Polisi wafanya Oparesheni ya Usalama barabarani, Makosa ya magari mabovu yaongoza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Jeshi la Polisi limekamata Watuhumiwa 1,251 wa Makosa ya Usalama barabarani na baadhi yao wamefikishwa Makahamani na wengine kutozwa faini katika oparesheni maalum iliyofanyika kwa wiki tatu.

Makosa mengi katika orodha hiyo ni ‘Kuendesha magari mabavu’ ambayo ni 840, ambapo ilifanyika mikoa ya Kipolisi Ilala, Temeke, Kinondoni, Pwani na Rufiji kuanzia Machi 21, 2022 - Aprili 2022 kwa lengo la kuzuia na kupambana na uhalifu wa makosa makubwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema: “Hairuhusiwi kuendesha gari ukiwa umelewa kwa zaidi ya kiwango cha Miligramu 80/mililita 100, pia hairuhusiwi kabisa kuendesha gari la abiria lenye leseni LATRA ukiwa umelewa, na huruhusiwi kuendesha gari la Serikali ukiwa umelewa.”

Makosa hayo ni:
1. Overtaking kwa njia ya hatari watuhumiwa - 36
2. Mwendokasi - 83
3. Kuendesha magari mabavu - 840
4. Kutojali alama za barabarani (Zebra na Taa Nyekundu) - 270
5. Madereva wa magari ya Serikali - 22

Aidha, Operesheni hii ilifanikiwa kukamatwa kwa Raia 45 wa Ethiopia na Somalia ambao walikabidhiwa Jeshi la Uhamiaji kwa mahojiano.

 
Back
Top Bottom