Pendekezo: Kijiji cha Makumbusho kihamishwe kutoka pale Kijitonyama jijini Dar es Salaam

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,523
27,020
Umuofia kwenu wakuu!

Kama raia wa kawaida, naleta hoja binafsi kama inavyojieleza hapo juu.

Sina nia ya kubeza umuhimu wa Makumbusho, ni vema kama Taifa kuwa kumbukizi zetu. Ndiyo maana tunayo pia Makumbusho ya Taifa pale mjini kati Posta.

Hoja yangu hapa ni ‘unyeti’ wa eneo ambalo Kijiji hiki kimewekwa, pale tunaweza kuwekeza miradi mikubwa na yenye manufaa kuliko ilivyo sasa.

Kijiji kilijengwa hapo miaka mingi iliyopita, ambapo hilo eneo lilionekana ni nje ya mji hivyo lilisadifu kuwa na ‘Kijiji’.

Kwa sasa pale ni ‘keki’ iliyonona, ni keki ya moto, serikali yangu sikivu naamini itapendezwa na wazo murua hili.

Kama lengo lake ni kumbukizi tu za mila zetu, basi kihamishiwe eneo lingine pembeni ya mji, ili pale patumike kwa miradi yenye tija zaidi kwa Taifa.

Nawasilisha.
 
Kipo sehemu maeneo ya posta, Au lile li ukumbi karibu na kirimjee jengo lake limepakana na IFM

Kama ni hapo hakuna jipya.
 
Kipo sehemu maeneo ya posta. Au lile li ukumbi karibu na kirimjee jengo lake limepakana na IF

Kama ni hapo hakuna jipya

Kivipi hakuna jipya?

Acha hayo Makumbusho ya Taifa, mi naongelea ‘Kijiji cha Makumbusho’ kilichopo pale Millennium Towers, Kijitonyama opposite na ofisi za Tigo.
 
Mkuu naunga mkono hoja yako. Vipi na huko nje ya mji kitakapo hamishiwa nako kukishakuwa ndani ya mji kihamishwe tena?

Kibaya ni gharama za kuhamisha kijiji ni za wananchi wote lakini upo uwezekano eneo likibaki tupu wanasiasa watagawana bure.

Ukiacha takwimu tunazopewa, bado kuna maeneo huduma za msingi hazijafika, hizi gharama acha zielekezwe huko.
 
HS CODE
Asante kwa kuniunga mkono!

Kuna maeneo ambayo kikihamishiwa ilimradi ni ndani ya Dar es Salaam, hatutarajii yatakuja kuwa ‘mjini’ kati... au basi tuseme miaka 50 ijayo.

Gharama za kuhamisha wala haihitaji kodi za wananchi, mwekezaji tu atasimamia kila kitu.
 
HS CODE
Asante kwa kuniunga mkono!

Kuna maeneo ambayo kikihamishiwa ilimradi ni ndani ya Dar es Salaam, hatutarajii yatakuja kuwa ‘mjini’ kati... au basi tuseme miaka 50 ijayo.

Gharama za kuhamisha wala haihitaji kodi za wananchi, mwekezaji tu atasimamia kila kitu.

Asante Mkuu. Vipi umeshawaza kuhusu suala la uhalisia?

Uhalisia wa kupatikana muwekezaji wa kutoa gharama za kuhamisha kijiji kisha ndipo atumie na pesa nyingine kufanya uwekezaji kwenye eneo litakalobaki tupu.

Huoni ataweza kuona ni bora atafute maeneo mengine yatakayotumia pesa yake yote kwenye mradi aliyo kusudia.

Pamoja na hayo, vivutio vingi vya kitamaduni vinazidi kupungua uhalisia kadiri tamaduni zinavyo zidi kubadilika.

Nina mashaka, Makumbusho ile iliyoandaliwa 1996, itakuwa tofauti sana na itakayoandaliwa 2025. Uhalisia utazidi kupotea zaidi. Tusijekujenga magofu tukakosa wa kuja yatazama.
 
Jamani kuwa mjini kati isiwe na maana tujenge jenge tu, kuna maeneo yanahitaji kupumua.
Haiwezekani upite barabara ya kilomita tatu bila kuona ukijani. Pabaki hivyo hivyo tu.

Ukijani!

Mkuu wa Mkoa anahamasisha upandaji miti hadi kando/kati ya barabara za mjini, japo tumekuwa tukimwangusha na kutokuunga mkono juhudi zake.

Binafsi wewe ukifika maeneo hayo, je utageuka utazame upande huo wenye vijumba au utageukia ‘DERM’ Complex?
 
Pamoja na hayo, vivutio vingi vya kitamaduni vinazidi kupungua uhalisia kadiri tamaduni zinavyo zidi kubadilika.

Nina mashaka, Makumbusho ile iliyoandaliwa 1996, itakuwa tofauti sana na itakayoandaliwa 2025. Uhalisia utazidi kupotea zaidi. Tusijekujenga magofu tukakosa wa kuja yatazama.

Usihofu kuhusu uhalisia!

Hata hivyo, kujenga makumbusho ya ‘vijumba’ mjini kati wakati huo hizo nyumba bado zipo watu wanaishi hatuwezi kuita ni Makumbusho.

Labda kama lengo ni kwa watu wa Dar pekee na wachache wengine, mikoani huku tunaona kama mmetufanyia mzaha ili kutukashfu. Kukumbuka maisha duni kwa gharama kubwa sio kitu cha kujivunia.

Hatuwezi kupoteza uhalisia, kwa kuwa hizo nyumba bado zipo huku mikoani na ni makazi ya watu.
 
Mara hii mshaanza kupataman mjenge sky scrapper

Patamu sana pale mkuu, ukizingatia muonekano wa mijengo jirani kile kipande kinaharibu sana... serikali sikivu italiona hili kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.
 
Patamu sana pale mkuu, ukizingatia muonekano wa mijengo jirani kile kipande kinaharibu sana. Serikali sikivu italiona hili kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.
Kwani pale hapako jirani na TISS? Mkiweka hayo ma sky scrapper si mtakuwa mnachungulia kwa wavaa suti black
 
Back
Top Bottom