Ulimsikia Juma Farijala aliposema JK anamiliki mbingu na ardhi?
Kipind hiki huwa nakifuatilia kila siku ya jumamosi
Mara nyingi
James Range mtangazaji wa Star tv hayuko makini na zaid yupo kiccm, anaowaalika mara nyingi ni makada wa ccm na michango yao ni ya ovyo wala Range hawasahihishi wanapopotoka.
Juma Farijala mmoja kati ya wazee wa ccm alikosa staha kabisa katika kuchangia kwake
1. Anasema mwangosi aliuwawa kwa bahati mbaya!!!
polisi 7 chini ya mkuu wa polisi kamuhanda ni bahati mbaya kwa misingi gani?
2. Anasema hata yazanziba kama sijakosea ni bahati mbaya!!! mzee huyu anapochangia hugeuka hakim nakuipa serikali uhalali kwa kila jambo.
3. polisi na mauwaji kule kagera .........Polisi si kwamba hawana akili......
Huyu mzee mara kwa mara anaitwa na james range kuitetea serikali ya ccm bila aibu.
Mkwawa mgeni star tv Dar es salaam
Ameongea mengi, lakini binafsi ameniudhi sana kuliponda mwanahalisi (mimi naamini mwanahalisi ndilo gazeti bora kabisa tanzania, lililozingatia uwazi katika kuripoti mambo mbalimbli kwa maslahi ya watanzania)
Sikuelewa lengo La Mhadhili Mkwawa, anapendelea udaku na mipasho ya Magazeti ya Uhuru na habari leo? au ule ubabaishaji wa TBC kuitangaza CCM kama vile ni chombo cha chama na si watanzania wote.
Mwisho nimpongeze
Doto Bulendu mtangazaji Star tv Mwanza. Vipindi vyake vyote yuko makini sana katika kuongoza mijadala na inapotokea mgeni kutoka nje ya mjadala makusudi au kwa bahat mbaya Doto huingilia kati na kurekebesha mambo.