Genekai
R I P
- Feb 9, 2010
- 12,514
- 5,003
Yah mkuu, i buy the idea!!!!Kila mmoja ana maeneo yake ambayo anafanya vizuri sana. Hakuna sababu yoyote ya kumng'ong'a mtu.
Yah mkuu, i buy the idea!!!!Kila mmoja ana maeneo yake ambayo anafanya vizuri sana. Hakuna sababu yoyote ya kumng'ong'a mtu.
Neno mwanamapinduzi limepoteza maana sasa Heche naye ni mwanamapindunzi.
![]()
![]()
Pichani ni katika mikutano mbalimbali inayoendeshwa na Mwenyekiti BAVICHA huko mkoani Kagera. Kijana huyu ameonyesha njia ya nini kinatakiwa sasa hivi kufanya badala ya kuhangaika na kulalakinia serikali kama Zitto afanyavyo.
Kwa mtazamo wangu afanyacho Zitto anataka serikali ya CCM ijirekebishe na hivyo kukosa uhalali wa kujenga hoja ya kuikosoa makosa yao wakati wa uchaguzi mkuu ujao, ndo maana naona viongozi wengi wa Chadema taifa hawako na ajenda za kulalamikia serikali au kuinyooshea vidole, ila kuwaelewesha wananchi.
Adui mkubwa wa CCM ni yule anayeingia vijijini kuwafungua akili wananchi, hawa wa kulalamika mjengoni hawainyimi serikali na CCM usingizi.
Zitto anatakiwa aelekeze nguvu huko kwenye kujenga chama matawini kama wenzake wanavyofanya. Kufanya afanyayo yamefanywa miaka nenda rudi na vyama vya upinzani kuanzia NCCM Mageuzi, CUF na vinginevyo bila kubadili sura ya wapiga kura kwa sababu hawakuingia kwenye source kubwa ya wapiga kura vijijini ambako CCM wamejichimbia kujihakikishia turufu ya kura kwenye uchaguzi mkuu.
Kumbe Heche nae ni Mchaga!!!!!!!! CDM bwana, Nami Suggestion nikianza mambo nitaambiwa Mchaga kumbe mm Muha wa KibondoWatu wa kaskazini hamumtaki zito kwani mnajua anakubalika katika urais na ndio maana hamkosi sababu kila kukicha. Hivi umaarufu wa zito unaweza ukafananisha na nani hapo chadema
paulss
Achana na hao, sisi wengine ni mahiri katika uchambuzi, na tumeshawahi kuwa na uzoefu katika vyombo vya kimataifa. Nafasi niliyofanya katika moja ya magazeti ya Marekani katika kipindi cha uchaguzi wa Bush nikiwa mwanafunzi huko nilipata kujifunza mengi ambayo waandishi tunatakiwa kufanya tofauti na tufanyavyo Tanzania.
Waandishi na vyombo vingi vya habari Tanzania kinachofanyika zaidi ni uhabarishaji, lakini uchambuzi katika mambo kama ninayofanya ni wachache sana, na ndio maana wanahitimisha kwamba unafanya kwa kulipwa na fulani. Vyombo vingi vinawoga, waandishi wengi wanafanya kazi zao kwa wasiwasi na kujaa woga. Woga huo ndio unaotumiwa na watawala kuwapumbaza kwa bahasha za kaki na kuishia kunyamazia habari muhimu.
Umegundua habari moja muhimu sana ya kuhusu mauaji ya Mwangozi ambayo Umoja wa nchi za Ulaya wameishuku Tanzania na kutaka haki itendeke kwa uwazi na uchunguzi uwe kwa uwazi na wahusika wachukuliwe hatua, utaona habari hiyo imenywea kabisa katika vyombo vyote vya habari, ni IPP tu ndio waliotoka kifua mbele katika hili. Huu ndio uanahabari wa Tanzania.
Unaweza kukumbuka mada kadhaa nyingi ambazo nilizileta kuhusu utendaji wa Mbunge Filikunjombe, wengi walinituhumu kuwa:
Ukweli umekuja kujithihirika baada ya wengi kujua undani wa Mbunge huyo na sasa kauli zile zimepotea baada ya kusoma ukweli.
- Filikunjombe mwenyewe anajitangaza
- Nafanya kazi ya kumtangaza kwa malipo
Tulio na uwezo wa kuchambua mambo haya tunatakiwa tujitahidi ili kuwaelimisha watanzania wengi ambao bado wanamwangalia mtu kwa upande mmoja tu bila kuangalia pande zote, matatizo ndiyo yanajitokeza mtu akishashika madaraka na kujutia, lakini kasoro tunazoziona na kuwatahadhalisha hawazioni na kuishia kuwa majuto ni mjukuu.
Hata vyombo vingi vya habari utakuta wanapomwita mhusika au kukutanisha jopo la watu kujadili jambo fulani, utakuta maswali muhimu ya msingi hayaulizwi ambayo hata mwanafunzi wa shule ya msingi angeweza kuuliza, na hivyo kukosa uwazi wa tukio na kukosa kupata msimamo na ukweli wa kitu halisi kutoka kwa wahusika. Hapo ndio utakapoona udhaifu huu wanautumia kujibu kwa majigambo na bila wasiwasi kwa vile hakuna wa kuwanyooshea vidole.
PakaJimmy
Dhahiri kila mmoja anakuwa na mwelekeo wa lipi anaona linafaa/linamfaa kufanya kwa manufaa ya mbadiliko kwa watanzania na chama au binafsi, lakini kuna kupishana katika mizani ya nini bora zaidi katika mageuzi tunayotaka kama tunataka kweli yafanyike. Hili la kuwanyoshea kidole mawaziri na wale wa magogoni limezoeleka tangu enzi za NCCR Mageuzi kwa vikubwa tu lakini mzizi wa fitiha haukukatwa; tunaohusika halituumizi kichwa kwa vile halitatuondolea kiti tunachokikalia. Hapa kwa kile kinachofanywa na Heche ndo kwenyewe, ndo maana unaona watu wazima wazima wanavyohaha huku na kule kutwa kucha kuzima kasi hiyo kwani wanajua vika walikojichimbia kunasambaratika, kwani tulizoea wa mijini tu hawatatutoa jasho. Kasi ya kuzima mikutano ya kufungua matawi ya vyama vya upinzani nini kama si kudhoofisha kasi ya badiliko nchini ya kuwafikia wananchi wa vijijini yaliko maskani ya CCM miaka nenda rudi?
Tunachofanya hapa ni kuwakumbusha ambao wanafikiri kushinda wananyoshea videle mawaziri na Ikulu kwamba ndio mageuzi kumbe huko ni hitimisho wakati mzizi wa fitina unaanzaia huko vijijini, ndilo linalotakiwa kufanyika kwa sasa.
Watu wa kaskazini hamumtaki zito kwani mnajua anakubalika katika urais na ndio maana hamkosi sababu kila kukicha. Hivi umaarufu wa zito unaweza ukafananisha na nani hapo chadema
Ok mkuu nimeipenda CV yako kama mwandishi mwenye weledi mkubwa.
Sasa mkuu labda nisaidie hapa kwanini habari za Heche dhidi ya Zitto zinakuwa nyingi?
Kwanini ni Heche vs Zitto na si heche vs wengine au Zitto vs wengine?
Just asking to know mkuu Candid Scope
Mkuu, binafsi nakusoma na najaribu sana kukuelewa. Ni kweli kuna logic kwenye hiki unachokizungumza, ila wasiwasi wangu ni namna unavyoonekana kumshambulia moja kwa moja bw Zitto. Nijuavyo mimi kuna mtu huwa ana jukumu la kufanya katika chama. Binafsi sijawahi kupata uthibitisho wa wa wazi wa MAKOSA ya bw Zitto. Na nimekuwa mfuatiliaji kwa kiwango cha kuridhsha wa siasa za Tanzania kwa sababu naamini kwa Tanzania, siasa imebeba msingi wa maendeleo. Wataalamu hawana tena thamani mpaka wanasiasa wawahurumie. Bahati mbaya tumekuwa na wanasiasa wabovu ajabu (ccm) ambao ndo wana jukumu la kututenganezea mazingira mazuri ya sisi watanzania kujiendeleza, matokeo yake hatupigi hatua za maendeleo zenye kuwiana na rasilimali tulizonazo.
Nikirejea kwenye mada yako hapo juu, napata shida kidogo kwa namna ulivyomshambulia bw Zitto, labda nisaidie hili swali, ni nini mantik ya wewe kuwapambanisha Bw Heche v/s Bw Zitto huku ukionesha kabisa kuwa tayari umeshamponda Bw Zitto??? kwa nini usiwapambanishe wanachama wengine wa CDM???Bw Zitto ana dhambi gani yenye uthibitisho ambayo mimi siifahamu??? nitasikitika sana kama yatakuwa majungu, kama unaweza nijibu hata kwa kuni-pm ili nami nimfahamu Bw Zitto pengine zaidi ya nimjuavyo kwa sasa. nakusubiri mkuu.
paulss
Achana na hao, sisi wengine ni mahiri katika uchambuzi, na tumeshawahi kuwa na uzoefu katika vyombo vya kimataifa. Nafasi niliyofanya katika moja ya magazeti ya Marekani katika kipindi cha uchaguzi wa Bush nikiwa mwanafunzi huko nilipata kujifunza mengi ambayo waandishi tunatakiwa kufanya tofauti na tufanyavyo Tanzania.
Waandishi na vyombo vingi vya habari Tanzania kinachofanyika zaidi ni uhabarishaji, lakini uchambuzi katika mambo kama ninayofanya ni wachache sana, na ndio maana wanahitimisha kwamba unafanya kwa kulipwa na fulani. Vyombo vingi vinawoga, waandishi wengi wanafanya kazi zao kwa wasiwasi na kujaa woga. Woga huo ndio unaotumiwa na watawala kuwapumbaza kwa bahasha za kaki na kuishia kunyamazia habari muhimu.
Umegundua habari moja muhimu sana ya kuhusu mauaji ya Mwangozi ambayo Umoja wa nchi za Ulaya wameishuku Tanzania na kutaka haki itendeke kwa uwazi na uchunguzi uwe kwa uwazi na wahusika wachukuliwe hatua, utaona habari hiyo imenywea kabisa katika vyombo vyote vya habari, ni IPP tu ndio waliotoka kifua mbele katika hili. Huu ndio uanahabari wa Tanzania.
Unaweza kukumbuka mada kadhaa nyingi ambazo nilizileta kuhusu utendaji wa Mbunge Filikunjombe, wengi walinituhumu kuwa:
Ukweli umekuja kujithihirika baada ya wengi kujua undani wa Mbunge huyo na sasa kauli zile zimepotea baada ya kusoma ukweli.
- Filikunjombe mwenyewe anajitangaza
- Nafanya kazi ya kumtangaza kwa malipo
Tulio na uwezo wa kuchambua mambo haya tunatakiwa tujitahidi ili kuwaelimisha watanzania wengi ambao bado wanamwangalia mtu kwa upande mmoja tu bila kuangalia pande zote, matatizo ndiyo yanajitokeza mtu akishashika madaraka na kujutia, lakini kasoro tunazoziona na kuwatahadhalisha hawazioni na kuishia kuwa majuto ni mjukuu.
Hata vyombo vingi vya habari utakuta wanapomwita mhusika au kukutanisha jopo la watu kujadili jambo fulani, utakuta maswali muhimu ya msingi hayaulizwi ambayo hata mwanafunzi wa shule ya msingi angeweza kuuliza, na hivyo kukosa uwazi wa tukio na kukosa kupata msimamo na ukweli wa kitu halisi kutoka kwa wahusika. Hapo ndio utakapoona udhaifu huu wanautumia kujibu kwa majigambo na bila wasiwasi kwa vile hakuna wa kuwanyooshea vidole.
Uchambuzi wako umetulia sana.Big up!Napenda umakini katika kujadili na kukosoa kwa nia ya kuwajenga watu. Tanzania tumekuwa na kawaida ya kushabikia viongozi bila kuwakosoa wanapofanya ovyoo na matokea baadaye tunajutia yanayojilia. Uongozi katika siasa si vema kushabikia kama timu ya simba na yanga, la sivyo yanayotukuta kama tungekuwa na uchambuzi wa kina na kujaribu kuona nani wa kweli yasingetukuta, ila basi sasa hakuna jinsi maji ukishayavulia nguo .......
Kama nilivyosema hapo awali, Zitto ni mpambanaji mzuri mjengoni kwenye mhimili wa bunge. Lakini chamani katika jitihada za kujenga chama anafanya kwa ujanja ujanja pale pasipo na dalili ya kupata matatizo anajaribu kuwepo. Lakini pale ambapo kunaweza kutokea matatizo Zitto hajawahi kujiingiza, hili ni tatizo na ni alama mbaya katika uongozi kwani ni dalili ya woga, kutojituma na kupenda kuelekea kwenye tambalare zaidi kuliko kupambana na magumu yanapotokea, kama nimekosea naomba nisahihishe. Zitto anakuwa mpambanaji mzuri pale sheria inapomlinda asidhurike au kuwajibishwa kisheria, ndivyo mfumo wa bungeni uliyvo tofauti na shguhuli za kujenga chama vijijini kupambana na mabomu ya polisi.
Zitto nilipoweka uzi mmoja hapa alijibu kupitia Twiter kuwa wanaopata matatizo ni kwa sababu ya kujitakia, ina maana kwa tamko hilo hayuko tayari kujituma palipo na ugumu katika kukijenga chama.
Zitto anaonekana kuwa busy zaidi na shughuli za Bunge kuliko shughuli za Chama, tungetazamia kama Kaimu Katibu Mkuu anakuwa na muda mwingi pia katika kukijenga chama, kwani ningetegemea Katibu mkuu angekuwa na mengi ofisini wakati fulani na kaimu wake kuingia vijijini kukijenga chama pamoja na makamanda wengine kwa kuwekeana zamu.
Weledi wa kupigania Urasi si kitu cha kawaida Chadema, lakini kama anafaa sina shaka Chama kitaridhia agombee, ila ana kazi ya ziada katika kuwa na ustahimilivu, kujituma katika mengi, maana kazi ya rais si kufuatilia wizara ya fedha na kashfa serikalini tu.
Kikwete alikuwa mzuri sana kama anavyofanya Zitto siku hizi, kama unaweza kuwa na kumbukumbu jinsi alivyomtoa kamasi hayati aliyefia Ulaya ambaye alikuwa waziri wa fedha wa kutokea kule Kilwa. Kitendo kile wengi tulimwona Kikwete ataweza kuwaadabisha na kuwawajibisha wazembe wengi serikalini akishika madaraka, kumbe tatizo tuliangalia kitu kimoja ambacho kikwete alikuwa anapigania na yule alionekana kuwa kukwazo cha yeye kupanda alipo.
Katika kujibu hoja yangu, Wamunzengo ulitakiwa uweke hoja zako hapa za kutetea utendaji wa Zitto, kwani hujaniletea hoja ambazo zinaleta uzito wa hoja yako ya kupinga hoja zangu. Huo ndio ungekuwa uchambuzi tunaotaka kwa weledi wa habari.
Naamini una uwezo wa kujenga hoja, nahitaji hoja hizo ambazo tutazijadili, na ndiyo ninayotaka ili kumjenga Kamanda Zitto. Tunajadili hoja, hatumchukii mtu kwa kujadili uwezo wake na udhaifu wake, bali tunampenda kwa kujaribu kumwezesha kwa kuonyesha kasoro na madhaifu ambayo yanaonekana ili ayafanyie kazi awe kiongozi wa kiwango tunachotazamia wengi.
Kwa hiyo ndugu yangu, usiwe na mtazamo hasi juu ya uchambuzi wangu, hapa tunajitahidi kuwajenga viongozi hawa wa kesho kwa njia mbalimbali, na tuonapo kasoro fulani zinajitokeza au udhaifu wa kibinadamu na wa kizembe tunahitaji kuwaweka kiti moto ili wafikie weledi tunaotazamia. Vinginevyo kushabikia tu fulani anafaa bila kumjenga tunafanya yaleyale ambayo tunajutia huku sisiem kwa vile tumezoea kujenga tabia ya kulindana kiushabiki bila kujali mambo ya msingi katika uongizo hadi mambo yao kama yalivyo kila mmoja sasa anaona anaweza kuingia Ikulu, kwa nini kama afanyavyo fulani mboma mimi naweza kufanya vizuri zaidi.
Mwakani mkwe wa mbowe hatasikilizwa tena mbowe na slaa hana chake ndani ya chadema lazima tubadilishe ukanda na ukabila maana tumechoka na huo ubaguzi yaani mpaka madeleva wa makao makuu ni wachaga watupu hii haikubaliki hata siku moja.
WEWA acha uongo madereva gani wachaga. Yule ABBAS uliyekuendesha kpndi unajipendekeza na ANTONI KOMU ni MCHAGA? mbona hausemi Tulikupa sh 2M na usafiri ukajijenge jimboni wakati wa chaguzi ndogo za vijiji MBOZI ulikuwa MCHAGA?
Mkuu achana na huyo mjinga ni sawa na pepo mchafu.
Tuko pamoja mkuu.