magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,201
- 3,322
Wanabodi,
Salaam;
Wimbi la viongozi kuhama chama kwa kisingizio cha kumuunga mkono Rais,linaendelea.
Viongozi hawa waliochaguliwa kwa jasho na damu,wanaamua kuziacha nafasi zao na wanaenda kuomba kugombea nafasi zilezile ktk chama kingine. Mfumo huu unatuingiza kwenye gharama kubwa km Taifa.
Serikali inatumia pesa nyingi kufanya chaguzi ndogo ambazo ni chaguzi za kihuni kabisaa! Tunapoteza pesa serikalini,kwenye vyama na wagombea wenyewe. Wananchi nao wanapotezewa muda kwenda kwenye mikutano ya kampeni na kupiga kura..!
Bunge la Tanzania,kwa nn msipeleke mswada bungeni kuweka kipengele cha kufutwa kwa chaguzi ndogo,badala yake iwe chama kilichoondokewa na kiongozi wake,iwe kwa kufa,kufukuzwa au kujiudhuru,kiteue kiongozi mwingine na kisha tume imthibitishe. Hii itapunguza gharama hizi za kipuuzi. Na nna uhakika sheria hii ikipitishwa,hakuna mbunge wala Diwani atakayeachia ngazi...!!
Nawasilisha.