Paul Sozigwa amepotea katika mazingira ya kitatanishi

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Paul Sozigwa.jpg

Mr. Paul Sozigwa, aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari katika serikali ya Mwalimu Nyerere, amepotea tangu jana mchana katika mazingira ya kitatanishi. Mara ya mwisho alionekana kanisani Mbezi Beach BCIC (kwa Gamanywa) jana Jumapili saa nane mchana. Kupotea huku kunaleta mashaka hasa kwa kuwa Mzee Sozigwa ni mgonjwa wa Alzheimer, na mara nyingi anapoteza kumbukumbu. Taarifa ya kupotea kwake imeshatolewa polisi na kupatiwa RB.

Sozigwa with Cabinet.jpg

Vilevile kupotea huku kunasadikiwa kunahusiana na suala la mauzo ya nyumba yake ya Kurasini ambayo iliuzwa kinyemela na aliyekuwa mkewe Monica Kuga. Huyo mama aliachana na Mzee Sozigwa kwa takriban miaka 34 kuanzia mwaka 1973 mpaka mwaka 2009, aliporudi kwa madai ya kuja kusaidia matunzo ya Mzee Sozigwa. Wakati huo huo akafanya utapeli na kuuza nyumba ambayo tayari Mzee alishaandika wosia kabla ya kuugua na kumkabidhi mtoto wake wa kiume anayeitwa Moses Sozigwa. Hiyo nyumba bado ina kesi kwa kuwa tayari wakati inauzwa na Mama Monica Kuga ilishakuwa na zuio la mahakama.

Mara ya mwisho Mzee Sozigwa alikuwa amevaa shati jeupe lenye mistari ya bluu na kijivujivu, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Anapoulizwa anakaa wapi hujibu Kisarawe ama Vidunda, wilaya ya Kisarawe. Atakayemuona anaombwa kupiga simu zifuatazo:

Mch. Moses Sozigwa 0712 379818, 0755 716158

Mrs. Irene Yussuf 0784 300418

Ms. Lucy Paul Sozigwa 0755 564080, 0717 310783

Mrs. Judith Mlawa 0712 834737

Unaweza pia kuwasiliana nao kwa Whatsapp na Viber

Namkumbuka mzee Paul Sozigwa ndiye aliyemshauri Mwalimu Nyerere astaafu ili apishe watu wengine wasimamie mageuzi ya kiuchumi kwani asingeweza kupingana na misimamo yake.

Baada ya maelezo ya Sozigwa, mawaziri wanafiki kama Malechela walitegemea mwalimu angehamaki na kumfuta kazi mwalimu, badala yake mwalimu alikuwa mpole na kumsifu sozigwa kwa ushauri wake.

Baada ya kikao kile mwalimu alimwita Cleopa Msuya na kumpatia kazi ya kusimamia mageuzi kama alivyopendekezwa na tume ya Paul Bomani. Msuya akapewa kazi ya kuzungumza na world bank na IMF juu ya reforms za kiuchumi na hapo mzee akaanza safari ya kung'atuka.

Kwangu mie mzee Sozingwa kupotea kama mlevi wa kimpumu sikubaliani hata kidogo, nakumbuka mara ya mwisho nilimwona akiwa na Majidd Mjengwa Sweden alikokuwa kwa matibabu, chonde JK hakikisha huyu mzee anapewa heshima inayostahili.

===========================
===========================

Tunawashukuru wote waliokuwa pamoja na familia katika suala hili. Mzee Sozigwa amepatikana jana usiku na amesharudi mikononi mwa familia!

Tuendelee kuombeana na kutiana nguvu katika kumtunza Mzee wetu. Anahitaji uangalizi wa hali ya juu sana, na hili limetupa fundisho litakalotusaidia siku zijazo. Pia nawaomba wanajamvi tuendelee kuelimishana na kuwaelimisha watu wengine ya kuwa kuna ugonjwa huu unaoitwa Alzheimer, ambao unakula ubongo na kufanya mtu kupoteza kumbukumbu. Ugonjwa hauna dawa ya kuuponya mpaka sasa, ila kuna dawa za kutumia mtu anapokuwa katika hatua za awali kuzuia usiendelee! Tafadhali tuwatazame na kuwachunguza wazazi na ndugu tulio nao ili kama mtu akionyesha dalili kama hizo awahi kupata dawa ili usiendelee.

Sina namna ya kuwashukuru zaidi ya kusema kutoka moyoni, ASANTENI SANA!
 
Dah, poleni sana. Mungu awasaidie mzee Sozigwa aonekane.

But....haikuwa lazima sana kuelezea details za huyo mama na utapeli wake, kama ni kweli. Ficheni siri za familia. Ukiweza, edit please....

Ila hata kwa hilo, I wish you all the best.
 
hiyo issue sio Siri kama ni msomaji wa magazeti!ilisharipotiwa na mwananchi
 
Dah, poleni sana. Mungu awasaidie mzee Sozigwa aonekane.

But....haikuwa lazima sana kuelezea details za huyo mama na utapeli wake, kama ni kweli. Ficheni siri za familia. Ukiweza, edit please....

Ila hata kwa hilo, I wish you all the best.

Asante sana. Hakuna siri hii habari ilishatolewa kwenye gazeti la Mwananchi wiki mbili tatu zilizopita. Kwa kuficha siri za familia ndiko kulikotufikisha hapa, kwani watu wengi walituonya kuhusu utapeli tukaona tusiuweke hadharani. Matokeo yake hatujui baba alipo na mama anagoma kutoa ushirikiano. Kwa mfano baba alipotea tangu jana mchana na yeye hakutoa taarifa kwa mtu yeyote wala polisi mpaka watoto tuliposituka wakati giza linaingia. Maombi yanahitajika sana. Tunashukuru kwa faraja!
 
Nakumbuka huyu Mzee alikuwa na kesi ya ndoa aliyofungua huyo mkewe kudai waachane.Kesi ilikuwa Kisutu sikujua iliishaje.Ila kwakweli kazi aliyofanya kwa taifa hili,Mzee huyu hakustahili kuhangaika namna hii.
 
Aisee poleni sana.

BTW:Habari ya huyu mzee Sozigwa na familia yake iko humu jamvini nadhani ilikuwa inahusu huo mvutano wa nyumba kati ya watoto na mama yao.
 
Ugonjwa huo alionao humfanya mtu kusahau kurudi nyumbani.atakuwa anatembea bila kujua aendako.poleni sana.
 
Watu wa aina hii waliolitumikia Taifa yangu enzi za Uhuru walipaswa kutazamwa kwa karibu. Mzee kaachwa aishi kilofa kana kwamba hakuna la maana alilofanyia Taifa hili. Utawala huu ndo umemuumiza kabisa huyu mzee baada ya kubeba mafaili yaliyojaa 'escrow' za Dk. JK. Mungu ni mwema. Tuongeze dua.
 
Asante sana. Hakuna siri hii habari ilishatolewa kwenye gazeti la Mwananchi wiki mbili tatu zilizopita. Kwa kuficha siri za familia ndiko kulikotufikisha hapa, kwani watu wengi walituonya kuhusu utapeli tukaona tusiuweke hadharani. Matokeo yake hatujui baba alipo na mama anagoma kutoa ushirikiano. Kwa mfano baba alipotea tangu jana mchana na yeye hakutoa taarifa kwa mtu yeyote wala polisi mpaka watoto tuliposituka wakati giza linaingia. Maombi yanahitajika sana. Tunashukuru kwa faraja!

Huyo Mwanamke Alaaniwe Milele
 
Watu wa aina hii waliolitumikia Taifa yangu enzi za Uhuru walipaswa kutazamwa kwa karibu. Mzee kaachwa aishi kilofa kana kwamba hakuna la maana alilofanyia Taifa hili. Utawala huu ndo umemuumiza kabisa huyu mzee baada ya kubeba mafaili yaliyojaa 'escrow' za Dk. JK. Mungu ni mwema. Tuongeze dua.

Nishani wanakuja kupewa akina Anna Makinda, majina ya mitaa wanapewa akina Makamba na majina ya Shule wanakuja kupewa akina Mama Salma Kikwete..! Yaani nchi hii ukiamua kuyafikiria yanayoendelea unaweza wehuka wallah..!
 
Nakumbuka ile filamu ya Serengeti shall not die yeye ndiye aliyetafsiri kwa kiswahili...ilituhamasha kufanya utalii wa ndani kwenda serengeti.mambo hii siku hizi hakuna.
 
Poleni sana,Mungu ni mwema atawasaidia.
Huyo mama nashauri atafutwe asadie polisi
Haya mambo yameanza na mzee mwenyewe
yanaweza pia kuhatarisha maisha ya huyo
mwanae aliyemlithisha nyumba,
Naomba vyombo vya dola vimfuatilie huyo
mama na wanunuzi wa nyumba ili kujiridhisha.
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV saa 2 usiku huu kuwa Mzee Paul Sozigwa amepotea nyumbani kwake Magomeni. Huyu mzee alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM zama za Mwalimu JKN
 
Back
Top Bottom