Penda unapopendwa! Ushuhuda wangu.

Penda unapopendwa! Ushuhuda wangu.

Habari za leo wanajf! Waswahili wanasema penda unapopendwa, asiyekupenda achana naye! Nilipokuwa naanza chuo nilikuwa na msichana X ambaye tulikuwa na uhusiano kimapenzi yeye akiwa form five. Nilikuwa nampa ushauri wa kimasomo na kum encourage na mambo ya shule ila sikuwa na fikra za kuoa kwa wakati ule, nilimpenda na yeye alinipenda sana. Nilipofika mwaka wa tatu nikapata msichana mwingine Y ambaye alikuwa anasoma chuo. Nilimpenda sana yani aliiteka akili yangu kabisa na na nilijiapia kwamba ndiye tutakayeishi pamoja maishani. Nilianza kupunguza mawasiliano na yule mwingine ili akate tamaa na kupata wa kwake mwingine. Lakini huyu dada alinipenda kuliko kawaida na hakukata tamaa kwani yeye ndo akaongeza mawasiliano(.niliwahi mcheat huko nyuma pia). Ilifika kipindi nikawa nashindwa kufanya uamuzi kwani sikuzoea kuachana na mtu kwa shari. Nikiwa mwaka wa tano huyu Y watu wakamwambia mbona huyo jamaa ana mtu wake wa siku nyingi na ana mpango wa kuoa, wakampa na namba ya X. Y akampigia yule dada na kumwambia naomba uachane na mchumba wangu kwani tupo njiani kuoana. X alinipia simu na kuniuliza kama nina mtu mwingine kwa nini sikumwambia? Mbona nimemtesa kiasi hicho? Alijuta sana hata kunipenda nami nilikuwa na majibu ya mkato tu. Ukweli nilimwonea huruma lakini ndo hivyo akili yangu imeganda sehemu. Miaka miwili baadaye nikiwa kwenye kujipanga nikamilishe familia Y akanitenda kiasi cha kunichanganya kabisa mpaka nikakumbuka maneno aliyoniambia mdogo wangu kuwa kuna watu tunawaacha kumbe ndo wake bora baada ya kumwambia nimemuacha X. Tusilazimishe kupendwa, wapo wanaotupenda kwa dhati nao tuwachukulie kwa umakini. Kazi njema.

haya nishauri mimi Kaunga na John
Mimi nampenda sana John, na John anampenda sana Joyce ambaye hampendi sana John (Joy anampenda sana Julius) na mimi napendwa sana na Michael ila simpendi kama ninavyompenda John
 
kwikwikwikwi ukome kabisa.......................pole sana siku nyingine utulizane.
 
Madamu umejifunza nakuombea kheri umpate akupendae Umpende kwa dhati.
Tunajifunza kwa makosa usijilaum sana
 
yah mkuu. Nilijutia na najutia. Nilimsaliti na nikamuumiza sana. Hata mdogo wangu alisikitika nilipomuambia nimemuacha x kwani alikuwa akimfahamu.
Ulimuumiza sana. Lkn hebu jaribu kumfuatilia tena huyo X pengine anakudanganya kua ana mtu. Kumbuka huyo ndiye aliekupenda kwa dhati na nadhani hata yeye hatopenda kama alivyokupenda wewe. Tafadhali hebu mfuatilie na utumie kila njia ili muwe pamoja. I believe anaweza kukubali sababu wewe ndiye anayekupenda na yeye anajua hilo.
 
Mbona story yako inafanana na ya demu wangu mpya aliyoniambia kuhusu her previous guy,usikute ndo X mwenyewe!
 
haya nishauri mimi Kaunga na John
Mimi nampenda sana John, na John anampenda sana Joyce ambaye hampendi sana John (Joy anampenda sana Julius) na mimi napendwa sana na Michael ila simpendi kama ninavyompenda John

kama kuna hata kahisia kadogo kwa huyo maiko ni bora ukajibanza tu. Huko mbele mambo yatajipa. Kama mlishakuwa kwenye uhusiano unajua mapungufu na strength zake hivyo ni rahisi kurekebishana.
 
Ulimuumiza sana. Lkn hebu jaribu kumfuatilia tena huyo X pengine anakudanganya kua ana mtu. Kumbuka huyo ndiye aliekupenda kwa dhati na nadhani hata yeye hatopenda kama alivyokupenda wewe. Tafadhali hebu mfuatilie na utumie kila njia ili muwe pamoja. I believe anaweza kukubali sababu wewe ndiye anayekupenda na yeye anajua hilo.

ye mwenyewe anajua kuwa alinipenda na bado ananipenda ndo maana nikimuomba nikutane naye hata mazungumzo yanabadilika. Hataki kabisaaa kusikia kukutana na mimi aafu sasa hivi tuko mikoa tofauti.
 
Mbona story yako inafanana na ya demu wangu mpya aliyoniambia kuhusu her previous guy,usikute ndo X mwenyewe!

ha,ha,haa. Sijui kwani wenye maisha ya aina hii wako wengi. Kwani uko mkoa gani mkuu?(unaweza nipm if u dont mind)
 
Unaposema upende unapopendwa inamaanisha unapopendwa wewe hupapendi sasa kama ungempenda vilivyo huyo x usingzingua by the way kwan huyo x ungekua nae ungekua bill gates ama..??not every thing is meant to be niggah..achana na majuto moyo wa binadamu hauridhiki ukimrudia x things would never be the same..na still ungependa kua na y pia..so ni wewe mwenyewe kutengeneza fatcs kichwani kwamba moyo hauridhiki..!!!
 
Majitu kama nyie ndo mnaofanyaga wanawake watuone wanaume wote ni matapeli wa mapenzi.
 
Back
Top Bottom