Paypal Petition

Mateja M.G Yango

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
613
Reaction score
1,097
UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU

Kwa miaka mingi sasa tumekuwa tukiumia sana na hili swala la kutokuweza kupokea malipo kupitia paypal, binanfsi ni member wa paypal toka mwaka 2007, hadi leo ni miaka 8 mwendo ni ule ule wa kufanya matumizi tu, kupokea malipo imekuwa ni ndoto.

Muda umefika sasa wa kuungana ili sauti za vilio vyetu zisikike walau mwaka 2016 nasi tuanze nufaika na huduma hii.
Karibu tupange wote mikakati ya kuwezesha swala letu kushughulikiwa, kama tukiweza fika watu hamsini litakuwa jambo jema sana na litarahisisha mambo mengi.
Ntaanza kwa kutengeneza group whats app, 0713752285, tuma message paypal petition, ntakuadd kwenye group.
Kama haupo whats app, pm your number, ntakushirikisha kwenye kila hatua.

Hakuna kurudi nyuma hadi tufanikiwe.

Together we can.

UPDATES: 04/12/2015.
So far watu6 wameshajitokeza kuunganisha nguvu katika hili, watu wengi zaidi wa kada mbali mbali mnakaribishwa kuweza kuungana pamoja na kufanikisha hili.

UFAFANUZI:
 
Mkuu umekuwa ukitumia kununua vitu kwenye mitandao?
 
Una visa card or master card?
Umesharegister card yako kwa paypal?
 
Una visa card or master card?
Umesharegister card yako kwa paypal?

Yeah na nimesharegister tayari mkuu, sasa ishu inakuja kwenye shipping address pale. Naomba nipe mwongozo nyinyi mnatumia njia gani si unajua bongo sio kama ulaya au marekani.
 
Hilo wazo zuri; unganisha na nyingine kama alipay ya wale jamaa wa alibaba ambayo inawatumiaji wengi kuliko paypal ila kwa kununulia vitu china.

Juzi nilijiunga nayo ili ninunue vitu alilbaba na aliexpress lakini ikashindikana kuungunisha visa card yangu kwasababu wahemiwa huku hawajaruhusu iweze kutumikaka kwa manunuzi na uuzaji.

Tuna kosa uwezekano wa kuuza vitu ebay au alibaba kwa kuwa hatuwezi kupokea pesa kwa paypal au kutuma na kupokea hela kwa alipay.

Nakuunga mkono kwa initiative yako
 

Wewe umeshawahi kununua kitu amazon au ebay? Lengo la swali hili ni ili unisaidie kwenye ishu ya shipping.
 
HansMapunda
Kama unanunua ebay, angalia seller anayeship vitu worldwide, kama hajaandika hivyo mtumie text muulize kama anaweza ship world wide,
Pia kama kitu kinatoka china nakushauri nutumie dhl, kama kinatoka marekani basi ems/usps express/priority ni njia nzuri zaidi.

Epuka kutumia standard mail kwa usps hata kutoka china, maana hautakuwa na tracking number, mzigo unachelewa na haujui uko wapi, unaweza fika posta bongo wakakaa nao hata siku 30 ndio ukaja upata, so ukitumia priority mail or express mail kwa usa na dhl kwa china mzigo unaupoata faster, actual dhl ndani ya week tu.

usisahau issue ya kodi, jua kitu unachoagiza kitatozwa kodi gani
inmport duty ni 25% ya ghalama za mzigo wako
Vat ni 18% ya gharama ya mzigo wako
 
Last edited by a moderator:
sio tu kuuza vitu online, pia tuna graduates wengi sana wa computer na \it, wangeweza jiingizia kipato kupitia free lancing.

 

Nashukuru sana kwa maelezo uliyonipa, kwa mfano kama nataka kutumia dhl address ninaandika vip? Maana nilitaka kununua nikahitajika kuandika address.
 
Last edited by a moderator:
Hili swala sio la kudeal na paypal, wao their system in already there fully functional, hawatokaa watoke kuja kuzungumza na banks zetu huku ziweze kuruhusu kupokea hela, hilo ni swala inabidi ku-address banks zilizopo nchini kukubali hizi transactions.

Na hiyo petition ya kufanyika whatsapp, whats the point? Hizi whatsapp groups mambo ya kushare contacts watu wengine its not a risk we are willing to take. A phone number is much more than just a number.
 
DHL hawaitaji P. O Box, wanataka namba yako ya simu, na phyisical address yako, yani nyumba namba, mtaa, wilaya n.k, pia kama unapatikana maeneo ya kazini kwako muda wa mchana utawapa address ya ofisini kwako. Maana wao watakupigia simu kabla ya kukuletea mzigo wako, kama wataitaji maelezo ya ziada kuhusu mahali ulipo utawapatia.
Pia kama mzigo wako unahitaji lipiwa kodi yoyote watakupigia simu mapema kukueleza kiasi kinachotakiwa, kama ni kidogo utawaambia utalipa on delivery kama ni amount kubwa watataka ulipe kabisa ndio waendeelee na process za tra.

Kama mzigo haunda kodi kabisa utawalipa elfu27 nadhani ya handling na delivery.
Nashukuru sana kwa maelezo uliyonipa, kwa mfano kama nataka kutumia dhl address ninaandika vip? Maana nilitaka kununua nikahitajika kuandika address.
 

Asante sana mkuu nashukuru sana. Maana hiyo ndiyo ilikuwa inaniumiza kichwa.
 
Swala la paypal ni swala la BOT kuruhusu bank zetu za ndani ziruhusu malipo ya paypal, paypal hawana tatizo kama wakipata go ahead toka BOT then bank zetu zenyewe zitaifuata paypal kusign contract, hata pamoja na kenya kuruhu paypal sio bank zote zilizosign contract na paypal.

Na hiyo petition ya kufanyika whatsapp, whats the point? Hizi whatsapp groups mambo ya kushare contacts watu wengine its not a risk we are willing to take. A phone number is much more than just a number.
Mkuu be confident, ndio maana sijaja hapa na pseudoname ya jf, nimetumia jina la kweli kuweza organise watu, wala sihitaji pseudoname yako ya jf, ntachoitaji ni namba yako tuweze share idea tunafikia vipi goal letu, wewe ukianza ni whats app, sitoweza jua youf jf pseudoname!
Kuna professionals wengi wangependa pata huduma hii, na hatudeal na illegal stuffs, so kuwa na amani kama unaona unaguswa ungana nasi!
 
Wewe umeshawahi kununua kitu amazon au ebay? Lengo la swali hili ni ili unisaidie kwenye ishu ya shipping.
Ndiyo. Kwenye shipping kuna options tatu. Option ya kwanza ambayo ni nzuri na huitumia mara kwa mara ni ku-ship kwa mtu ambaye yupo US na anakaribia kuja. Hvyo mzigo hupelekwa kwake (hoteli au nyumbani) halafu anakuja nao.

Option ya pili ni kununua address ya US kupitia mtandao wa www.myus.com. Hapo utapewa virtual address yako ya US ambapo baada ya mzigo wako kufika pale, watakufahamisha na baadaye kukutumia kwa DHL/FedEx/EMS na kukukata gharama kupitia kadi yako ya benki (Visa/Mastercard). Advantage ni kwamba hata kama selller ha-ship nje ya US, bado utaweza kununua bidhaa yake.

Option ya tatu ni kuwapa address yako ya Tanzania na ila nadhani utaenda kuchukua mzigo wako DHL/FedEx kutegemea ni courier gani alisafirisha mzigo. Hawataleta nyumbani kutokana na kodi. Same na option ya pili, unless ulichonunua hakihitaji kulipiwa kodi. Kwa FedEx, experience niliyo nayo ni kwamba kama unatakiwa kulipa kodi, watakutumia kiwango cha kodi ya kulipa ambao utawalipa wenyewe, kabla ya kukuletea mzigo.
 
Naunga mkono hoja, binafsi Ni mhanga WA miaka nenda nenda Rudi, kazi zangu nyingi nauza nje, nipo registered kwenye Website flani kubwa Kama Freelancer! Nauza mzigo Na natakiwa nilipwe online kwa njia ya Paypal lakini haiwezekani, nimeshakosa pesa kibao Na kupoteza pesa kibao, nchi nyingine hawaruhusu kutumia Western Union kutuma pesa Africa, kwa sababu ya Frauds!.....lakini group ya Whatsapp unaweza kuwa jibu? Kwa nini kusiwe Na special thread hapa, watu wakawa wanatoa Mawazo Yao, Na wahusika wanaona, then kupitia hapa tunaweza ku- organize watu wachache Na kwenda kumwona ama Waziri wa fedha, BOT ama wabunge wachache wenye ushawishi huu ya hili, haiwezekani tuwe nyuma kwenye kila kitu!
 

Kuhusu option ya tatu, ya DHL nimejaribu kununua kitu (sustain pedal ya kinanda kutoka ebay) lakini sijapata option ya kutumia dhl, kilichoandikwa ni standard int'l shipping, naomba msaada kwa hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…