KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,150
- Thread starter
-
- #461
Chama cha siasa kisipokuwa na ndoto ya URAIS hakipaswi kuendelea kuwepo. Hakifai. Wakigeuze kiwe NGO kama TAMWA ya Mama Nkya.
Dr Slaa tayari ana kazi kubwa na nzuri tu. Arumeru haijapungukiwa vichwa vya UBUNGE. Ubunge hauhitaji watu wa kukodi. Uliona Mrema hakumaliza kipindi chake cha Ubunge pale Temeke. Hakujali waliompigia kura. Aliondoka kihuni tu. Hawezi kufanya hivo kwao Vunjo.
KK,kwa hiyo unataka kusema sugu nae ataondoka kihuni mbeya mjini kama mrema temeke sio?
Kuhusu urais usikunyime usingizi mzee,unaweza kuwa rais lakini bila serikali sasa sijui huo urais utakuwa na faida gani?ndio mana tunawaambie mfunguke mpanie kuichukua serikali sio urais,urais ni kitu kidogo sana,ambacho kitakujachenyewe mkiweza kuunda serikali.
KIM KARDASH
- ulisha sikia katibu mkuu wa CCM ni mbunge - CDM ni chama tawala cha upinzani na katibu mkuu anazo kazi za kufanya
- kazi ukiianzisha si rahisi kuimalizia mwenywe wapo wanao kuunga mkono wataimalizia kwa techniques mpya kama ikina Tundu Lissu, Godbless Lemma, Sugu etal
- TFFA ina rais . Rais ni kiongozi wa watu na huwezi kuwazuia wanao mwita rais kumbuka yeye hajiiti kama Rais sijui kinacho kuuma nini
- Basi huo msamiati usengekuwepo kama kura haziibiwi
- hili ndilo lililo mwangusha Mpesya aliroka kuwa vijana wengi ni mashabiki tu na hawapigi kura na kwambia safari hii wapiga watakuwa hawa unao wadharau maadamu daftari liboreshwe utaona
SIIUNGI MKONO HOJA DR SLAA ASIGOMBEE UBUNGE
KK,
Mr Sugu ni mwenyeji wa Mbeya! Lile jina Mbilinyi lisikufanye umpeleke Songea. Hauwezi kuwa Rais bila serikali. Unautenganishaje Urais na serikali? Uelewa wako wa mambo haya unatosha kweli! Arumeru ina vichwa vingi vizuri kuliko huyo Dr Slaa.
Nashukuru kwa msaada wako Duble Cris, nilikuwa najiuliza jinsi ya kumuelewesha hu Kim Kadash. Hoja yake ni dhaifu sana sana tu, mie nahofia anatumikia upande flani hivi wa kushoto. Tunamuomba sana dk Slaa asigombee ubunge ubunge Arumeru Mashariki sababu bado ana nafasi yake yake ndani ya mioyo yetu. YEYE NI RAIS AJAYE.
Ndio maana nikakueleza sifa mama za kuupata Ubunge majimbo mengi nchi hii ukiondoa yale ya miji mikubwa kama Dar:Bwana mzee mbeya hawakuwa na hiyo huko nyuma,marehemu Bruno mpangala angekua hai ningekutuma ukamuulize,yeye kiasili alikua anatoka mkoa mmoja na kabila moja na sugu lakini alikua mwenyeji wa mbeya pia kama sugu,lilipokuja suala la ubunge akachukua fomu ya kugombea ubunge pale mbeya mjini(kumbuka alikua katibu mkuu wa ottu taifa)hivyo alikua ni mtu mwenye ushawishi lakini wanyakyusa wakasema hapana hata ccm wenzake hawakumpigia kura,wote wakampigia mnyakyusa mwenzao bwana Mwaisyeje aliesimama kwa tikiti ya NCCR mageuzi ya mrema,hiyo ndio mbeya nilioifahamu,lakini watu wanabadilika,alipokuja sugu kamshinda mzawa japo hakua mnyakyusa,alikua ni msafwa ambao kiasili kabisa ndio wenye mbeya yao,tena kukuonyesha kwamba nakijua zaidi ninachosema sugu alimshinda mwalimu wake wa literature pale mbeya secondary bwana Mpesya!
Narudi kwenye mada kama sugu kaweza kuivunja mizizi mizito ya ukabila pale mbeya ambapo hapakuwahi kutokea mbunge asie mzawa wa pale itakua slaa mwenye muscles za kutosha,slaa ni heavy weight politician miongoni mwa wagombea wote watakaosimamishwa arumeru,labda lowassa agombee ndio wanaweza kulingana kitu ambacho hakiwezi kutokea cuz lowassa tayari ni mbunge
siungi nkono hoja.Nassari apewe haki yake.Slaa ana kazi kubwa ya kuimarisha chadema nchi nzima akijiandaa kukamata dola 2015
ndio maana nikakueleza sifa mama za kuupata ubunge majimbo mengi nchi hii ukiondoa yale ya miji mikubwa kama dar:
-uwe mwenyeji wa jimbo husika. Dr slaa hana sifa hii kule arumeru.
-sifa yako mwenyewe. Mr sugu alikuwa celebrity na chadema ya dr slaa 2010 iliwakamata wamachinga wengi wa mijini.
-dini nayo inashika kasi siku hizi.
Kk, ubunge wa dr slaa kule arumeru utaisaidia nini chadema na nchi yetu? Nyongeza ya ruzuku?
Najua Mwalimu KK lakini sio kwa TANZANIA. Katiba yetu ya sasa haisemi hivo! Ila Rais atalazimika kumteua Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi. Hawa wawili kwa kushauriana wataunda serikali.kwa hiyo huoni umuhimu wa upinzani kuongeza viti bungeni sio?basi kazi ipo.sasa ndio nimekuelewa kwanini hunielewi ninaposema muhimu ni serikali sio urais.
Ok kwa kuwa mimi ni mwalimu kitaaluma ntakuingiza darasani kwanini nasema serikali ndio muhimu kuhusu urais,hapa ni suala la mahesabu tu,unajua kwamba chama chenye wabunge wengi ndio kinaunda serikali?pengine tuanzie hapo kwanza ndio tutaenda sawa..unalifahamu hilo?
kwahiyo urais hakuna vichwa huko chadema mwenye akili ya kuwa rais ni yeye tu?Mi naomba nipingane na wewe. Nimshauri Dr. afokas kwenye mbio za urais na harakati nyingine za Chama. Kugombea jimbo hilo ataonesha ana uchu wa madaraka coz there others who can stand for that post. He better stays behind
Najua Mwalimu KK lakini sio kwa TANZANIA. Katiba yetu ya sasa haisemi hivo! Ila Rais atalazimika kumteua Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi. Hawa wawili kwa kushauriana wataunda serikali.
Majimbo ya Dar ni "No man's land", kama hicho ni kiingereza sahihi. ARUMERU ni ngazi nyingine kabisa. Hata wilaya na majimbo yenyewe unaona majina yake. Tusifichane bwana. Nchi hii Ubunge na Udiwani vigezo hivi ni muhimu sana ukiondoa majimbo ya miji mikubwa ya Dar, Mwanza na Arusha. Narudia, vigezo vizito vya Ubunge wa Arumeru Mashariki ni:
-Uwe Mmeru wa koo kama Kaaya, Ndosi, Pallangyo...
-Uwe Mlutheri. Ukatoliki kama wa Dr Slaa ni kikwazo tosha.
-Lowasa anakufahamu?
Acheni Dr Slaa aendelee na kazi yake ya kukiimarisha chama chake. Hana wabunge waasi kama alookuwa nao Mrema mwaka 1995 kule NCCR-M.