Pendekezo: Mashindano Makubwa ya kuhifadhi Kitabu Kitakatifu cha Biblia 2017/2018

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Ndugu zangu Wakristo nawasalimu. Tumsifu Yesu Kristo!

Ndugu zangu nawaomba wakristo wenzangu kwa nafasi zetu, vipawa vyetu na karama alizo tujalia Mwenyezi Mungu na sisi Tuanzishe Mashindano ya Kuhifadhi Biblia Takatifu kwa Vijana Wetu ili kuwajenga katika kulijua Neno LA Mwenyezi Mungu.

Nawasilisha ndugu zangu tuanze kampeni ya kuanzisha mashindano aya [HASHTAG]#BibliaTakatiguNuruyaUlimwengu[/HASHTAG]
 
Mkuu liliishia wapi hili zoezi. Mrejesho plz.

Thanks.
 
Ndugu zangu Wakristo nawasalimu
Tumsifu Yesu Kristo
Ndugu zangu nawaomba wakristo wenzangu kwa nafasi zetu,vipawa vyetu na karama alizo tujalia Mwenyezi Mungu
Na sisi Tuanzishe Mashindano ya Kuhifadhi Biblia Takatifu kwa Vijana Wetu ili kuwajenga katika kulijua Neno LA Mwenyezi Mungu
Nawakilisha ndugu zangu tuanze kampeni ya kuanzisha mashindano aya
[HASHTAG]#BibliaTakatiguNuruyaUlimwengu[/HASHTAG]

Kama wakristo wataanza kukariri Biblia waislamu wao watafanya kazi gani???Ukristo haukujengwa kwa kukaririshwa vitabu kichwani!!!
 
Ndugu zangu Wakristo nawasalimu
Tumsifu Yesu Kristo
Ndugu zangu nawaomba wakristo wenzangu kwa nafasi zetu,vipawa vyetu na karama alizo tujalia Mwenyezi Mungu
Na sisi Tuanzishe Mashindano ya Kuhifadhi Biblia Takatifu kwa Vijana Wetu ili kuwajenga katika kulijua Neno LA Mwenyezi Mungu
Nawakilisha ndugu zangu tuanze kampeni ya kuanzisha mashindano aya
[HASHTAG]#BibliaTakatiguNuruyaUlimwengu[/HASHTAG]

Wakristo wanaweza kuiga jambo la kumfanya mtu ajisogeze karibu zaidi na muumba wake. Kukariri Biblia ni upumbavu na haina uhusiano na imani inayomfanya mtu ampendeze Mungu. Nitashangaa nikisikia watu wanaojiita Wakristo wakianzisha mashindano eti ya kukariri Biblia. Hakuna na wala hakutakuwepo mashindano ya imani ya Kikristo ambayo mshindi ataamuliwa na mwanadamu.
 
Yesu mwenyewe ambae ndiye neno la Mungu alikuwa antumia neno "imeandikwa" haijakufundisha tuu kuwa ukristo si kukariri maneno kama yalivyo bali kujua nguvu inayoamabatana na hayo maneno na kuiyumia hiyo nguvu ukiwa na mamlaka.
Hata hivyo bado si vibaya kuijua hata ukiweza kuikariri sio mbaya ila tu usifanye mashindano. Imeandkwa " Msifanye jambo lolote kwa kushindana "
 
Wakristo wanaweza kuiga jambo la kumfanya mtu ajisogeze karibu zaidi na muumba wake. Kukariri Biblia ni upumbavu na haina uhusiano na imani inayomfanya mtu ampendeze Mungu. Nitashangaa nikisikia watu wanaojiita Wakristo wakianzisha mashindano eti ya kukariri Biblia. Hakuna na wala hakutakuwepo mashindano ya imani ya Kikristo ambayo mshindi ataamuliwa na mwanadamu.
unatoka nje ya mada. anazungumzia kuhifadhi biblia siyo kushindana imani. imani inapimwaje?
 
Labda ungesema wakristo waongeze juhudi kuwafuta wanadamu ujinga kwa kuongeza shule na mahospital kuliko kukariri biblia kuhifadhi biblia kichwani.hushangai mchungaji anaponya waumini wake lakini yeye na familia yake wana bima ya afya mkuu.!sanuka hukuona Gwajima alienda kutibiwa India babalai..
 
Kwani wakristo wanatumikia mabwana wawili mkuu...?

Kama wanapigania maslahi binafsi = kumtumikia shetani
Kama wanatumikia waumini wao pasipo kujali watalipwa ama la = wanamtumikia Mungu aliye hai
 
Back
Top Bottom