Pendekezo: Faini makosa ya barabarani ziongezwe hadi kufikia 50,000/=

waweke tu hata laki tutalipa naenda Tunduma from dar km zaidi ya 900 nitembee spidi mbili na kila mahali kuna kibao cha 50 na matuta kibao tutatenga bajeti ya faini wasiogope, by the way faini haisaidii wafanye kampeni ya elimu shule keenye kwenye media nk labda itasaidia
 
Kutokana na ongezeko la ajali za barabarani kutokana na mwendokasi na matukio mengine mengi ya barabarani nafikiri umefika wakati sasa Jeshi la polisi/ Wizara ya Mambo ya Ndani ipeleke muswada Bungeni kuongeza faini za makosa ya barabarani ili kuboresha sheria hiyo iliyotungwa miaka ya mwanzoni mwa 1970s.

Hii itasaidia kupunguza makosa hayo na kutunisha mfuko mkuu wa Hazina ya Taifa.

Nawasilisha.


Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.


Ingekuwa vizuri Iwe laki 300,000 ili tuheshimu sheria
 
Wananchi tuchangie huduma za jamii kupitia faini kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Sikatai kwamba ongezeko la faini linaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza ajali,ila ufanisi wake si mkubwa sana.
Nadhani pamoja na faini tuangalie ufumbuzi makini na wa kudumu....kutoa elimu ya kutosha kwa raia.Njia nzuri ya kufanikisha hili ni pamoja na kuongezwa kwa somo la USALAMA BARA BARANI kwenye mtaala wa elimu kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha nne ili kuongeza awareness ya raia kuhusu jambo hili,ili hata kijana baadae anapokuja kuingia mafunzo na kupata leseni ya kuendesha vyombo vya moto tayari anakuwa na basics kwenye fingertips tokea shuleni,na raia wanapotumia bara bara kama watembea kwa miguu au kama abiria watakuwa na level flani ya kujitambua itakayowasaidia kurekebisha baadhi ya mambo kwa faida yao.Siyo kila ajali hutokea kwa kukusudiwa na driver ili kwamba faini kubwa iwe ndio tegemeo la kupunguza ajali.
 
Makosa ya barabarani yanatofautiana. Hata kama utawatoza watu shilingi laki moja na nusu kwa kila kosa, drivers wasipobadilisha attitudes zao, ni kazi bure maana haiwezekani kuweka traffic police barabara nzima kumonitor mienendo ya watu.

Mbona torch ni za kumwaga Dar to Dodoma; lots of 50km/hr speed limit signs etc lakini ajari ni daily? Tunachofanya ni kupunguza speed tu kwenye vile vibao then tunarudi kwenye speed tulizozizoea baada ya kuvivuka.
 
Ongezeko la ajar barabarani halipunguzwi kwa kuweka faini ya fedha nyingi. Badala yake kuwepo na kifungo cha mwezi mmoja na ukitoka faini. Ili kuheshimu sheria na uendeshaji wa vyombo vya moto barabarani.


Hio isiwe kwa kundi dogo la watu liwepo kwa yeyote atakaetenda kosa la usalama barabarani.



Faini hazisaidii kupunguza ajar
 
tujifunze kwa nchi zilizoendelea, hata kwa jirani zetu RWANDA na wenzetu wa SADC (Afrika ya Kusini).
 
Tshs 50,000/= ili iwaje hasa... Kuna makosa mengine ya kionevu... Atasikia unamakosa matatu cjui... obstruction na kama hujui imekula kwako... Kuna makosa mengine ya kuonywa ila.... Mungu anajua
 
Watanzania bila mjeledi hatuendi. Trafiki endeleeni kutunyoosha. Mna Support yangu.
 
Siyo Dawa.Ikiwa kuna sheria ya kunyongwa hadi ufe unapothibitika kufanya mauaji,bado watu hawakomi na mauaji yanaendelea itakuwa hiyo kuongeza faini?

I can guarantee you.. additional fine will work. Mkuu hivi unadhani kupigwa fifty on the sport ni kitu kidogo? na hii 30000 ya sasa hivi naona imeanza kuwabadilisha watu.

In fact serikali isihangaike na mtu..iwe ni mwendo wa faini tuu. Tutanyooka.
 
Siyo Dawa.Ikiwa kuna sheria ya kunyongwa hadi ufe unapothibitika kufanya mauaji,bado watu hawakomi na mauaji yanaendelea itakuwa hiyo kuongeza faini?

Waseme tu ukweli kuwa hili eneo linachukuliwa kama chanzo kipya cha mapato na serikali yetu. Ndio maana sasa hivi trafiic wametengeneza mitego kila mahali.
 
faini ya speed ataikiwa 100000 itakuwa siyo mbaya.ila mkosa mengine ibaki 30000.kama hutaki kulipa faini fata sheria.
 
Tena ikibidi mbali na faini hao madereva watupwe jela angalau miezi 6 na akitoka achapwe bakora 12.
 
Back
Top Bottom