Tarishi
Senior Member
- May 9, 2008
- 103
- 133
*KIONGOZI WANGU ZITTO KABWE USITUYUMBISBE*
Anaandika Paul Kerra mwanaACT Kinondoni.
Nimesikia leo kiongozi wangu wa Chama amezungumza na wanahabari.Kwa niliyoyasikia aliyoongea nimezidi kuona kiza mbele ya chama.Nitatoa mifano:
1.Kwanza mimi ni mwanachama ambaye kila siku niko karibu na tawi langu sijasikia tukiulizwa ili kutoa maoni juu ya maamuzi magumu ambayo tunashangaa tu yametangazwa.Haujaja waraka wowote kwa wanachama.Hii ndi demokrasia ya kuendesha chama?
2.Nasikitishwa Zito analalamikia Demokrasia wakati ndani ya Chama sasa ni kama vile nafasi za uongozi wa juu kwa sasa anazishikilia mwenyewe zote na ndiye mwamuzi wa kila kitu akiamua mkutano upi ukae upi usikae na kuchagua agenda zake. Nafasi ya matawi haipo.
3. Nasema hivi kwa sababu ni wazi tamko la kususia uchaguzi si la Chama sisi hapa ktk jimbo letu kuna mgombea wetu makini msomi na mwenye maono tulishamwandaa...tamko la kutoshiriki uchaguzi kapata wapi uhalali?
4.Nimeona anasimamia mambo yasiyo na tija mara IMF mara uchumi.Hafanyi utafiti anakidhalilisha Chama.Juzi Serikali imefafanua kwa hoja mambo hayo yeye anaropokaropoka tu na kutupa wakati mgumu kujibu hoja.Kwa sasa hatujui maoni yake binafsi na yale ya Chama ni yapi.
4.Ameonesha udhaifu mkubwa kuungana na Ukawa kususia uchaguzi wa marudio.Kiongozi Zito sio mtu wa kuaminika tena ni mnafiki...imetuuma sana wanachama. Leo anaungana na Ukawa watu aliopata kuliambia Taifa kuwa ni "walaghai wakubwa?"
5.Ametulaghai wafuasi wake na wanaomfadhili nje ya nchi kuwa eti Demokrasia inabanwa.Naanza kuamini kuna.mambo yake binafsi yamebanwa.Hii ilikuwa fursa ya chama kwenda kwa wananchi na kufanya siasa unaikataaje.Tunaikimbiaje kwa hoja dhaifu hivi?
6. Leo anajifanya kuguswa na maslahi ya wafanyakazi wakati Chamani kwake kunawaburuta watendaji wake...wako hoi na haki zao zinabanangwa.Niko hapa watendaji wako hoi na hakuna hata mawasiliano na makao makuu.
Inauma sana.