Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,084
*MAKONDA AKAMATWE*
*Taarifa Kwa Umma*
Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda ya kusema "atakaye nunua makontena yaliyopo Bandarini atalaanika pamoja na kizazi chake";
Ni kauli ya vitisho yenye nia ya kuzuia Serikali isipate na isikusanye mapato kutoka kwenye makontena hayo.
Wafanyabiashara wataingia hofu juu ya kauli hiyo kwasababu tu imetolewa na Paul Makonda, mtu ambaye pia amepewa mamlaka ya kiserikali ya kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam (ikiwemo na bandari yake)
Wananchi wanasababu ya kuingiwa hofu ya kununua makontena hayo kwani Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa), ana uwezo wa kutumia vibaya madaraka aliyopewa kufanya visa, fitina na hujuma zaidi dhidi ya biashara au shughuli za mwananchi atakayenunua makontena hayo ili aweze kutimiza kila alichokiita "laana ya kizazi hadi kizazi".
Kwa serikali inayosimamia utawala bora na utawala wa sheria; na iliyojipambanua kuwa haina mchezo na watu wanaohujumu mapato ya serikali; kwa namna yoyote ile inapaswa mara moja kumkamata Paul Makonda na kumchukulia hatua kali za kinidhamu na kimahakama bila kujali cheo chake.
Ni vema ikakumbukwa na kuzingatiwa kuwa kufanya hujuma kwa nia ya kuikwamisha serikali isipate mapato ni kosa kwa mujibu wa sheria na ni uhujumu wa uchumi kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi.
Kiongozi anatakiwa kuwa mfano bora katika Jamii. Tulitegemea Mkuu wa Mkoa awe mstari wa mbele katika kulipa na kuhamasisha ulipaji wa kodi na kuisaidia serikali kupata mapato kila penye fursa ya serikali kupata mapato.
Aidha, moja ya kosa kubwa kabisa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni ukwepaji wa kodi. Mkuu wa Mkoa amekosa sifa za kuendelea kuwa Kiongozi na hivyo naitaka mamlaka yake ya uteuzi pia itengue uteuzi wake mbali ya kumchukulia hatua nyingine kali za kisheria.
Imetolewa Na;
Henry Kilewo
Katibu Dar es Salaam Kuu (Chadema)
28/08/2018
Sent using Jamii Forums mobile app