Unless kama hauna kumbukumbu lakini hata huko nyuma, wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu si tu kwamba kunakuwaga na additional recruitment of police bali pia vitendea kazi. Na hilo la kuondoka physically, si tatizo la Tanzania tu, mambo kama hayo yanatokea sana duniani!
But, pamoja na yote hayo ndugu yangu, let's be honest here--- ni mara ngapi JK ametuhumiwa kutaka kumweka mrithi atakayelinda maslahi yake? Kwa bahati mbaya au mzuri; wote wale ambao tulisema JK anawandaa ili waje kumfichia madhambi yake hakuna hata mmoja ambae alifika angalau Halmashauri Kuu! Sitaki kuamini kwamba unaamini JK hakufahamu kwamba mwisho wa Membe ungekuwa Kamati Kuu! Huyu Membe ndio alisemwa sana kwamba ndio ngao ya JK! Sitaki kuamini kwamba unaamini JK alitarajia Asha-rose Migiro angeweza kufurukuta; lakini huyu Migiro ni mmoja wa watu tuliokuwa tunamtuhumu JK kwamba anamwandaa! Sitaki kuamini kwamba unaamini JK hakuhusika kukatwa kwa Lowassa lakini hata alipochaguliwa Jaji Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume, watu tukasema JK anamwandalia EL njia kwa kuwa tu EL na Lubuva ni mashemeji!
Sasa ikiwa hata kuteuliwa kwa mtu ambae hatukuwahi kusema kwamba atawekwa kumlinda JK; bado leo tunasema mteuliwa Magufuri yupo pale kumlinda JK, sasa ni nani basi angesimama kwa tiketi ya CCM ambae tusingesema kwamba
yupo pale kulinda maslahi ya JK?
Hebu turudi nyuma kabla ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM! Hivi wewe ungekuwa ndie JK-- ni wapi ungejisikia kuwa more safe kati ya kumwachia Magufuri kijiti au kumwachia kijiti Lowassa? Lowassa yule wa kabla ya kukatwa-- Lowassa yule ambae hakukutana na JK barabaran-- Lowassa yule aliyedai ikiwa kimbukumbu zitawekwa sawa, hakuna President aliyemfikia JK kuifanyia hii nchi mambo makubwa!!!