Paul Makonda awavuruga CHADEMA hata kabla hajashika maiki na kuunguruma

Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika CHADEMA wamepigwa na kitu kizito kwelikweli kichwani mwao kilichopelekea kuvurugika akili zao. Uteuzi wa komandoo Makonda umewapiga sindano ya ganzi na kupooza miili yao na akili, kujawa na hofu na uoga wa hali ya juu sana.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa CHADEMA nzima haina mtu wa kuweza kupambana na Makonda jukwaani na mahali popote pale. Ndio maana unaona namna wanavyohangaika na jina la Makonda hata kabla hajafungua kinywa chake kuunguruma na kuzungumza.

Wanatambua Makonda ni silaha ya maangamizi kwa hoja dhaifu na siasa za matukio walizozizoea CHADEMA kutembea nazo. Sasa kwa Makonda ndio mwisho wao,n dio mwisho wa pumzi yao iliyokuwa imesalia katika mtungi wa hoja zao dhaifu.

CHADEMA wanajuwa komandoo Makonda ni jasiri, shupavu, madhubuti, imara na hodari sana wa siasa hapa nchini. Wanajuwa nguvu kubwa ya kihoja aliyonayo Makonda, wanajua ushawishi alionao na namna alivyo maridadi na hodari katika kupanga mipango mikakati ya ushindi katika vita na mapambano ya kisiasa.

Wanajua jina tu la Makonda ni kampeni na ushindi tosha, ndio maana tangia ameteuliwa muda wote wanamjadili kwa hofu na uoga, wanajuwa Makonda ni mkubwa kuliko kamati kuu yao yote.

Wanasema ukiona adui yako analia lia juu ya silaha unazotumia basi jua ameshaona kiama na mwisho wake, ameshaona kuwa hana uwezo wa kusimama nawe katika uwanja wa mapambano. Sasa CHADEMA wameshajua kuwa wanakwenda kupoteza mapambano yote mbele ya legendari Paul Makonda.

CHADEMA endeleeni kutulia hivyo hivyo na msijifaye mmekuwa washauri wa CCM au kujifanya mnaipenda sana CCM kwa sasa. Sahauni ushindi wa aina yoyote ile katika uchaguzi wowote ule na wa ngazi yoyote ile maana mnamfahamu vyema Makonda kuwa ni mtu wa kazi juu ya kazi, mguu kwa mguu mpaka kieleweke.

Tafuteni ajenda na siyo kurukia vimatukio vya kupita, maana mtaumia sana mbele ya CCM hii ya Rais Samia iliyojaa manguli na wabobezi wa sayansi ya siasa na wenye mipango ya kisayansi kwa kila jambo.

Oneni namna suala la Bandari mlivyoangukia pua baada ya serikali kuja na mkataba ulio pongezwa na kila mtu kutoka kila pande ya nchi yetu na kupokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania.

Sasa wameanza kuhamisha magoli kwa kusema eti mkataba uwekwe hadharani pasipo kutuambia ni wapi Duniani ambako mikataba ya kibiashara na kiuwekezaji huwa inawekwa hadharani kama nguo za mtoto.

Hiyo yote ni baada ya kuishiwa hoja na ajenda hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa CHADEMA hainaga ajenda inazosimamia zaidi ya kudandia vimatukio ambavyo hutupiwa kama mfupa ili kuwavuruga, hasa kwa kutambua ukweli kuwa CHADEMA ni mkusanyiko wa watu wenye uwezo mdogo wa kuchanganua mambo na kuelewa mambo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Tutazidi kumuombea. sema Makonda ni kama kinyonga anajua kubadilisha rangi zake zote...
 
Mwamba
Screenshot_20231024-110245.jpg
 
heshima na adabu zimepunguwa sana ndani ya CCM. Lazima wawepo watu wa kashikashi.

Tunamtaka na mwanaharakati huru, msiba nae arudi ulingoni.

Kiukweli, upande wa uenezi CCM kumepwaya sana. Natumai Makonda ataendesha kazi hizo kwa staili ya mama ya R R R R.
 
heshima na adabu zimepunguwa sana ndani ya CCM. Lazima wawepo watu wa kashikashi.

Tunamtaka na mwanaharakati huru, msiba nae arudi ulingoni.

Kiukweli, upande wa uenezi CCM kumepwaya sana. Natumai Makonda ataendesha kazi hizo kwa staili ya mama ya R R R R.
Katibu uenezi Ccm ana kila kitu lkn idara kweli ilipwaya, PM anaenda kuboresha zile Media ,kuanzia Uhuru gazeti,Radio hadi Channel Ten, kuna vilaza kibao huko
 
Makonda na Sabaya ndio walikuwa doa la awamu ya tano. Wengi walimkubali JPM na mipango yake na utendaji kazi wake lakini wakaushusha thamani urais wake kwa kukumbatia unyama walioufanya Sabaya na Makonda.

Samia anatafuta kuungwa mkono na kanda ya ziwa na anaeleweka kwanini kamrudisha Makonda, hataki kupoteza ushawishi wa CCM wa kanda ya ziwa.
Haya uliyoyaeleza ni kweli kabisa, lakini huyu Lucas na vibaraka wenzake hawawezi kukuelewa. Samia yuko Smart la sivyo angeshamrudisha Makonda muda mrefu kutokana na ukaribu wao.

Pamoja na kutafuta uungwji mkono kanda ya Ziwa, lakini ssh aangalie Makonda anaweza akawa doa kubwa sana lisiloweza kusafishika ktk utawala wake. Ni mtu mwongo, anaependa kujipendekeza, siasa za kibabe, vitisho na kulewa madaraka. Sifa za aina hii alizipenda jpm lakini ilifika pahala nae alishaanza kumchoka.
 
Bashite atakupigia ameona namba yako hapo juu.
Ni hasara kubwa baba yako kumwaga mbegu zake na hatimaye wewe kuzaliwa.
Nampa pole za dhati kabisa bora angepiga nyeto ingesaidia sana.
Kwani ungemjibu kwa ustaarabu kwa hoja zenye mashiko ungepungukiwa nini. Tabia hizi za matusi na kejeli ni za watu waliokosa kuelimika na wasio wastaarabu
 
Back
Top Bottom