Pendekezo: Mbunge au Diwani akiachia ngazi,chama kilekile kiteue mbunge/Diwani mwingine

Bora uwe mbunge au diwani wa kujitegemea kuliko kuwa wa chama flan utakumbana na bakora ya ma -Rc wanaotaka uunge mguu itikadi na falsafa za Mimi ndio mahakama hakuna nyioro wala vyoro
 
Wanabodi,

Bunge la Tanzania,kwa nn msipeleke mswada bungeni kuweka kipengele cha kufutwa kwa chaguzi ndogo,badala yake iwe chama kilichoondokewa na kiongozi wake,iwe kwa kufa,kufukuzwa au kujiudhuru,kiteue kiongozi mwingine na kisha tume imthibitishe. Hii itapunguza gharama hizi za kipuuzi. Na nna uhakika sheria hii ikipitishwa,hakuna mbunge wala Diwani atakayeachia ngazi...!!

Nawasilisha.
Naunga mkono hoja.
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.

Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
P
 
Hoja maridhawa,kwa upande wangu nahisi mtu akijiuzuru aliyemfuatia kwa idadi ya kura apewe. Mfano CDM 1996, CCM 1905,ACT 369, basi achukue huyo mwenye kura nyingi na chaguzi ndogo marufuku.
Hiyo haitasaidia kama (mfano) CUF ilikuwa ya kwanza na kura 5,000 na ACT ya pili kura 4,000 ni rahisi kwa ACT kwenda kumnunua wa CUF ili wapachukue pale kwani wanajua automatic wao ni wa pili watachukua kiti!Piga picha Kuubwaaaa hapo,nadhani umenielewa,watu wanaweza kuuana wa pili ikimuwinda aliyekuwa wa Kwanza.Hili wazo lililoletwa ndilo mwarobaini wa yote.
 
Michingo yenu wote ni mizuri hakuna kinachoshindika,ukiangalia katiba Rais au Makamu wa Rais wanapo ondoka madarakani kunafanyika mabadiliko wa kupanda cheo au kuteuliwa mwingine. Alipofariki Dr. Omar Juma aliteuliwa Dr Shein ikitokea Rais anafariki Makamu wa Rais anamalizia kipindi kwa kushika nafasi ya Urais. Kweli chaguzi ndogo ni upotevu wa Fedha usiofaa.
 
Hata swala la Ruzuku pia limulikwe upya vyama vijitegeme katika kujiendesha vimekwisha komaa vya kutosha
 
Wanabodi,
Salaam;

Wimbi la viongozi kuhama chama kwa kisingizio cha kumuunga mkono Rais,linaendelea.

Viongozi hawa waliochaguliwa kwa jasho na damu,wanaamua kuziacha nafasi zao na wanaenda kuomba kugombea nafasi zilezile ktk chama kingine. Mfumo huu unatuingiza kwenye gharama kubwa km Taifa.

Serikali inatumia pesa nyingi kufanya chaguzi ndogo ambazo ni chaguzi za kihuni kabisaa! Tunapoteza pesa serikalini,kwenye vyama na wagombea wenyewe. Wananchi nao wanapotezewa muda kwenda kwenye mikutano ya kampeni na kupiga kura..!

Bunge la Tanzania,kwa nn msipeleke mswada bungeni kuweka kipengele cha kufutwa kwa chaguzi ndogo,badala yake iwe chama kilichoondokewa na kiongozi wake,iwe kwa kufa,kufukuzwa au kujiudhuru,kiteue kiongozi mwingine na kisha tume imthibitishe. Hii itapunguza gharama hizi za kipuuzi. Na nna uhakika sheria hii ikipitishwa,hakuna mbunge wala Diwani atakayeachia ngazi...!!

Nawasilisha.
Wazo zuri sana! Anayeteuliwa aishike nafasi mpaka uchaguzi mkuu.
Hivi vyama vya upinzani hawawezi kufikiri na kuleta mapendekezo kama haya?
Wakati mwingine natatizwa na nia/ madhumuni ya upinzani kama yana dhati ya kutetea na kulinda nchi au na wao ni kujitengenezea ulaji tu kama watawala.
 
Yaani km wabunge na Rais wangekuwa wazalendo kweli,hii sheria ingefaa sana. Huu upuuzi ungeisha kabisa,hakuna Diwani wala mbunge angejiudhuru!
Kama akiamua kujiuzulu ni kwamba imekula kwake na kuunga mkono kwao!
 
Hoja maridhawa,kwa upande wangu nahisi mtu akijiuzuru aliyemfuatia kwa idadi ya kura apewe. Mfano CDM 1996, CCM 1905,ACT 369, basi achukue huyo mwenye kura nyingi na chaguzi ndogo marufuku.
Hapana. Ingekuwa vizuri awe wa chama kile kile mbunge wake aliyejiuzulu. Hii itakomesha hii mbinu ya kijinga ya ccm kuwafuja wananchi kodi zao huku wakijinadi wanawajali wanyonge.
 
HAPANA, MGOMBEA WA UBUNGE/UDIWANI ALIYEMFUATIA KWA KURA KWENYE UCHAGUZI HUSIKA ACHUKUE NAFASI YAKE!
Mkuu,hii wala haina maana kabisa...ukifanya hivyo ccm wataendelea tu kununua wabunge na madiwani wa upinzani. Kwa sababu kwenye chaguzi zetu,kwa 99% pale ambapo upinzani umeshinda,anayefuatia kwa kura huwa ni ccm. Tena hiyo itawanufaisha zaidi...! Tufanye tu km wenzetu wa Africa ya kusini,sasa hv ANC wanamshinikiza Zuma aachie ngazi,wanajiamini kwa sababu hawaendi kwenye uchaguzi,bali ANC ndo watateua mrithi wa Zuma wa muda mpaka uchaguzi mwingine utakapoitishwa...!!
 
Hapana. Ingekuwa vizuri awe wa chama kile kile mbunge wake aliyejiuzulu. Hii itakomesha hii mbinu ya kijinga ya ccm kuwafuja wananchi kodi zao huku wakijinadi wanawajali wanyonge.
Lakini mkuu huoni kama itampa majaribu makubwa mwenyekiti,akipata mchepuko anakununua au kukufukuza tu ili ampe mwingine. Hii bora iratibiwe NEC kabisa,ujinga uishe.kabla hujajiuzuru ujijue tu kama umeua bendi.
 
No ahame na Cheo chake maana wananchi wamemchagua yeye sio Chama. Chama ni mdhamini tu!
Hoja ya kuteua kutoka ktk chama alichotoka inaweza ikapita kwani ina manufaa katoka chama cha manunuzi, ila hoja ya kuhama na ubunge/udiwani wake au hata urais ni kaa la moto kwa ccm kwani watahofia akina nape kutimkia upinzani na ubunge wao. Na kwa upande mwingine hoja hii ni ngumu kwa mtu anayejiuzulu udiwani/ubunge, ila rahisi kwa anayehama chama. Hoja hii ikipita sio ajabu hata rais akahama chama na urais wake. # Siasa hadi 2020#
 
Yes naikubali hii pia aliyejiuzulu Bila sababu za Msingi apelekwe mahakamani kutumia fedha za umma vibaya
 
Back
Top Bottom