Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kujua kipi useme, useme wapi, wakati gani, na kwenye mazingira gani, kunahitaji akili ya kiwango fulani. Kama huna hiyo akili utabakia kuropoka chochote, wakati wowote na mahali popote.

Rais Samia ameyataka mwenyewe. Hakuna aliyemlazimisha amteue Makonda kwenye nafasi yoyote ile. Haya ni madogo, asubirie makubwa zaidi. Magufuli aliamua kuachana naye kabisa alipokuja kugundua kuwa aliyekuwa anamwamini alikuwa tapeli. Akaenda kugombea ubunge huku akiwadanganya watu kuwa ametumwa na Magufuli agombee ubunge ili ateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani. Hayati Magufuli alipoambiwa, aling'aka na kusema kuwa yeye hajamtuma mtu yeyote akagombee ubunge. Ndipo akaomba arudi kwenye ukuu wa mkoa, marehemu akamkatalia katakata, wakati huo akiwa tayari amefikishiwa taarifa kuwa jamaa amewatapeli GSM nyumba kwa kuwadanganya kuwa Rais alikuwa ameomba wamjengee, kumbe ni yeye ndiye aliyekuwa anahitaji kujengewa nyumba. Hapo akawa takataka mbele ya JPM.

Samia, takataka aliyoitupa mtangulizi wake, ameiona lulu. Asubirie kashfa zitakazompata kwa kupitia huyu mtu. Atapora magari, fedha na nyumba za watu kwa kutumia jina la anayemwita eti ni mama yake. Rais ameyataka mwenyewe, hajajua kuwa tumbili huwa hafugiki.
Unauzungumziaje ukimya wa zaidi ya wiki wa Waziri wa habari kabla ya kumshambulia RC?
 
Above 35 yrs kwangu wote hao ni wastaafu,nchi inatakiwa ijengwe na vijana wa 18yrs hadi 30yrs,sasa huyu suspect wa mauaji,utekaji etc etc why achukiwe na pensioners?Bunge letu love limejaa vizee vyenye kusinzia bungeni,na wengi wao hawana jipya ni kama wimbo uliorekodiwa ,utakua unajirudia tena,Urais wangu nitawastaafisha wote above 35 yrs na kuajiri young women &men ili waipe nchi directions mpya,na elewa btn 18 yrs to 35 yrs ndio kwenye wasomi wengi na wengi wao ni unemployment
 
Habari wana Jf
Kama ilivyo kawaida nimechunguza sana Kwa nini ndugu poul makonda anachukiwa sana,na watanzania wenye huo umri nilioutaja hapo.
Nimegundua ni kupitwa kwa mafanikio,nimekuja kuona wanatanzania kinachotusumbua ni wivu wa mafanikio ya mtu.

Leo hii hata makonda akiongea jema vipi bado watanzania wataendelea kumsakama acheni wivu huo na roho mbaya poul makonda mungu kampa kipaji cha kuongoza watu na anavitu vingi sana kwake na kama watanzania tunatakiwa kujifunza kupitia yeye poul makonda.

Chukua hii Kama hamjui

Kitendo cha Rais @SuluhuSamia kumrudisha Makonda kwenye siasa ni kwasababu kuna mahali amezidiwa nguvu. Makonda ni yule kijana asiye na soni, mwenye kufanya/kuongea yale ambayo wakubwa hawawezi kuyaongea wenyewe.
Hapa, Makonda ni kipaza sauti tu,na anakipawa cha uongozi

Ukweli nimefurahi sana mh rais wetu wa JMT kumchagua poul makonda kurudishwa katika nafasi inatakiwa Tanzania tupate vijana Kama 50 au 100 Kama alivyo poul makonda hii nchi tungekuwa mbali sana.

Watanzania tuigeni mfano kwa ndugu mh.poul makonda tuacheni wivu na chuki tufanyani kazi kutwa tunamtaja makonda bora tungemtaja kwa mema ila Watanzania tunamtaja makonda kana kwamba yeye sio binadamu kila baya anatupiwa yeye.

Watanzania wooote inatakiwa tumuunge mkono poul makonda,huyu ni adhina ya taifa.
Ahsante mh.raisi kwa kumrudisha ndugu poul makonda huyu atakusaidia sana katika kuijenga nchi.

Sisi wengine tumekalia kukosoa na kupiga majungu.
Mungu mlinde ndugu poul makonda
Mungu mlinde mh raisi wetu JMT

NAKARIBISHA MAONI.
KIKUBWA ACHANENI NA WIVU WA PAMOJA NA ROHO MBAYA.
ndio urika wake huo gubu haziepukiki...

kila moja anatamani awe kama yeye Lakini ndio hivyo tena haiwezikani.. ...

hata hivyo ni vizuri kua na wivu,

Lakini, wa kimaendeleo na huo wivu, ukusaidie kufanya kazi kwa bidii, na maarifa zaidi, ili hata kama hutafikia alikofika Makonda basi angalau umkaribie kiuchumi, kisiasa na hata kijamii 🐒

wivu wa malalamiko tu na mihemko ni useless kabisa 🐒
 
Tamko alilotamka Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni tamko mbaya sana na linaleta uchochezi na chuki. Ni aibu kutamka mbele ya kadamnasi ya watu kuwa kuna watu wanamtukana Mhe. Rais. Jambo hili alitakiwa amueleze Mhe. Rais kwa siri kubwa. Mhe. Rais Mkuu wa Mkoa wa Arusha hakufai ni bora umtumbue mapema atakuletea uadui mkubwa na Watanzania. Kikubwa anajipendekeza kwako.
Umenena
 
Kwa sababu wa chini ya umri huo Bado nyie Mko kwenye foolish age mnaongozwa na mihemko na ni rahisi kuwa manipulated na Wanasiasa wanaojua siasa za ulaghai kama kina Makonda and the likes.

Kuanzia umri huo ni watu waliopevuka wanajua nyie wajinga mnafanywa ngazi huku mnachekelea Kwa sababu hamjitambui.
Wanampendes makarios
 
Tupunguze chuki za wazi wazi kwa konda
Najua weng hatumpend ila ifike hatua tuache chuki zidi yake tuache afanye kaz
Jf kuna nyuzi zaidi ya 10 juu ya makonda mnaweza zani mnamshusha kumbe ndo mnazidi mpandisha na kumtengenezea jina zaidi na mwisho wa sku atakuja pata cheo kikubwa iv iv
Konda ni mkuu wa mkoa wa Arusha cheo ambacho ni kdg sana ebu wachni apige kaz
Kabisa !
Jamaa nyota inang’ara zaidi !
Inasemekana kwamba ukiona mtu anasemwa sana hata kwa ubaya maana yake ni kwamba jamaa huyo anatisha mbele ya macho ya maadui zake 🙏🙏
 
ccm inajulikana, hasa ikiwa inakaribia kipindi cha uchaguzi... Figisu za hapa na pale, kuraruana makucha, mwisho wa siku lao ni moja
Kikipita kipindi hiki,wengine watu wengine watavuka wakiwa hata masikio wakiwa hawana🤔 au hata vichwa😁
 
Tamko alilotamka Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni tamko mbaya sana na linaleta uchochezi na chuki. Ni aibu kutamka mbele ya kadamnasi ya watu kuwa kuna watu wanamtukana Mhe. Rais. Jambo hili alitakiwa amueleze Mhe. Rais kwa siri kubwa. Mhe. Rais Mkuu wa Mkoa wa Arusha hakufai ni bora umtumbue mapema atakuletea uadui mkubwa na Watanzania. Kikubwa anajipendekeza kwako.
Watanzania wanakushangaa wewe yaani tangu lini Makonda aliwahi kuwa na busara?

Huyo yupo pale kutafuta kujikomba na wenzake waonekane hawana thamani mbele ya Rais.

Makonda hana uwezo wa kuwa kiongozi popote pale
 
Back
Top Bottom