Nakubali kwamba "Operesheni Sangara" ilikuwa nzuri sana na matunda yake yameonekana ila si vizuri kuendelea na jina hilo hilo - opesheni ni kitu kina kuja kwa kusudio na wakati maalumu na kupita. Sangara imekamilisha malengo yake, ije nyingine. Pia unaweza kushangaa ni kwanini opesheni hii imeleta mwamko mkubwa maeneo ambako "Sangara" wanapatikana, yawezekena ukanda wa kati na kusini wa nchi yetu hakukuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na jina lililotumika - SANGARA - ambako wakazi wengi hawamfahamu vizuri? Sijui.
Mimi nashauri litafutwe jina na kauli mbiu ambayo hata mtoto mdogo akiisikia itamtoa machozi na kuamsha moyo mpya wa kizalendo - Afrika Kusini walitumia sana mbinu hii dhidi ya makaburi - muulize Jacob Zuma anajua vizuri sana hili. Tanzania hapa ilipo sasa hivi ina matatizo nadhani yanayokaribia ya Afrika Kusini ya enzi zile. Unahitajika ushawishi mpya, mwamko mpya, hamasa mpya - vijini na mijini hata kwa wa-Tz waishio ng'ambo. Watu wajue thamani ya kujiandikisha na kupiga kura; kutokuuza shahada, kufikia maamuzi sahihi, kutokughilibiwa na hadaa za wanasiasa wanaotumia mbinu mbali mbali zikiwemo chafu za UDINI, amabao kimsingi haupo ila unajaribu kupandikizwa na kuchochewa.
Na wakati wa kuanza hayo si kusubiri hadi wakati wa kampeni, vyama vya upinzani anzeni haya mambo sasa. Ni haki yenu kisheria kufanya siasa na si kudanganyana eti kampeni zimeisha!!!