Paul Makonda akamatwe kwa kudhamiria kuhujumu zoezi la ukusanyaji kodi

Ninavyo mjua jiwe hana urafiki wa kudumu lolote laweza kutokea, kama ilivyokuwa kwa mhongo na nchemba mwiguru

Sent using Jamii Forums mobile app
Twasubiri tuone, Mwana mpendwa wa Mfalme Jiwe, Prince Makonda mwana wa Bashite, atațokewa na nini. Ingekuwa maneno aliyoyasema yametokea kwa mmoja wa waliyo upinzani, ungewasikia wengi tu pamoja na mbwa koko wanabweka. Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa sana
1. Huyu anakwepa kodi

2. Nikiongozi wa kitaifa ngazi ya mkowa

3. Mkowa wake upepata mapato ya chini kabisa

Haiwezi kuwa sahihi akaachwa,
-anakwepa kulipa kodi
-anakoseha serikali mapato
-hana maadili wala weledi
-haiwezi kuwa mfano bora...hafai

Ilikuifanya serikali kuonekana bora, makini na hainamzaha kwenye kukusanaya kodi, kuhakikisha viongozi wanakuwa na maadili

HAKUNA NAMNA
a) Makonda avuliwe madaraka

b) Makonda afikishwe mahakamani

AMEKUBALI KUWA MALI NIYAKE NA HIVYO LAZIMA AWAJIBIKE LA AWAJIBISHWE MARA MOJA
Mkowa ndiyo kitu gani??
 
Lo wapo watu wako juu ya sheria iwe wameumbwa hivyo au ndio wateule wa ngazi ya juu.
Usitegemee kabisa Makonda kukamatwa,muulize Sinde Warioba.
 
Nasubiri mwenye mamlaka ya teuzi yupo njiani mchana alikuwa Singida najua anakaribia kufika sasa
 
Kilewo ndio kupata pa kulipiza kiasi baada ya kushurutishwa kulea watoto aliozaa na Joyce Kiria.
 
*MAKONDA AKAMATWE*

*Taarifa Kwa Umma*

Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda ya kusema "atakaye nunua makontena yaliyopo Bandarini atalaanika pamoja na kizazi chake";

Ni kauli ya vitisho yenye nia ya kuzuia Serikali isipate na isikusanye mapato kutoka kwenye makontena hayo.

Wafanyabiashara wataingia hofu juu ya kauli hiyo kwasababu tu imetolewa na Paul Makonda, mtu ambaye pia amepewa mamlaka ya kiserikali ya kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam (ikiwemo na bandari yake)

Wananchi wanasababu ya kuingiwa hofu ya kununua makontena hayo kwani Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa), ana uwezo wa kutumia vibaya madaraka aliyopewa kufanya visa, fitina na hujuma zaidi dhidi ya biashara au shughuli za mwananchi atakayenunua makontena hayo ili aweze kutimiza kila alichokiita "laana ya kizazi hadi kizazi".

Kwa serikali inayosimamia utawala bora na utawala wa sheria; na iliyojipambanua kuwa haina mchezo na watu wanaohujumu mapato ya serikali; kwa namna yoyote ile inapaswa mara moja kumkamata Paul Makonda na kumchukulia hatua kali za kinidhamu na kimahakama bila kujali cheo chake.

Ni vema ikakumbukwa na kuzingatiwa kuwa kufanya hujuma kwa nia ya kuikwamisha serikali isipate mapato ni kosa kwa mujibu wa sheria na ni uhujumu wa uchumi kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi.

Kiongozi anatakiwa kuwa mfano bora katika Jamii. Tulitegemea Mkuu wa Mkoa awe mstari wa mbele katika kulipa na kuhamasisha ulipaji wa kodi na kuisaidia serikali kupata mapato kila penye fursa ya serikali kupata mapato.

Aidha, moja ya kosa kubwa kabisa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni ukwepaji wa kodi. Mkuu wa Mkoa amekosa sifa za kuendelea kuwa Kiongozi na hivyo naitaka mamlaka yake ya uteuzi pia itengue uteuzi wake mbali ya kumchukulia hatua nyingine kali za kisheria.

Imetolewa Na;

Henry Kilewo
Katibu Dar es Salaam Kuu (Chadema)
28/08/2018

Sent using Jamii Forums mobile app
Utapata tabuu sanaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema mtu atalaanika au watu watalaanika si kosa la kupelekea mtu kukamatwa.

Mambo ya laana ni mambo ya kiimani.

Ni lini Tanzania tumeanza kuadhibu watu kwa sababu ya imani zao?

Tuadhibu matendo. Siyo imani.
Hata maombi ya Lissu kanisani ilikuwa ni ya kiimani pia!
 
"Ni vema ikakumbukwa na kuzingatiwa" kwamba "mimi sipangiwi, sishinikizwi. Unaposhinikiza ndio unaharibu kabisa. Kachape kazi kijana."
Watu wengine mna vichwa ngumu. Sijui muambiweje ndio muelewe!
Kwani mhusika alipoyasema hayo maneno ya 'laana' alikuwa hajui?
Mleta hoja unajuaje kwamba laana aliyoielezea kuwa itawapata hao wanunuzi itakuwa ni kutoka kwa 'mungu' anayemuelewa na kumuamini yeye!
 
Enzi za nyerere angesikiwa tuu ameleta makontena 36 yeye binafsi angekua kijijini saa hii chini ya uangalizi.Vijizawadi vinatia shaka sana

Wanikumbusha aliekuwa waziri wa uchukuzi, mzee John Malecela, aliesema kwamba wale wote wanaolalamika kuna shida ya usafiri reli ya kati "they can go to hell".. Saa mbili usiku kwenye taarifa ya habari RTD, tukasikia yeye ndo ame-go kwa hell..
 
Makonda wakamatwe kwa kweli itakuwa safi sana

Makonda ni mnafiki sana. Sijui ni kwa nini watu wa ovyo kama hawa Jiwe kawapa uongozi.
He is such a coward. Wenye hela zenu kachukueni mzigo wake bandarini. Msibabaishwe na vitisho vya kizamani alivyovitoa.
Mara nyingi watu wasiojiamini na waliojaa unafiki na undumilakuwili kama Makonda humsingizia Mola hata kwa mambo ya kipuuzi.
Pamoja na pomposity zake jamaa ajue .... The law is the law. Aache kukwaza wenzie bwana.
 
Back
Top Bottom