Paul Kerra: Kiongozi wangu Zitto Kabwe usituyumbishe

Tarishi

Senior Member
May 9, 2008
103
133
*KIONGOZI WANGU ZITTO KABWE USITUYUMBISBE*

Anaandika Paul Kerra mwanaACT Kinondoni.

Nimesikia leo kiongozi wangu wa Chama amezungumza na wanahabari.Kwa niliyoyasikia aliyoongea nimezidi kuona kiza mbele ya chama.Nitatoa mifano:

1.Kwanza mimi ni mwanachama ambaye kila siku niko karibu na tawi langu sijasikia tukiulizwa ili kutoa maoni juu ya maamuzi magumu ambayo tunashangaa tu yametangazwa.Haujaja waraka wowote kwa wanachama.Hii ndi demokrasia ya kuendesha chama?

2.Nasikitishwa Zito analalamikia Demokrasia wakati ndani ya Chama sasa ni kama vile nafasi za uongozi wa juu kwa sasa anazishikilia mwenyewe zote na ndiye mwamuzi wa kila kitu akiamua mkutano upi ukae upi usikae na kuchagua agenda zake. Nafasi ya matawi haipo.

3. Nasema hivi kwa sababu ni wazi tamko la kususia uchaguzi si la Chama sisi hapa ktk jimbo letu kuna mgombea wetu makini msomi na mwenye maono tulishamwandaa...tamko la kutoshiriki uchaguzi kapata wapi uhalali?

4.Nimeona anasimamia mambo yasiyo na tija mara IMF mara uchumi.Hafanyi utafiti anakidhalilisha Chama.Juzi Serikali imefafanua kwa hoja mambo hayo yeye anaropokaropoka tu na kutupa wakati mgumu kujibu hoja.Kwa sasa hatujui maoni yake binafsi na yale ya Chama ni yapi.

4.Ameonesha udhaifu mkubwa kuungana na Ukawa kususia uchaguzi wa marudio.Kiongozi Zito sio mtu wa kuaminika tena ni mnafiki...imetuuma sana wanachama. Leo anaungana na Ukawa watu aliopata kuliambia Taifa kuwa ni "walaghai wakubwa?"

5.Ametulaghai wafuasi wake na wanaomfadhili nje ya nchi kuwa eti Demokrasia inabanwa.Naanza kuamini kuna.mambo yake binafsi yamebanwa.Hii ilikuwa fursa ya chama kwenda kwa wananchi na kufanya siasa unaikataaje.Tunaikimbiaje kwa hoja dhaifu hivi?

6. Leo anajifanya kuguswa na maslahi ya wafanyakazi wakati Chamani kwake kunawaburuta watendaji wake...wako hoi na haki zao zinabanangwa.Niko hapa watendaji wako hoi na hakuna hata mawasiliano na makao makuu.

Inauma sana.
 
*KIONGOZI WANGU ZITTO KABWE USITUYUMBISBE*

Anaandika Paul Kerra mwanaACT Kinondoni.

Nimesikia leo kiongozi wangu wa Chama amezungumza na wanahabari.Kwa niliyoyasikia aliyoongea nimezidi kuona kiza mbele ya chama.Nitatoa mifano:

1.Kwanza mimi ni mwanachama ambaye kila siku niko karibu na tawi langu sijasikia tukiulizwa ili kutoa maoni juu ya maamuzi magumu ambayo tunashangaa tu yametangazwa.Haujaja waraka wowote kwa wanachama.Hii ndi demokrasia ya kuendesha chama?

2.Nasikitishwa Zito analalamikia Demokrasia wakati ndani ya Chama sasa ni kama vile nafasi za uongozi wa juu kwa sasa anazishikilia mwenyewe zote na ndiye mwamuzi wa kila kitu akiamua mkutano upi ukae upi usikae na kuchagua agenda zake. Nafasi ya matawi haipo.

3. Nasema hivi kwa sababu ni wazi tamko la kususia uchaguzi si la Chama sisi hapa ktk jimbo letu kuna mgombea wetu makini msomi na mwenye maono tulishamwandaa...tamko la kutoshiriki uchaguzi kapata wapi uhalali?

4.Nimeona anasimamia mambo yasiyo na tija mara IMF mara uchumi.Hafanyi utafiti anakidhalilisha Chama.Juzi Serikali imefafanua kwa hoja mambo hayo yeye anaropokaropoka tu na kutupa wakati mgumu kujibu hoja.Kwa sasa hatujui maoni yake binafsi na yale ya Chama ni yapi.

4.Ameonesha udhaifu mkubwa kuungana na Ukawa kususia uchaguzi wa marudio.Kiongozi Zito sio mtu wa kuaminika tena ni mnafiki...imetuuma sana wanachama. Leo anaungana na Ukawa watu aliopata kuliambia Taifa kuwa ni "walaghai wakubwa?"

5.Ametulaghai wafuasi wake na wanaomfadhili nje ya nchi kuwa eti Demokrasia inabanwa.Naanza kuamini kuna.mambo yake binafsi yamebanwa.Hii ilikuwa fursa ya chama kwenda kwa wananchi na kufanya siasa unaikataaje.Tunaikimbiaje kwa hoja dhaifu hivi?

6. Leo anajifanya kuguswa na maslahi ya wafanyakazi wakati Chamani kwake kunawaburuta watendaji wake...wako hoi na haki zao zinabanangwa.Niko hapa watendaji wako hoi na hakuna hata mawasiliano na makao maku
Amepotosha mambo gani? Mbona hata huyataji tukakuelewa vizuri. Halafu, unataka tukuamini wewe ambaye hujui hata kujieleza?
 
Wewe sio mpinzani kwa sababu kuu mbili

Unamshangaa zitto kulalamikia demokrasia inayokufa nchini kwamba unadai ni fursa ya chama kushuka kwa wananchi?? Ssa siasa zimepigwa marufuku nje ya ubunge utashukaje kwa wananchi wa mbagala ilihali hamna diwani wala mbunge au nyandekwa ambako hamna hta mwenyekiti wa mtaa???

2. Unamshangaa zito kususia uchaguzi je ulitaka ashiriki ili ahalalishe uharamia wa CCM?? Je ina maana malalamiko ya chaguzi kutokuwa huru huyaamini?? Kma huyaamini ww sio mpinzani maana haiwezekani rafu zote zile zinachezwa kwenye udiwani ww unashabikia leo washiriki uchaguzi.....huyo mgombea wenu hta kma ni msomi mna uhakika akishinda atatangazwa???

3. Unashangaa zitto kujiunga na UKAWA kususa uchaguzi eti kisa aliwaita walaghai na wachumia tumbo. Hivi hao CUF hawakuwahi kuwaita chadema chama cha makafiri na chadema hawakuwahi ita cuf chama cha mashoga n.k mbona waliungana why not ACT?? Masuala yenye maslahi ya kitaifa ni lazima muungane at any cost kma zitto ameona demokrasia inakufa asiungane na wanaukawa wanaopinga demokrasia kufa kisa tu aliwaita walaghai???

Kma ww ni mwanaACT na unatoa hoja hizi basi chama chenu kitakufa siku si nyingi
 
Ametulaghai wafuasi wake na wanaomfadhili nje ya nchi kuwa eti Demokrasia inabanwa.

Nina wasiwasi sana na ufadhili wa huyo bwana
Cc: Financial Intelligence Unit, TRA, BOT, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na nk.
 
Naanza kuamini kuna.mambo yake binafsi yamebanwa.
Mipesa na zawadi kedekede alizokuwa akipokea pindi akiwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu ya mashirika ya umma imeminywa na Magu 'uongozi wa awamu ya tano'
 
Nina wasiwasi sana na ufadhili wa huyo bwana
Cc: Financial Intelligence Unit, TRA, BOT, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na nk.
Kwanini usiwaambie hao TAKUKURU wachunguze nani mwenye richmond?? Kwanni wasichunguze aliyebeba masandarusi ya mabilion pale stanbic ??wasichunguze mmiliki wa simba trust?? Kwanni wasichunguze ufisadi wa kutisha bandarini??? Anyway wale waliotajwa kwenye kamati ya madini watakamatwa lini
 
Wewe sio mpinzani kwa sababu kuu mbili

Unamshangaa zitto kulalamikia demokrasia inayokufa nchini kwamba unadai ni fursa ya chama kushuka kwa wananchi?? Ssa siasa zimepigwa marufuku nje ya ubunge utashukaje kwa wananchi wa mbagala ilihali hamna diwani wala mbunge au nyandekwa ambako hamna hta mwenyekiti wa mtaa???

2. Unamshangaa zito kususia uchaguzi je ulitaka ashiriki ili ahalalishe uharamia wa CCM?? Je ina maana malalamiko ya chaguzi kutokuwa huru huyaamini?? Kma huyaamini ww sio mpinzani maana haiwezekani rafu zote zile zinachezwa kwenye udiwani ww unashabikia leo washiriki uchaguzi.....huyo mgombea wenu hta kma ni msomi mna uhakika akishinda atatangazwa???

3. Unashangaa zitto kujiunga na UKAWA kususa uchaguzi eti kisa aliwaita walaghai na wachumia tumbo. Hivi hao CUF hawakuwahi kuwaita chadema chama cha makafiri na chadema hawakuwahi ita cuf chama cha mashoga n.k mbona waliungana why not ACT?? Masuala yenye maslahi ya kitaifa ni lazima muungane at any cost kma zitto ameona demokrasia inakufa asiungane na wanaukawa wanaopinga demokrasia kufa kisa tu aliwaita walaghai???

Kma ww ni mwanaACT na unatoa hoja hizi basi chama chenu kitakufa siku si nyingi

Hivi upinzani na vinasaba? Kwamba MTU yeye ni mpinzani kwa kuwa amezaliwa mpinzani hivyo kazi yake kupinga tu?

Upinzani ni permanent?
 
Mtu anayeamini kwamba;

1. Zitto
2. Lipumba
3. Maalim
4. Mbatia
5.
6.
Ni watu wa upinzani anahitaji kumuonea huruma.
 
Tarishi: Hongera kwa kujiuza. Chama cha Manunuzi wamekusikia. Leo halitatua jua kabla hawajaja. Unataka uchaguzi gani wewe nawe? Eti serikali imefafanua kwa hoja mambo ya uchumi. Hoja gani hizo ndugu yetu? Njaa inakusumbua, lakini hongera zako maana biashara inayolipa kwa sasa ni kuwa mpinzani unayeipenda CCM, utalipwa kiasi chochote utakacho. Kafie mbali wewe kibaraka. Eti ulitaka ukajitangaze kwa wanachama, kwani kama mnaruhusiwa kufanya siasa si ungeenda kujitangaza mapema? Au ulitaka hiyo fursa ili uuze kura? Au ulitaka uwe wakala ili wakakununue upate fedha ya kusogeza maisha? Lazima hapo kwa jinsi ulivyolalamika kuna maslahi binafsi yameingiliwa na msimamo wa Zitto na chama chake.
 
Hivi upinzani na vinasaba? Kwamba MTU yeye ni mpinzani kwa kuwa amezaliwa mpinzani hivyo kazi yake kupinga tu?

Upinzani ni permanent?
Sio VINASABA ila ni mentality/Fikra ambayo unaiishi mpaka mabadiliko uliotaka yanakuja sasa huwezi ukawa mpinzani unaona mfumo wa uchaguzi ni mbovu alafu unamshangaa kiongozi wako wa chama akisusia uchaguzi kwa fikra hizo ww sio opposition
 
Opposition ni fikra, fikra za kususia uchaguzi, fikra za kushiriki uchaguzi, zote hizo ni fikra, wote hao ni wapinzani maana wanataka mabadiliko..

Fikra za upinzani wa fulani anapitaka jambo fulani ndio sahihi na upinzani wa mwingine sio sahihi.

Wakati wapinzani wakitoka bungeni yeye alibaki, Leo eti ni mpinzanii, kesho unaweza usiwe mpinzani japo Leo ni mpinzani bila kujali kama mabadiliko yametokea au la.

Bora unyimwe mali lakini sio akili
 
Act karibia inakua chama cha upinzani, baada ya kina mkumbo na wenzie kununuliwa naona kuna wapuuzi wachache waliobaki wamepewa task ya kupambana wakiwa ndani.
 
Back
Top Bottom