Paul Sozigwa amepotea katika mazingira ya kitatanishi

Paul Sozigwa amepotea katika mazingira ya kitatanishi

""Huyo mama nashauri atafutwe asadie polisi"" hii statement ya kidukuzi, umetumia akili sana huwezi jua nyuma ya pazia
 
poleni,na hongereni kwa kumpata baba yenu.those days niliwahi kusoma na mdada Neema Sozigwa pale Jangwani A level.
 
Umesimuliwa udaku nimeishi nao miaka yote sasa unaposema kila kitu sijui unamaanisha nn !! Huyu Moses ( aka bonge enzi za utotoni) tumesaga nae sana, mabasi na hata walipokuwa forodhani ilikuwa mara moja moja kuletwa na gari...tena asubuhi tu, mchana tunapiga mihogo kwa mzee Mselemo na kudandika ikarusi kwenda home..

Viatu ni bora tuu na hata watoto wa kawawa akina Amani walikuwa wanawacheka hawa..! Sasa wewe unataka kutuambia nn..? Sawa na haya majangili akina Rz1 ??

Dah!!!mzee mselemu na mihogo,ikarus kumbakumba!!! Unanikumbusha kitambo sana mkuu!!!
 
Tunawashukuru wote waliokuwa pamoja na familia katika suala hili. Mzee Sozigwa amepatikana jana usiku na amesharudi mikononi mwa familia!

Tuendelee kuombeana na kutiana nguvu katika kumtunza Mzee wetu. Anahitaji uangalizi wa hali ya juu sana, na hili limetupa fundisho litakalotusaidia siku zijazo. Pia nawaomba wanajamvi tuendelee kuelimishana na kuwaelimisha watu wengine ya kuwa kuna ugonjwa huu unaoitwa Alzheimer, ambao unakula ubongo na kufanya mtu kupoteza kumbukumbu. Ugonjwa hauna dawa ya kuuponya mpaka sasa, ila kuna dawa za kutumia mtu anapokuwa katika hatua za awali kuzuia usiendelee! Tafadhali tuwatazame na kuwachunguza wazazi na ndugu tulio nao ili kama mtu akionyesha dalili kama hizo awahi kupata dawa ili usiendelee.

Sina namna ya kuwashukuru zaidi ya kusema kutoka moyoni, ASANTENI SANA!

Mkuu Kiwi, hivi Diana mdogo wake Augustino na Tina wako wapi? Naikumbuka sana hii familia aisee.
 
Nishani wanakuja kupewa akina Anna Makinda, majina ya mitaa wanapewa akina Makamba na majina ya Shule wanakuja kupewa akina Mama Salma Kikwete..! Yaani nchi hii ukiamua kuyafikiria yanayoendelea unaweza wehuka wallah..!

Kura yako ndio chanzo cha mabadiliko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom