PCCB: Tuna manufaa nayo?

hao maofisa wamelikisha wapi...wewe hujatosa source, sie tunaejua anaevujisha hilo data ni wewe, unless ungetuambia umeokota barabarani, tungejua....Kama wale waandishi waliochapisha mitihan wakasema tumeona imebandikwa ktk vituo vya basi
 
mAAFISA HAO HAO WA PCCB mkubwa

sasa si ni vizuri na sisi ambao tulikuwa hatujui nini kilitendeka tunaona sasa.
Waendelee kuvujisha hadi za mapapa kwani hawa ni dagaa tu walio tajwa humu.Waambie wakupe na za mapapa tuwakomalie.
 
Everyday's crap.Vidagaa tuu alafu Makambale wanajinomi tuuuuuuu.Huyu Prof.Chambo hana lolote namfahamu inside out fisadi tuu na yeye.
 
Kuna uwezekano wa kutofanyiwa kazi report hiyo kwa sababu za kifisadi/ upendeleo /au tu kupindisha sheria ilikuogopa kuset precedency kama kawaida yao, hivyo wameamua kuivujisha ili isiwe siri.

Au kuna mchezo mchafu wa kumsacrificemtu aliyeiandaa hiyo report aonekane ameivujisha hence lack of profesionism/violation of code of conduct ili atimuliwe = consipracy, maana naona it was ably and professionally prepared!

Halafu report hii inatuonyesha kumbe tuna watu wenye uwezo wa chunguza mambo lakini aidha hatutaki kuwatumia au tukatupa kwenye bins report zao.

Tunataka ujuzi huu ukatumike kuibua mapapa na manyangumi na mchezo uchezwe kwenye leveled playing field sidagaa wala papa wote wawajibishe!
 
Kadagaa kameiba millioni moja na nusu ndiko kanaonewa. Imagine time waliyochukua PCCB na shsh ngapi wanalipwa kwa mwezi na simu walizopiga. Zinazidi hiyo 1.5million walizogundua. Hata hivyo ni poa maana wameprevent za baadaye kuibiwa
 
Watuletee hapa ripoti za uchunguzi wa wakina Lowasa, Chenge, Rostam, Mkapa na wakubwa wengine wengi tu. Watulambishe upuuzi wa vipesa hivi wakati wanaoiba 152m kwa siku wanapeta.
Hii ni kutaka tuwaone ni wachapa kazi wakati hakuna lolote ni walambaji wa kodi zetu tu.
Wezi wakubwa si hawa. Wapo na hao ndiyo tunataka kuona wanashughulikiwa.
 
Ni janja yao kutaka waonekane wanafanya kazi wanleta ripoti za wizi wa shilingi miamibili? kwanza watueleze kwanini walimsafisha fisadi na mwizi mkubwa RICHMOND?

Pili watuletee ripoti za wizi wa EPA, ujenzi wa BOT siyo hivi viwizi uchwara!, By the way hivi ile hoja ya bunge kwamba PCCB haifai ivunjwe na kuundwa upya ilifia wapi? ama nasahau na kujichanganya?
 
Kazi ipo! Hawa wamelamba vijiposho tu, tungependa kupata docs za wazee wa vijisenti na siyo mijihela kama hii!
 
would be interesting ati wakivuja ile ya Ubalozi wa Italia the way they cooked it on behalf of...............
 
Nguvu yote na muda wote kuchunguza upotevu/wizi wa 400,000/- jaman? Tungependa kuelewa PCCB walitumia kiasi gani kuchunguza kashfa hii ili tuone kama ni matumizi mazuri ya fedha. Kifupi tu tatizo liko wazi halikuhitaji PCCB.
 
Fisadi mdogo wa leo ndio lijifisadi kubwa la kesho, hongereni PCCB, tunajua hamna meno yakuwatafuna kina-vijisenti na wanzao kwa hiyo nyie kuleni tuu vichwa vichovu, atleast mtaonekana hamjasinzia kabisaaaa!!!!!
 
Ivi watu wanataka pccb wasikamate hawa walarushwa wadogo au?????
 
jamani ni masikitiko tupu kumbe ndivyo nchi yetu ilivyo. kumbe ndio maana hata kusimama kwa ZE COMEDY kuna tetesi kuwa ni mkono wa fisadi mmoja wa richmond. si mnakumbuka jinsi ze comedy walivyoirudia ile issue ya kuresign ya mhe. kule bungeni

this is the shouting death
 
Hii ndiyo hali halisi ndgu yangu. si unajua tena hata mapokezi yake yalivyokuwa kule kwetu? mafisadi wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hawaumbuliwi na kwa sababu fedha wanazo, ambazo hawakuzitolea jasho, basi hawaoni taabu kuzimwaga kwa vijifisadi vidogo.
 
Lkn vipi kuhusu ile nyumba ambayo nasikia huyu jamaa wa pccb anadaiwa kuinunua kwa fedha za taasisi? hivi kuna ukweli wowote au ndo kujitetea kwake kwamba wapo jamaa wanataka kumchafulia kwa kukawania kacheo kake?
 
kwa vyovyote ukifanya kazi iliyo juu ya uwezo wako lazima maji yatakufika shingoni
 


Rubbish! Tunataka za mafisadi wakubwa, siyo za fisadi mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…