PC nzuri ina sifa zipi?

Daaaah mkuu kwa maelezo uliompa anaweza ishia nunua PC iliyo pigwa msasa tuuuu... hayo maelezo ungetoa kwa ambaye ni Pro or Expert tayari ila sio kwa #Beginner
 
Mi nasema aksante kwamleta uzi aksante Chief mkwawa kwa kututoa tongo za macho na aksante wachangiaji wote!
Hii kutojua mambo ni majanga nimeuziwa Dell inspiron 15 series mbili kwa 450$ a piece(900$ total wakati kwa mkwanja huo ningepata za ukweli tu!
 
pamoja mkuu nimekupata,ntarefer humu siku nikitaka kununua laptop mya,maana hii nilionayo ishachokachoka.
 
Hapana mkuu, nilimaanisha RAM za ddr4..
sijakuelewa mkuu unamaanisha hizo processor mpya zinapatikana kwenye computer za apple ambazo bei zake ni sawa na shamba?

zipo pia processor za skylake ambazo zinapatikana kwenye computer za bei za kawaida kama i3 6100u
 
Mkuu ikiandikwa version 6.1.7600 humaanisha nini?
hizo ni namba tu za kutofautisha matoleo.

mfano kitabu cha eric shigongo kinaweza kuwa na toleo la kwanza, la pili, la tatu etc

kwenye software nako ni hivyo hivyo kunakuwa na matoleo tofauti tofauti na kila toleo jipya huongezwa mambo mapya na kuzidi kuwa zuri.
 
Sasa utajuaje kuwa ni ddr4 or 3? Je model hii ni nzuri? Intel (R) core (TM)i3-2330M?
 
"Chief-Mkwawa, post: 16409800, member: 44606"]ndio kwa matumizi ya kawaida ni nzuri na hio ni ddr3 ram zake
Ahsante sana mkuu
 
bei za ddr4 ni sawa tu na ddr3 zamani ndio zilikuwa ghali ila sio sasa hivi hii inatokana na demand kubwa ya skylake.
mkuu vipi hizi processor za intel centrino zipo kundi gani? ninayo T7300 emb ichambue kwangu iko poa ila nkitaka kuifanya ishee internet inakataa inasema inataka wi fi card kama sio adapter sikumbuk. nlidownload app moja inaitwa host wifi sikumbuk vizur hiyo adapter ntaipat wapi?
 
hizo ni za zamani sana kabla hata hizi generation hazijaanza. na inawezekana hio laptop ikawa haina wifi kabisa hadi ununue nyengine ueke, pia inawezekana ikawa ni driver tu. nitajie full name ya laptop nikuangalizie kama driver na kama unataka kununua wifi itabidi utafute kitu kama hiki



vinapatikana around 10,000 hadi 30,000 unachomeka tu kwenye port ya usb na computer yako inakuwa na wifi.
 

Mkuu nakumbuka nishawahi kusoma mahali kwamba M inasimama kwa ajili ya mobile hivyo ipo kwenye notebooks pekee ambazo zimelengwa ziwe na power backup nzuri zaidi. Hivyo nimepata mkanganyiko kidogo kuhusiana na ya hio Prefix!
 
Mkuu nakumbuka nishawahi kusoma mahali kwamba M inasimama kwa ajili ya mobile hivyo ipo kwenye notebooks pekee ambazo zimelengwa ziwe na power backup nzuri zaidi. Hivyo nimepata mkanganyiko kidogo kuhusiana na ya hio Prefix!

compare na desktop M zinatumia umeme mdogo, compare na HQ (quadcore za laptop) hizi M zinatumia umeme mdogo compare na U hio M inatumia umeme mwingi, compare na atom hio U pia inakula umeme mwingi. hivyo hio sentesi yako juu ni sahihi kama unacompare na desktop.

kikawaida hizi ndio TDP za processor za intel kwa sasa

-watts 51 kupanda
hapa unapata processor zote za desktop za kawaida kuanzia i3, i5, i7

-watts 45 hadi 47
hizi ni quadcore za laptop nyingi zinaishiwa na HQ kwa mbele mfano i7 6700hq

-watts 35 hadi 37
hapa mara nyingi ndio unapata hizo M kama vile i5 4200m na zote ni dual core hata ikiwa i7 inaishiwa na M ujue ni dual core. pia zipo zinazoishiwa na S na T hizi zinakuwa ni za desktop lakini zinazotumia umeme mdogo kama i5 4570T

-watts 28
hizi zinakuwa ni za U lakini zina graphics kubwa kama i3 6167U

-watts 15
hizi zinaishiwa na U kama hizo hapo juu sema zina graphics za kawaida kama i7 6500u

-watts 7 hadi 10
hizi ndio zinazoanziwa na N kwa ajili ya laptop ndogo za bei rahisi na zinakaa sana na charge

-watts 4
hapa unapata core M za tablet na vilaptop vyembamba kama macbook air mpya na dell xps 13 hizi pia hukaa sana na charge

-watts 2
atom series hutumika kwenye simu na tablet za bei rahisi

hivyo ukiangalia huo mtiririko utaona position ya cpu zinazoishiwa na M, pia kuwa makini usichanganye core M na cpu zinazoishiwa na M ni vitu tofauti
 
Pc nzuri andaa budget ya kama laki 7 na nusu kwa sasa, processor utachagua ila iwe ni miongoni mwa zile corei series either i3,i5,i7...chukua corei5 ila uhakika sana ni kuwa utapata ya corei3 chagua yenye clockspeed at least 2.4GHz
Nunua yenye minimum hard disk volume 750GB kama utakosa ya 1TB.
RAM inatakiwa isiwe chini ya 4GB so kama ukipata zaidi ni poa either ikiwa ddr3 au ddr4 freshi tu.
Graphics card iwe ni intel HD 4000 na zaidi usinunue chini ya hapo kama itakuwa na dedicated card kama Nvidia itakuwa poa zaidi.

Purchase options:
Brands nzuri ni HP design nzuri, battery nzuri zinadumu cooling system iko poa plus loud speakers.

Acer design nzuri ,ziko cheap kidogo na zina offer feature hizo hizo sema speakers wanachemkaga na battery inawahi kufa coz zina pata moto sana ukitumia muda mrefu na kama utakuwa huishi kwenye mazingira ya a/c ni mtihani.

Dell zipo cheap design zao sio appealing sana,ila nina historia ya kukutana na factory defects katika mashine zao,hazikawilii kuharibika hasa zile inspiron labda uchukue za latitude. Kuhusu battery wanajitahidi sana!

Lenovo nazi rank next after hp, ziko very reliable especially battery na display zao angavu.

Asus is a newbie kibongo bongo, wapo very innovative katika technology sina uhakika nao sana katika reliabilty.

ushauri: Nunua hp mkuu ama lenovo kama hela ikiruhusu.
 
Kiongozi, nichekie na mimi specs za hii laptop, dell latitude 5020 (kama sijakosea.)

specs za pc bonyeza start/search halafu andika dxdiag then click hicho kiprogram kitakachotokea utaziona

au nenda my computer halafu right click then properties pia utaziona

ni ngumu kwangu kukutajia sababu laptop moja inakuwa na variety nyingi hadi uangalie mwenyewe
 


ni hp compaq 6910p with window vista, centrino vPro, energy star processor ni Core(TM) 2Duo Cpu T7300 2.0GHz.
ndo hiyo mkuu vipi inaweza ingia window8 maana nlipata kaujumbe niweke window10 nkaoga maana hawa wafanya biashara waongo pia iko fasta sana na inachoma kwa kweli na sauti kubwa sana ya kale kadude kakizunguka ku cool pia ina ddr2 ram 1gb kama 60gb hivi hdd
 

wifi inayo cheki driver hapa.
Drivers & Software for HP Compaq 6910p Notebook PC - HP Support Center.

kuhusu kueka windows 8/10 inawezekana sababu pc yoyote ya vista inakubali hizo os ila sikushauri sana kueka sababu ya support ya driver itakuwa hakuna utasumbuka.

hivyo kuheat ni kawaida kwa mashine ya core 2 duo hasa kama yako yenye watts 35 hakikisha tu uwe unaieka mazingira mazuri yenye upepo ili isijibane sana
 
Hivi mkuu laptop za lenovo thinkpad zina kitu gani cha ziada mbona ghali sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…