PCF yatenga Milioni 270 kutekeleza kampeini ya 'Msitiri Mwanamke Gerezani', Wanawake 1500 wakusudiwa kufikiwa

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Prison Charity Foundation (PCF), inatarajia kuanza kampeni ya 'Msitiri Mwanamke Gerezani' inayohusishautoaji msaada kwa wanawake waliopo gerezani ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabiri.

Kampeni hii itahusisha ununuzi wa mahitaji muhimu kwa wanawake kama taulo za kike,
nguo za ndani, upimaji wa saratani na kugawa vijarida mbalimbali vinavyotoa elimu juu ya afya ya akililengo likiwa ni kuwastiri baadhi wanamke waliopo gerezani nchini Tanzania.

Katika kampeni hiyoKampeni la wadau hao ni kuwafikia wanawake waliopo gerezani takribani 1,500. huku ikitarajiwa kugharimu kiasi chashilingi milioni 270,000,000, gharama itakayohusisha ununuaji wa taulo za kike, nguo za ndani,kuchapisha, kusafirisha na kusambaza majarida yenye kutoa elimu inayohusu afya ya akili, pamoja nakuongeza uelewa wa changamoto zinazowakabili wanawake waliopo gerezani na walio katika hatari yakuingia gerezani.

Imeelezwa kuwa kampeni hiyo ina lengo la kutatua changamoto za usafi wakati wa hedhi, tiba ya changamoto za afya yaakili na upimaji wa magonjwa wa saratani. Kampeni itaenda kuwapa wanawake waliopo gerezani bidhaa
zinazohitajika wakati wa hedhi.

"Tunaamini kwamba kila mmoja anastahili msaada na usafi kwamwanamke na mahitaji yao ya kibinadamu bila kujali mahali walipo. Vitu hivi vya msingi vitasaidiakuboresha utimamu wa kimwili na kiakili kwa wanawake waliopo gerezani, unaopelekea kuwa na afya njema." wameeleza hayo leo Desemba 12, 2023.

Katika tamko lao kwa vyombo vya habari wameeleza kuwa malengo ya kampeini hiyo ni kutoa taulo za kike na nguo za ndani kwa wanawake waliopo gerezani, kuboresha afya ya akili kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kuhusiana na tatizo hilo na kuwapa ujuzi mbalimbali wanaoweza kutumia ili kustawisha utimamu wao wa akili, kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusiana na changamoto zinazowakabili wanawake waliopogerezani na njia sahihi za kutatua changamoto zao.

Itakumbukuwa taasisi ya PCF imekuwa ikijikita katika kutoa msaada wa kibinadamu na kisheria kwa Wafungwa, Mahabusu, watoto navijana waliokinzana na sheria ama walio katika hatari ya kukinzana na sheria , ili kuhamasisha upatikanajiwa haki kwa makundi hayo.

Hata hivyo katika kutekeleza kampeini hiyo baadhi ya wadau wameanza kujitokeza kutaka kuwaunga mkono ili kuwafikia walengwa wengi zaidi kwa kujitolea kutoa mahitaji mbalimbali.

IMG_20231212_114110_891.jpg
 
Back
Top Bottom