Tunawashukuru wote waliokuwa pamoja na familia katika suala hili. Mzee Sozigwa amepatikana jana usiku na amesharudi mikononi mwa familia!
Tuendelee kuombeana na kutiana nguvu katika kumtunza Mzee wetu. Anahitaji uangalizi wa hali ya juu sana, na hili limetupa fundisho litakalotusaidia siku zijazo. Pia nawaomba wanajamvi tuendelee kuelimishana na kuwaelimisha watu wengine ya kuwa kuna ugonjwa huu unaoitwa Alzheimer, ambao unakula ubongo na kufanya mtu kupoteza kumbukumbu. Ugonjwa hauna dawa ya kuuponya mpaka sasa, ila kuna dawa za kutumia mtu anapokuwa katika hatua za awali kuzuia usiendelee! Tafadhali tuwatazame na kuwachunguza wazazi na ndugu tulio nao ili kama mtu akionyesha dalili kama hizo awahi kupata dawa ili usiendelee.
Sina namna ya kuwashukuru zaidi ya kusema kutoka moyoni, ASANTENI SANA!