Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,710
- 36,166
Habari!
Nitatoa sababu mbili tu muhimu kwanini RAIS wa TUCTA na katibu wake wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi.
1. Wanaonyesha dharau kwa RAIS SAMIA.
Miaka 6 ya utawala wa Magufuli hapakuwa na kupanda madaraja kwa watumishi wala ongezeko la MISHAHARA.
Samia ndani ya miezi 3 tu alipandisha madaraja watumishi wengi sana kuanzia kwenye majeshi mpaka kwenye taasisi zingine.
Kupandisha madaraja au vyeo kumetumia mabilioni. Mbona kipindi cha Magufuli hawakuwezi kutoa kauli yoyote?
Ni heri Rais SAMIA aliyewakumbuka wale wa kima cha chini ingawa ni kwa kidogo.
2. Bilioni takribani 700 kila mwezi zinatumika kuwalipa watumishi. Endapo serikali ikiongeza MISHAHARA kwa asilimia 15-23.3 kwa watumishi wote pamoja na wale wanaolipwa zaidi ya milioni 1 hapo ni dhahiri kuwa makusanyo ya nchi hii 70%-80 yatatumika kuwalipa watumishi tu. Hii ni haki?
TUCTA wangeishauri serikali ipunguze watumishi ili watakaobaki waongezewe maslahi. Hapo serikali haitaelemewa.
Juzi tu posho za viongozi au watumishi waandamizi zimeongezwa kwa zaidi ya 100%, hivi kuna haja tena hawa viongozi na watumishi waandamizi kuongezewa mshahara?
Nakazia: RAIS wa TUCTA na katibu wake wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi.