McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetenga mfuko wenye Sh50 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha vijana wanaojihusisha na sekta ya ubunifu nchini, hatua inayolenga kukuza uchumi wa ubunifu na kutoa fursa zaidi za kiuchumi kwa vijana.
Akizungumza jijini Arusha jana Machi 11, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda alisema mfuko huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sekta ya habari, sanaa na ubunifu.
Alisema, awali Wizara ilikuwa imepangiwa Sh20 bilioni lakini baada ya mazungumzo na Benki ya CRDB, kiwango hicho kimeongezwa na kufikia jumla Sh50 bilioni ili kupanua wigo wa vijana watakaonufaika na mfuko huo.
Alieleza kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni tarehe rasmi ya uzinduzi wa mfuko huo, ambapo baada ya uzinduzi fedha hizo zitaanza kutolewa kwa vijana waliopo katika sekta ya habari, sanaa na ubunifu ili kuwawezesha kukuza kazi zao na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.
“Wizara inapanga kuzindua rasmi mfuko huo katika hafla maalum inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, ambapo Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.”