ccm akae pembeni kuangalia ukawa anavopaform au waunde mseto
Nina maana kuwa CCM wakae pembeni ili UKAWA wachukua madaraka ya kuongoza serikali ya mpito maana CCM watakuwa wameshindwa kutimiza majukumu ya kuandaa uchaguzi mkuu.
 
Kiasi inaweza kuwapima waongeaji kama kweli ni wazalendo paletu wawapo ktk serikali je rushwa, ufisadi utakoma walau kwa kipindi kifupi? natamani iwe hivyo hata kwa miaka 2tu uzalendo uonekane kwa nafsi za watu
Sawa, UKAWA wanaweza.
 
Back
Top Bottom