Penda unapopendwa! Ushuhuda wangu.

Penda unapopendwa! Ushuhuda wangu.

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,066
Habari za leo wanajf! Waswahili wanasema penda unapopendwa, asiyekupenda achana naye! Nilipokuwa naanza chuo nilikuwa na msichana X ambaye tulikuwa na uhusiano kimapenzi yeye akiwa form five. Nilikuwa nampa ushauri wa kimasomo na kum encourage na mambo ya shule ila sikuwa na fikra za kuoa kwa wakati ule, nilimpenda na yeye alinipenda sana. Nilipofika mwaka wa tatu nikapata msichana mwingine Y ambaye alikuwa anasoma chuo. Nilimpenda sana yani aliiteka akili yangu kabisa na na nilijiapia kwamba ndiye tutakayeishi pamoja maishani. Nilianza kupunguza mawasiliano na yule mwingine ili akate tamaa na kupata wa kwake mwingine. Lakini huyu dada alinipenda kuliko kawaida na hakukata tamaa kwani yeye ndo akaongeza mawasiliano(.niliwahi mcheat huko nyuma pia). Ilifika kipindi nikawa nashindwa kufanya uamuzi kwani sikuzoea kuachana na mtu kwa shari. Nikiwa mwaka wa tano huyu Y watu wakamwambia mbona huyo jamaa ana mtu wake wa siku nyingi na ana mpango wa kuoa, wakampa na namba ya X. Y akampigia yule dada na kumwambia naomba uachane na mchumba wangu kwani tupo njiani kuoana. X alinipia simu na kuniuliza kama nina mtu mwingine kwa nini sikumwambia? Mbona nimemtesa kiasi hicho? Alijuta sana hata kunipenda nami nilikuwa na majibu ya mkato tu. Ukweli nilimwonea huruma lakini ndo hivyo akili yangu imeganda sehemu. Miaka miwili baadaye nikiwa kwenye kujipanga nikamilishe familia Y akanitenda kiasi cha kunichanganya kabisa mpaka nikakumbuka maneno aliyoniambia mdogo wangu kuwa kuna watu tunawaacha kumbe ndo wake bora baada ya kumwambia nimemuacha X. Tusilazimishe kupendwa, wapo wanaotupenda kwa dhati nao tuwachukulie kwa umakini. Kazi njema.
 
Hapo ndipo ningeeeeeeeeeeeeeeee! huanza. Eheee malizia mwisho wake ukarudi kwa x ama?
Pole kwa maswahibu kijana
 
kajinyenyekeshe uombe msamaha..
km alikupenda na hana mtu atakukubalia...lakin km ashapata Y wake na yeye ahh ni muda muafaka kwako kutandika majamvi kwa matanga....:bounce:
 
Naona mambo ya X+Y= Something

Sijui ni kitu gani ulichokua unakikosa kwa juyo X wako mpaka kikakufanya umtende kiasi hicho maana hapo ni kama kumhukumu mtu bila kosa, hebu fikiria ni maumivu kiasi aliyoyapata kwa kumkatili pasi na kosa lolote?

Hapo ulifanya maamuzi bila kufikiria, kitu ambacho kimekuja kukucost vibaya sana.

Jaribu kujishusha sana kwa kumuomba X wako msamaha ila usifanye lolote kama utamkuta tayari kashapata mwingine kwani nafasi tayari umeshaichezea haina budi na mwenzako ajaribu bahati yake.
 
Mtaka yote hukosa yote.

sikutaka yote ndugu yangu. Nilinasa sehemu isiyokuwa na faida nikaacha pazuri. Niliyempenda zaidi sikujua kuwa hanipendi au ni tamaa ndo zimemfanya hivyo.
 
kajinyenyekeshe uombe msamaha..
km alikupenda na hana mtu atakukubalia...lakin km ashapata Y wake na yeye ahh ni muda muafaka kwako kutandika majamvi kwa matanga....:bounce:

ndugu yangu huyu dada alishanambia kwamba nimemtesa sana na atapata shida kuanzisha uhusiano. Mara ya mwisho alinambia ana mtu wake na hatopenda kuonana na mie kwani anajua yatakayotokea tukikutana. Najutia mwenyewe kwa kulinda mawe na kuacha dhahabu ikaibiwa.
 
Hapo ndipo ningeeeeeeeeeeeeeeee! huanza. Eheee malizia mwisho wake ukarudi kwa x ama?
Pole kwa maswahibu kijana

asante ndugu yangu. X alinambia ana mtu wake kwa sasa hivi na hataki kabisaaa kuonana na mie face to face
 
Saudari, x+y imeniletea maumivu na kustalk njiani.
 
Pole sana, ila hicho unacho kifeel sasa hivi ni haki yako kwasababu ni matunda ya usaliti

yah mkuu. Nilijutia na najutia. Nilimsaliti na nikamuumiza sana. Hata mdogo wangu alisikitika nilipomuambia nimemuacha x kwani alikuwa akimfahamu.
 
kweli kabisa..happened kwangu but nadhani mimi ndo x .
Kuna wakati unapenda na kuteswa na mtu ila u hang on to something unadhani kitabadilika which never happens.unajua kabisa the person is taking your affection for granted ila upo tu.
Tatizo linakuja siku ukichoka na kupata mtu ambaye anajua your worth ndo hapo mtu anashtuka na kuona alichokua anakitafuta siku zote kwa watu wengine its worthless.
Na most of the time,when you treat someone who truly loves you vibaya na kuona hafai,sijui ni karma but hua inarudi.
Pole.
 
Back
Top Bottom