Pendekezo: Naomba shule zifunguliwe baada ya zile siku 30

Pendekezo: Naomba shule zifunguliwe baada ya zile siku 30

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Kwanza nianze na pongezi kwa viongozi wetu wa nchi, waziri wa afya na wataalam wote washauri kuhusu hili suala la janga la Corona. Kwa kweli katika kipindi hichi cha tatizo, nimejivunia sana nchi yangu.

Mengi yamesemwa, tumeandika na yameshauriwa humu.

Natambua mlikuwa katika nyakati ngumu pengine kufanya maamuzi njia ipi itumike maana jambo ni geni na kila nchi ilitumia njia inayoona inafaa. Hiyo ikatoa nafasi kwa kila nchi kujifunza makosa ya wengine huku wakiangalia mazingira.

Kuna kitu kinashangaza hasa kwa baadhi yetu wananchi. Tumekuwa tukieneza hofu na hata kulaumu kwa kila kinachofanyika.
Tusichokijua ni kuwa, japo sisi ni nchi ya dunia ya tatu au masikini kwa lugha rahisi lakini kitengo chetu cha kuhudumia magonjwa ya milipuko kipo vizuri na wana uzoefu wa kutosha pengine kuliko nchi nyingi (najua kuna watu watabisha, na waendelee kubisha). Ninawapongeza sana sana wataalam wetu.

Tanzania kama nchi imekuwa ikikumbwa na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, dengue na mengineyo. Magonjwa haya yanapotokea huwa yana fatiliwa na taarifa sahihi zinafikishwa kwa wafanya maamuzi na hatua kuchukuliwa.

Sasa hapa kuhusu ugonjwa corona kuna watu wanajidai wanajua kuliko serikali. Mtu anasema kuna wagonjwa wa covid 19 wamefichwa, wakiulizwa wako wapi wawaonyeshe wanajificha. Hivi kweli mtu mgonjwa kazidiwa anaweza kuficha?

Hadi sasa katika mazingira yetu Tanzania imechukua njia bora kabisa kupambana na covid 19. Njia hizo ni: kutoa elimu, kutenga wanaotoka nchi zenye ugonjwa, kupima na kuwatenga wagonjwa nk.

Njia hizi kuna watu wanaona hazitoshi lakini njia bora kabisa kwa mazingira yetu.

Kuhusu kufungua mashule, hebu tuangalie nchi kama ya Sweden. Wao wakati majirani zao Norway na Denmark wao hawakufunga shule zao. Waliendeleza shule isipokuwa waliwapa walimu mamlaka ya kufuatilia na kuangalia hali za wanafunzi ikiwa wakibaini chochote watoe taarifa. Na sisi tunaweza kuweka utaratibu mzuri kwa mashule hasa tukihimiza usafi na kufuatilia hali za wanafunzi.

Vile vile hata suala la kupima kila mtu, Sweden wameachana na utaratibu huo, wanashughulika na wazee na wale ambao ni wagonjwa haswa. Angalia, maisha yanaendelea vizuri Sweden na hakuna kinachosumbua.

WHO na wakubwa kadhaa wa dunia walitabiri kuwa ndani ya wiki 2 hadi mwezi Africa itakuwa na hali mbaya. Kwanza tunashukuru Mungu halijatokea, maana hadi sasa tangu nchi nyingi za Africa zipate mgonjwa wa kwanza ni zaidi ya wiki tatu sasa na haukuna ile 'wave death' kama ya nchi za Ulaya. Hata hapo South Africa tu hawajafikia hapo. Hivi kwa wale ambao wanafata mkumbo, who knows kama taarifa hizi zinazotolewa ni hizo hizo za vifo vya influenza ambavyo hutokea kila mwaka ambazo zinaua watu wengi sana Ulaya na America kila mwaka?

Raisi Museveni ameshashtuka kuhusu hii covid 19 na i think soon Uganda will come to normal.

Tusiache kufungua shule maana kwa hatujui janga hili litaisha lini lakini tunachojua tu kuwa janga sio as deadly as other diseases ambayo yanatusumbua na kupoteza watanzania wengi kila mwaka.
 
Nionavyo Mimi shule za boarding zitakuwa salama iwapo walimu watakeep distance wakati anafundisha maana wao ndo wanaingia mtaani na kurudi shule,Ina maana mwalimu anaekohoa au mafua asiingie kufundisha na tahadhari za kunawa mikono zifaatiliwe,

Kw shule za kutwa ishu iko katika wanafunzi kusafiri kwenda na kurudi shule kila siku,

Kwa shule za mikoani za kutwa wanafunzi hutembea,hivyo Hilo SI tatizo,
Huu ugonjwa kwa huku bado uko stage za mwanzo na hakuna uhakika Kama utalipuka au utakuwa mild,

So wafungue mashule ama wasifungue Ni kitendawili
 
Kuna mtu nimesikia anasema kuwa ratiba iliyopo hadi sasa ni hadi tar. 4 mwezi wa tano. Hizi si taarifa rasmi ila nimesikia tu kwa mtu.
Tusubiri tuone wataamua nini.
 
subiri tunatumia hosteli kwanza
 
Kuna mtu nimesikia anasema kuwa ratiba iliyopo hadi sasa ni hadi tar. 4 mwezi wa tano. Hizi si taarifa rasmi ila nimesikia tu kwa mtu.
Tusubiri tuone wataamua nini.
Wenzetu Israel wamefunga mashule mpaka September 1,Ina maana mwaka mmoja wa masomo umepotea,,
 
Back
Top Bottom