Paul Kagame: An African role model?

Kagame for Times 100 nomination
The president of the Republic of Rwanda, Paul Kagame, has been nominated for TIME Magazine’s 100 Most Influential People of the Year which I think is an accolade he deserves.
Post-colonial Rwanda was characterised by the worst leadership which lacked both the vision and ambition to stir the country to achieve at least modest development.
The classification of citizens made sure that some went to schools, involved in leadership of their country and it gave them a right to be called Rwandans while others languished in poverty, ignorance and they were not humans but cockroaches that needed to be killed.
With the RPF led by President Kagame winning the struggle in 1994 and restoring sanity, he embarked on reconstruction and reconciliation of a country that had been polarized by genocide.
15 years on, Rwanda has not only won respect around the world, but the name Kagame has become synonymous with democracy, development, human rights and most importantly, a man loved by the people who had lost hope in themselves.
Ranked 24th, Kagame is the highest ranked African beating global figures such as Russian premier Vladimir Putin (35th).
The World Bank and UN indices released every year will confirm that the man has taken giant strides to make his country a better place where investors throw their money and a place where his countrymen live in harmony and happiness.

Paul Kagame - The 2009 TIME 100 Finalists - TIME
 
MJADALA kuhusu ziara nyingi za nje za Rais Kikwete; hususan za Marekani na Ulaya, umekataa kufa. Mjadala huu unasinzia tu kwa muda; lakini huibuka upya pindi anapofanya safari nyingine ya nje. Na ndivyo ilivyokuwa hivi karibuni alipokwenda tena Marekani (mara ya sita au saba?).
Wananchi wamekuwa wakizijadili safari hizo majumbani, maofisini, vijiweni, kwenye baa, na hata kwenye intaneti. Wako wanaoziunga mkono na wako wanaoziona kuwa ni matumizi mabaya ya pesa za walipakodi.
Katika moja ya hotuba zake Rais Kikwete alipata kujitetea kuhusu safari hizo kwa kutoa mfano wa Soko la Mitaji la Nasdaq alilolitembelea New york, Marekani.
Rais alisema hivi: “Nilipotembelea Soko la Hisa la New York, ambalo biashara yake inazidi dola 22.8 trilioni za Marekani, tulipewa heshima ya kuzindua biashara ya siku ile. Ni kwa sababu nilikuwepo ndiyo maana tulipewa heshima hiyo. Hivi unadhani Jonathan Njau (Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam –DSE), angeweza kukutana na jamaa wale angekuwa peke yake?”
Kauli hiyo ya Rais wala haielezi Tanzania ilinufaika vipi kwa yeye kutembelea soko hilo la mitaji la Nasdaq; ukiachilia mbali kwamba alipewa heshima hiyo ya kufungua rasmi biashara ya siku hiyo.
Kwa hakika, mtu unashindwa kujizuia kujiuliza: Hivi Rais wetu alikatisha bahari ya Atlantic hadi Marekani kwa ajili ya kulitembelea soko la hisa la Nasdaq? Hivi alitaka kujifunza kitu gani hasa kutoka katika soko hilo la hisa linaloongoza duniani ambacho asingeweza kujifunza kutoka katika masoko yaliyoendelea ya mitaji ya baadhi ya nchi za Afrika.
Ni nani asiyejua kwamba tofauti kati ya soko letu changa la hisa la Dar es Salaam (DSE) na lile la Nasdaq la New York, ni tofauti kati ya Mlima na kichuguu?
Kama Rais na ujumbe wake walitaka kujifunza masuala ya masoko ya hisa ili labda waje waisaidie DSE, basi hawakuwa na sababu ya kuvuka bahari ya Atlantic kwa hilo! Kenya tu hapo kuna Soko la Mitaji la Nairobi ambalo ni bora mara 20 kuliko DSE yetu! Na kama hilo la Nairobi haliwavutii, basi kuna jingine la Johannesburg, Afrika Kusini ambalo nalo ni bora mara 30 kuliko la kwetu!
Ninachojaribu kueleza hapa (kwa mfano huo) ni kwamba wakati mwingine watawala wetu hawana sababu yoyote ya kukatisha bahari ya Atlantic kwenda kujifunza Marekani; kwani, kwa baadhi ya mambo, mafunzo yako hapa hapa Afrika; tena wakati mwingine katika nchi jirani tu!
Ndiyo maana siziungi mkono baadhi ya ziara anazozifanya rais wetu. Ningeziunga mkono safari hizo kama zingekuwa ni za kutafuta kweli kweli ‘mwarobaini’ wa kutukwamua ki-maendeleo, na si za kufungua biashara ya siku ya Nasdaq au za kutembeza kwingineko bakuli la ombaomba!

Ningeziunga mkono kama zingekuwa ni za kututafutia teknolojia ya kutengeneza boti na nyavu za uvuvi, na si za kutuombea samaki! Ningeziunga mkono kama zingekuwa za kuwaombea Watanzania wafundishwe namna ya kutengeneza vyandarua (kama hawajui), na si za kuomba msaada wa vyandarua!
Kwa maneno mengine; ningeziunga mkono kama zingelenga kutuletea maendeleo endelevu, na si za kuomba kusaidiwa kutatuliwa shida za muda mfupi za hapa na pale.
Kwa mantiki hiyo hiyo, ningekuwa naziunga mkono kama zingekuwa ni za kwenda katika nchi kama za India, Brazil, Singapore, Malaysia, Korea Kusini, na hata nchi chache za Afrika, kudadisi na kujua ni kwa nini wenzetu walifanikiwa kupata maendeleo katika kipindi kifupi wakati sisi tumekwama.
Miaka si mingi sana iliyopita, nchi hizo zilikuwa hazitofautiani sana nasi ki-maendeleo; lakini zilipozinduka, zilipiga kasi ya maendeleo haraka na kutuacha mno nyuma. Zilikuwa dunia ya tatu kama sisi, lakini sasa zinabisha hodi dunia ya kwanza; huku zikituacha sisi pale pale!
Nchi kama Malaysia na Korea Kusini tulikuwa kiwango kimoja cha maendeleo mwaka 1961, lakini sasa ni tajiri kutuzidi mara 20 (msome Robert Guest katika kitabu chake The Shackled Continent).
Lakini hata Afrika, kuna baadhi ya nchi ambazo tunaweza kabisa kujifunza kitu. Moja ya hizo ni Rwanda. Miaka 13 iliyopita Rwanda ilianza upya (majivuni) baada ya kuharibiwa vibaya na vita na mauaji yale ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyosababisha vifo vya Watusi na Wahutu wenye msimamo wa kati, zaidi ya 800,000.
Lakini leo hii, Rwanda iko mbali mno kimaendeleo (hasa vijijini) kutuzidi. Alichoweza Rais Kagame kukifanya Rwanda katika miaka 13, ni kile ambacho sisi, kama Taifa, tumeshindwa kukifanya kwa miaka 20 iliyopita. Na wala hatujasikia Rais Kagame akienda, mara kwa mara, Marekani au Ulaya!
Mwaka 2004 nilikuwa mmoja wa wahariri wachache wa Tanzania tulioalikwa na Serikali ya Rwanda kwenda huko kujionea maendeleo yaliyofikiwa baada ya miaka 10 ya yale mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Tukiwa huko, tulipata fursa ya kuzungumza na wananchi wa kawaida mijini na vijijnini. Tulizungumza pia na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, mameneja, wahandisi, wahadhiri nk. Na si mazungumzo tu; bali tulitembelea miji na vijiji kadhaa na kushuhudia, kwa macho yetu, jinsi nchi hiyo inavyosonga mbele kwa kasi kimaendeleo.
Nikiri kwamba, kwa nilichokiona Rwanda (mijini na vijijini), ilikuwa vigumu kwangu kuamini kwamba miaka 10 iliyopita nchi hiyo iligubikwa na vita na umwagaji damu mkubwa!
Ni vipi Rwanda katika kipindi cha miaka 13 tu iliyopita imeweza kunyanyuka toka majivuni na kujipatia maendeleo hayo ya kasi? Siri yao ya maendeleo ya haraka ni nini?
Nadhani hicho ndicho kitu ambacho Rais Kikwete na wenzake wanapaswa kwenda Rwanda kujifunza, na si kukimbilia tu Marekani; ingawa naambiwa kwamba maofisa wake hawazipapatikii safari kama hizo za Rwanda; kwa vile hazina malipo makubwa ya posho kama za Marekani!
Kwa ufupi, Rwanda ni somo kubwa kwetu. Miaka michache tu iliyopita iliharibiwa vibaya na vita na mauaji yale ya kimbari ya mwaka 1994, lakini sasa inachanja mbuga kimaendeleo kutuzidi sisi ambao miaka yote tumekuwa “kisiwa cha amani”.
Nilijifunza katika ziara hiyo kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala wetu na viongozi wa Rwanda. Wa kwao ni wazalendo kweli kweli kushinda wa kwetu. Akili na mioyo yao vyote huzama kwenye kuijenga nchi yao ya Rwanda.
Katika Rwanda kiwango cha rushwa (ufisadi) ni kidogo mno. Kiongozi fisadi anachukuliwa kama ni msaliti wa umma na hivyo adui wa umma; wakati hapa kwetu kiongozi fisadi akirejea jimboni hupokewa kwa maandamano ya magari na pikipiki!
Baraza la mawaziri la Rwanda limejaa vijana wasomi na wachapakazi kweli kweli wanaoipenda nchi yao. Kagame aliwafuata vijana hao sehemu mbalimbali duniani na kuwashawishi waache, ama biashara zao au ajira nono walizokuwanazo, na kurejea nyumbani kuijenga upya nchi yao.
Uchapakazi wa baraza la mawaziri la Rwanda unaanzia kwa Rais Kagame mwenyewe. Huyu ni rais ambaye huchapa kazi hadi usiku. Nakumbuka tulipokuwa Kigali mwaka 2004 tulifanikiwa kukutana naye kwa mahojiano saa 6 usiku! Na bado baada ya sisi alikuwa na mkutano na wasaidizi wake wengine!
Tulipoonyesha kushangaa kukutana na Rais Kagame saa 6 usiku, wenyeji wetu walitushangaa kwa kulishangaa hilo. Wakatwambia kwamba Kagame aliwahi kuamka saa 9 usiku na kwenda uwanja wa ndege kuipokea timu ya soka ya taifa ambayo ilikuwa inarejea nyumbani na ushindi mkubwa!
Hapa kwetu Tanzania sijapata kusikia habari za waziri yeyote, au kiongozi yeyote mwenye kawaida ya kuchapa kazi hadi saa 6 usiku. Kama yupo nitajieni. Kiongozi wa mwisho tuliyekuwanaye, aliyekuwa na tabia hiyo, ni Edward Sokoine. Huyo alikuwa na kawaida ya kusoma mafaili usiku na kuwapigia simu (hata saa 8 usiku) mawaziri, ma-RC au hata ma-DC; kuwauliza hili na lile!
Kwa hiyo, kwa uchapaji kazi wa Kagame haishangazi kuona kuwa kwa muda mfupi tu amefanikiwa kuugeuza mji wa Kigali kuwa kitovu kikubwa cha biashara; achilia mbali kufufua kwa kasi ya ajabu kilimo cha biashara cha mazao ya kahawa na chai ambacho kilikuwa kimekufa kabisa wakati wa vita na mauaji yale ya kimbari.
Hata mkakati wake wa kupambana na umasikini vijijini ni wa matendo zaidi kuliko blah blah. Mpango kama ule wa kutoa ng’ombe wanne kwa kila mwanakijiji, umewanyanyua wengi nchini Rwanda.
Rwanda wana visheni wanayoifukuzia kimatendo na si ya kwenye makaratasi tu kama visioni 2025 yetu. Kwa mfano, wameshaanza kutekeleza kidogo kidogo Mpango Mkuu wa Ujenzi wa Kigali Mpya ambayo ni visheni ya miaka 50. Hapa kwetu sidhani kama tuna hata mpango mkuu (master plan) wa Dar es salaam itakavyokuwa miaka 20 ijayo; achilia mbali miaka 50!
Kilichoniuma moyo wakati wa ziara hiyo, hata hivyo, ni kwamba baadhi ya walioiwezesha Rwanda kupata maendeleo hayo ya haraka ni Watanzania. Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Kigali cha Sayansi na Teknolojia (KIST) ambacho kimechangia sana kusukuma maendeleo katika vijiji vya Rwanda, nguvu yake kubwa ya mwanzo ilikuwa ni Watanzania.
Si tu kwamba mkuu wa chuo mwanzilishi, Profesa Silas Rwekabamba ni Mtanzania aliyechukuliwa na Kagame kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, lakini pia idara kadhaa za KIST zilikuwa zinaongozwa na Watanzania wakati nilipokitembelea mwaka 2004.
KIST ndiyo chachu ya maendeleo ya Rwanda; hususan vijijini. Kama utakwenda vijijini na kukuta wananchi wanatumia nishati ya jua, ni kwa sababu ya KIST, kama utakuta madaraja mapya yamejengwa vijijini, ni kwa sababu ya KIST; vivyo hivyo kwa zana za kilimo na viwanda vidogo vidogo.
Natujiulize: Kwa nini Watanzania hao (kina Rwekabamba) walipokuwa kitivo cha uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), hawakukifanya kitivo hicho kuwa chachu ya maendeleo ya vijiji vyetu kama walivyoifanya KIST kwa Rwanda?
Jibu lake ni rahisi; nalo ni kwamba mazingira ya Tanzania si mazingira ya Rwanda. Nchini Rwanda si tu walilipwa vyema, lakini vipaji vyao vilithaminiwa na kutumiwa vyema. Aidha, viongozi wa Rwanda wako nao bega kwa bega katika jukumu kubwa la kuhakikisha sayansi na teknolojia inasambaa hadi vijijini, tofauti na hapa nyumbani.
Ukiachilia mbali kina Profesa Rwekabamba, hata baadhi ya mawaziri wa Rwanda wamepata elimu yao ya msingi na sekondari hapa Tanzania. Nazungumzia watu kama Donald Kaberuka ambaye alikuwa Waziri wa Fedha wa Kagame kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
Hata sasa ambapo ni bosi mkuu wa ADB, bado mapenzi, akili na mawazo ya Kaberuka yameelekezwa kwa nchi yake ya Rwanda; na hiyo inaeleza ni kwa nini Rwanda inafaidika sana na misaada ya benki hiyo.
Natujiulize: ni Watanzania wangapi wenye nyadhifa kubwa nje (kina Migiro na kina Profesa Tibaijuka) ambao wameikumbuka nchi yao na kuisaidia kuipa miradi mikubwa; kwa namna ambayo kina Kaberuka wanaisaidia Rwanda? Mimi siwajui, kama wapo naomba nitajiwe.
Nihitimishe hoja yangu kwa kusisitiza tena kwamba si mara zote ziara za watawala wetu nchini Marekani na Ulaya zina kitu kipya cha kujifunza kinachoweza kutuletea maendeleo endelevu. Sana sana nyingi zinakuwa tu za kutembeza bakuli la omba omba; yaani kutafuta msaada wa pesa wa kutatua matatizo yetu ya muda mfupi ya hapa na pale.
Nionavyo, badala ya kukimbilia tu Marekani na Ulaya, ni vyema watawala wetu waende kujifunza katika zile nchi ambazo miaka michache tu iliyopita tulikuwanazo dunia ya tatu, na sasa zinabisha hodi dunia ya kwanza!
Lakini pia kuna nchi jirani kama Rwanda ambazo katika muda mfupi tu zimejipatia maendeleo makubwa kutuzidi. Kwa nini Rais wetu Kikwete asiende huko kuijua siri yao?
Simaanishi ziara ya siku moja kwenda mkutanoni au kuzungumza tu na Kagame. Naamanisha ziara ya karibu wiki nzima ya kutembelea vijiji na miji mbalimbali ya nchi hiyo na kujionea mwenyewe kasi yao ya maendeleo, na kisha kurejea Kigali kumsihi Kagame na wenzake wammegee ‘siri’ ya mafanikio yao ya haraka!

Najua kuna watakaosema kwamba Kagame ni dikteta. Ni kweli, lakini ni ‘dikteta karimu’ (benevolent dictator). Hata Nyerere walimwita dikteta, lakini ni nani aliyewafanyia Watanzania mema mengi kati ya Nyerere na marais waliomfuatia? Tafakari.
 
DAH, WE ACHA kAGAME NI KICHWA BWANA!

Najua kuna wengi watakuja na post za kupinga hoja yako, lakini ukweli unabaki palepale kwamba Kagame ni mfano wa kuigwa na marais wooote wa Afrika. A meweza kufanya mambo makubwa ktk kipindi kidogo tu. Kuna jamaa walikuwa wanafanya kipindi kinaitwa LONG WAY DOWN(National Geographic Channel) walipitia pale ikulu ya Kagame, duh nao walikubali.

Ushauri wa Bure; Mpendwa Rais wetu Kikwete.. Kimbia hapo Rwanda ukajifunze mengi, acha habari za kukimbia unaenda huko marekani, au kukimbizana na wajinga akina zeutamu.... kimbia hapo Rwanda tu ukajifunze jinsi ya kuendesha nchi! Then ukitoka huko wanyanganye mawaziri wote na makatibu wakuu hayo mavx wanayotanulia njiani... mbona wa rwanda walipokonywa na mambo yanaenda shega? Jamani hata kuangalizia huweziiiiiiiiiiii?
 
Waliosoma na JK wanadai jamaa ni Kilaza sana, Mgumu kuelewa na mwepesi kusahau...kumpeleka kujifunza kitu ni kupoteza resource zetu! Mwacheni alivyo he is at his best...
 
@Juakali ulichosema ni kweli tupu mpaka tutakapokuwa na roho ya uzalendo nakujiuliza kila mmoja wetu je mimi nimeifanyia nini nchi yangu ndipo tutakapofanya mapinduzi ya kiuchumi,
Roho inaniuma sana ninapoona nchi hii ilivyojaliwa kuwa na rasilimali, nyingi na zinanufaisha wageni ambao sio wazawa,magabachori na waarabu wamepatiwa mianya yote ya unafuu wakupata mikopo mikubwa mikubwa kwenye mabenki na kwa maana hiyo kuwa na fursa kubwa ya kuendelea
Vipi ni lini viongozi wetu tunaowachagua ka imani kubwa watarejesha heshima japo kidogo kwetu.
Bado mimi nasema sio lazima tukaangalie Rwanda pamoja na lawama zinazoelekezwa kwa Mkapa lakini katika kipindi cha miaka kumi alifanya mabadiliko makubwa pamoja na kudhibidi mfumuko wa bei
Naomba nifahamishwe kwa ujumla mimi naona katika utawala huu mambo yameenda mrama kabisa,hii serikali ingefuata mambo ambayo yalikuwa kwenye ilani yao ya uchaguzi wa mwaka 2005 tungefika mbali.
Sasa hivi pia namuoana hata waziri mkuu kama hasaidii sana naona kama kweli anazunguka mikoani kote kuangalia maendeleo lakini naona ni kisiasa zaidi mbona hakuna hatua zinachukuliwa,

Angalia Jiji la Dar es Salaam lilivyo chafu,uchafu,uchafu tuu kila mahala hakuna bustani hakuna mandhari yeyote nzuri utakayojivunia,maeneo ambayo wangeweza kutengeneza ikawa bustani ya jiji kama pale jangwani au pale walipokuwa wananchi walikuwa wanachimba kokota(Kunduchi) pameachwa panavamiwa watu wanaendelea na ujenzi na hakuna aneyekemea,hakuna hata vyelezo kwenye barabara ,(pervement)hata tungeweka za mawe basi Jiji likawa na sure nzuri kidogo kila mahala matope,
Hakuna mpango mkakati wa kutengeneza mifereji mikubwa ya kutoa maji na elimu ya mzaindira kuwahasisha wanachi kueshimu vitu vya kijamii ikiwemo mifereji barabara shule na hospitalki wala sheria ndogondogo hazifuatwi kwa kweli nadhani utawala huu umeshindwa kabisa kutuweka kwenye mwelekeo wa maendeleo
Dharau za kudharau wataalamu wetu umezidi na hauna kikoma lakini nchi za kusini mwa Afrika na mashariki wananufaika na wataalamu wetu we ngoja sisi tukalaghe baho,hawapewi fedha za utafiti wala mipango hawahusishwi wala kitu chochote huu ni umbumbumbu usio na kikomo
je jibu lake nini ni maopinduzi ya kifikra kuweza kuwang'oa hawa waonadhani nchi ni ya mama yao wanaweza kufanya chochote wakati wowote.
 
Waliosoma na JK wanadai jamaa ni Kilaza sana, Mgumu kuelewa na mwepesi kusahau...kumpeleka kujifunza kitu ni kupoteza resource zetu! Mwacheni alivyo he is at his best...

Masa, I think you have hit the nail on the head. Nilizipata hizi habari wakati wa kampeni 2005 na niliwabishia sana jamaa lakini sasa ninajitahidi kwa gharama zote kuwakwepa kwani walichosema ndicho tunachoshuhudia wote live bila chenga. Maskini watz pole yetu. Anyway labda next time we will think twice na kutofautisha umiss/mr tz na urais.
 
JK hafundishiki. Tulikosea kumpa kiti wacha tuvune tu tulichopanda. Japo mm sikumpa kura yangu na hataipata hata anipe nini. Msinilaumu, sikumchagua.
 
nawaunga mkono wote hapo juu na lingine nadhani viongozi wetu hawana mapenzi na nchi yetu,hawajali na sio viongozi kwa kipaji ni watu waliotaka uongozi kwa maslahi yao binafsi.ni tofauti mtu anapotaka kuwa kiongozi kwa uchungu wa maendeleo na yule mtu anaye taka uongozi kwa vile kaona ni ulaji kuwa kiongozi.na hawa viongozi wa kuona ulaji ndio tuliokuwa nao tanzania.
 
Wamepigania kuingia Ikulu ajili ya kikundi chao cha watu wachache si kwa ajili ya uzalendo na mapenzi ya nchi yao kunyanyua wanyonge hapana tena hapana kabisa.....JK anakamilisha ratiba na muda tu maana hana jipya ,hajawahi kuwa na jipya...na hana vision.....wala mission.
 
-June 9 2009 Kagame opens a laptop per child leaning centre at KIST(reach out center for whole of Africa).Kigali has already placed order for 100.000 laptop (@ $ 200 each) to ease teaching and studying.

This the type of leadership that we desire and make as(we in the region) proud.
 
Kagame yuko smart and serious sana na anauchungu sana na Rwanda. Sasa ukija kwa Kikwete ni vice versa, kwa hiyo hata akienda hataweza kujifunza kitu. Watanzania tuendelee kukaa kimya wakati Presidaa wetu akisafiri kwenda Marekani na Ulaya kwa sababu anaenda kupitisha bakuli la kuomba misaada, sasa Rwanda atarudi na nini???

Sisi Wandanganyika tutaendelea kupiga kelele kwenye vijiwe vya kahawa na kwenye stuli ndefu (Grocery/Bar) bila hata ya kuchukua action yoyote ile juu ya mustakabali mzima wa nchi yetu, Embu tuamke kutoka usingizini. Ni zaidi ya miaka 40 tangu uhuru mpaka leo Tanzania bado inazidi kuwa maskini. Uchanguzi mkuu hauko mbali ni 2010, sasa tujitahidi hata kuchagua viongozi watakao kuwa serious na nchi yetu na sio kusafiri safiri bila ya sababu.
 
Kagame yuko smart and serious sana na anauchungu sana na Rwanda. Sasa ukija kwa Kikwete ni vice versa, kwa hiyo hata akienda hataweza kujifunza kitu. Watanzania tuendelee kukaa kimya wakati Presidaa wetu akisafiri kwenda Marekani na Ulaya kwa sababu anaenda kupitisha bakuli la kuomba misaada, sasa Rwanda atarudi na nini???

Sisi Wandanganyika tutaendelea kupiga kelele kwenye vijiwe vya kahawa na kwenye stuli ndefu (Grocery/Bar) bila hata ya kuchukua action yoyote ile juu ya mustakabali mzima wa nchi yetu, Embu tuamke kutoka usingizini. Ni zaidi ya miaka 40 tangu uhuru mpaka leo Tanzania bado inazidi kuwa maskini. Uchanguzi mkuu hauko mbali ni 2010, sasa tujitahidi hata kuchagua viongozi watakao kuwa serious na nchi yetu na sio kusafiri safiri bila ya sababu.
muheshimiwa na kuunga mkono kwa asilimia 100.
 
Nakosa cha kusema! make mkuu data ulizota zinaonesha ni jinsi gani una uchungu na maisha ya walala hoi wa nchi hii in real sense we need people like you! sio kwamba nakupaka kilemba cha ukoka ila ukweli ni kweli umenikuna nikiwa kama mzarendo na mtu ninayependa maendeleo ya nchi yangu na kuchukia ubabaishaji wa viongozi wetu hasa hasa hawa wa awamu ya nne! Kama WATANZANIA wangekuwa na akili na mtazamo kama wangu, NATHANI MWAKA 2010 TUSINGEWAPA RIDHAA YA KUINGIA IKULU NA KUENDESHA SERIKALI KATIKA MWELEKEO WALIO NAO SASA! MAWAZO YANGU LAKINI! Nasema hivyo kwa sababu hawana uchungu na watu wanaowaongoza! wala rasilimali za nchi, wamegeuza rasilimali zetu kuwa shamba la bibi, kila mtu anachukua wakiwamo wenyewe kwa kasumba ya kulindana! kifupi hawa jamaa na serikali yao ni wasaka TONGE! wito wangu kwa wanajf "2cwape kula!"
 
Wakuu hii kitu nimeona nifanze ile wenyewe munasema copy and paste.
Ila nimeipenda kweli hii kama iko in reality.
why not in TZ?

By Andrew M. Mwenda

Last week I was in Kigali , this time at the heels of a cabinet decision to
impound all luxurious four wheel drive vehicles bought at government
expense and driven by ministers, security and military chiefs, foreign
experts and their local handlers. In a morning crackdown, all the big men
and women of this republic woke up to find that police constables along the
main roads were stopping and taking away their vehicles and leaving them to
walk to office.
The international donor community, known all over Africa for its corrupt
and profligate life styles which they indulge in the name of fighting
poverty, was this time caught with their pants down. They claim to fight
poverty while riding in luxurious four-wheel drive vehicles, sitting in
opulently furnished offices, earning obscene salaries and living in
executive mansions. In a bold act of defiance, Rwanda impounded even those
vehicles belonging to donor projects. After cleaning his own government of
corruption, he has now taken on the profligacy of the international aid
industry and its experts are now scared.

In a discussion with President Paul Kagame, he told me that he had looked
at some of the "poverty reduction" projects and they smelt bad. "There are
projects here worth only $5m and when I looked at their expenses, I found
that $1m was going into buying these cars, each one of them at $70,000.
Another $1m goes to buy office furniture, more $1m for meetings and
entertainment, and yet another $1m as salaries for technical experts,
leaving only $1m for the actual expenditure on a poverty reducing activity.
Is this the way to fight poverty?" he asked as I shifted with glee in my
chair.

Already, the government is auctioning these vehicles and so far has gotten
over $3m from the sales. Mr Kagame has now issued a new directive, saying
government should not purchase cars for its officials with more than 2,500
cc. But there is more: the government has placed a ceiling on mobile
telephone expenses for all its ministers, military and security chiefs to
50,000 Rwanda Francs (Shs150, 000), and also ordered MTN Rwanda to cut off
their international roaming access.

The directive also stops the holding of workshops, seminars and conferences
on poverty reduction in posh hotels like the Intercontinental, Mille
Collins etc, insisting they should be in government owned buildings at no
cost. The order also requires all government ministries; departments and
agencies to move from privately owned buildings where they pay high rents
to government owned buildings.

I told Kagame that whereas some of the most highly skilled Africans are
going to Europe and North America to clean streets and toilets, our
development partners send us Œtechnical experts on these projects at
individual monthly salaries of between $10,000 and $20,000, a salary that
could pay 12 Africans of better training and experience and save this
continent from severe brain drain. In fact, most of these so-called experts
are a miserable, career-stranded lot in their own countries, but are dumped
in Africa and other poor countries through foreign aid protocols.

Donors never shy from lecturing our governments on fiscal frugality, yet
their aid driven projects are the most profligate. Of total project aid to
Uganda 's ministry of Health, 93 percent of it goes into technical
assistance (i.e. salaries and allowances for the experts) and overheads
(i.e. four wheel drive vehicles, opulent office furniture, computers,
stationary, tea and cakes).

Only a miserable 7 percent of this aid goes into purchase of drugs. Now you
understand why, in spite of a huge health budget, our people cannot find
drugs in hospitals. We in the media have been shouting ourselves hoarse
against government corruption. It is time to expose the worse forms of
profligacy, which forces our governments to pile up huge sums in debt.

In fact, of the total money from the Uganda government budget to the
ministry of Health, 98 percent reaches its intended beneficiaries, clearly
showing that in spite of its corrupt ways, the government of Uganda is a
better evil than donors. Of total project aid to Uganda , 68 percent goes
into overheads and technical assistance. Only 32 percent to its intended
beneficiaries.

A few weeks ago I presented the above facts to President Yoweri Museveni
and asked him to act. My heart bleeds to say he is so deeply discredited by
his inability to tackle corruption in his government, and his own
profligate public administration expenditure that he lacks moral authority
to take on donors.

The other reason is that his regime lives off this coalition of mutual
deceit with donors that both are fighting to eradicate poverty in Uganda .
Kagame, however, is able to act boldly because he occupies a moral high
ground in fighting corruption, has ensured fiscal frugality and also
because his government pursues strategies of survival - not necessarily
dependant on donor approval.

In Rwanda , ministers and other high ranking public officials resign and or
are fired by the week because of allegations of corruption. From the lowest
clerk in a government office to the most powerful minister or military or
security chief, no one is immune to jail when they steal; none close to the
president, none distant from him. You steal, you get jailed.

If there is some prima facie case that you stole, but there isn't not
enough evidence to convict you in a court of law, then you are asked to
resign or get fired. What a tough guy this Kagame man is!!








 
wakuu hii kitu nimeona nifanze ile wenyewe munasema copy and paste.
Ila nimeipenda kweli hii kama iko in reality.
Why not in tz?

by andrew m. Mwenda

last week i was in kigali , this time at the heels of a cabinet decision to
impound all luxurious four wheel drive vehicles bought at government
expense and driven by ministers, security and military chiefs, foreign
experts and their local handlers. In a morning crackdown, all the big men
and women of this republic woke up to find that police constables along the
main roads were stopping and taking away their vehicles and leaving them to
walk to office.
The international donor community, known all over africa for its corrupt
and profligate life styles which they indulge in the name of fighting
poverty, was this time caught with their pants down. They claim to fight
poverty while riding in luxurious four-wheel drive vehicles, sitting in
opulently furnished offices, earning obscene salaries and living in
executive mansions. In a bold act of defiance, rwanda impounded even those
vehicles belonging to donor projects. After cleaning his own government of
corruption, he has now taken on the profligacy of the international aid
industry and its experts are now scared.

In a discussion with president paul kagame, he told me that he had looked
at some of the "poverty reduction" projects and they smelt bad. "there are
projects here worth only $5m and when i looked at their expenses, i found
that $1m was going into buying these cars, each one of them at $70,000.
Another $1m goes to buy office furniture, more $1m for meetings and
entertainment, and yet another $1m as salaries for technical experts,
leaving only $1m for the actual expenditure on a poverty reducing activity.
Is this the way to fight poverty?" he asked as i shifted with glee in my
chair.

Already, the government is auctioning these vehicles and so far has gotten
over $3m from the sales. Mr kagame has now issued a new directive, saying
government should not purchase cars for its officials with more than 2,500
cc. But there is more: The government has placed a ceiling on mobile
telephone expenses for all its ministers, military and security chiefs to
50,000 rwanda francs (shs150, 000), and also ordered mtn rwanda to cut off
their international roaming access.

The directive also stops the holding of workshops, seminars and conferences
on poverty reduction in posh hotels like the intercontinental, mille
collins etc, insisting they should be in government owned buildings at no
cost. The order also requires all government ministries; departments and
agencies to move from privately owned buildings where they pay high rents
to government owned buildings.

I told kagame that whereas some of the most highly skilled africans are
going to europe and north america to clean streets and toilets, our
development partners send us Œtechnical experts on these projects at
individual monthly salaries of between $10,000 and $20,000, a salary that
could pay 12 africans of better training and experience and save this
continent from severe brain drain. In fact, most of these so-called experts
are a miserable, career-stranded lot in their own countries, but are dumped
in africa and other poor countries through foreign aid protocols.

Donors never shy from lecturing our governments on fiscal frugality, yet
their aid driven projects are the most profligate. Of total project aid to
uganda 's ministry of health, 93 percent of it goes into technical
assistance (i.e. Salaries and allowances for the experts) and overheads
(i.e. Four wheel drive vehicles, opulent office furniture, computers,
stationary, tea and cakes).

Only a miserable 7 percent of this aid goes into purchase of drugs. Now you
understand why, in spite of a huge health budget, our people cannot find
drugs in hospitals. We in the media have been shouting ourselves hoarse
against government corruption. It is time to expose the worse forms of
profligacy, which forces our governments to pile up huge sums in debt.

In fact, of the total money from the uganda government budget to the
ministry of health, 98 percent reaches its intended beneficiaries, clearly
showing that in spite of its corrupt ways, the government of uganda is a
better evil than donors. Of total project aid to uganda , 68 percent goes
into overheads and technical assistance. Only 32 percent to its intended
beneficiaries.

A few weeks ago i presented the above facts to president yoweri museveni
and asked him to act. My heart bleeds to say he is so deeply discredited by
his inability to tackle corruption in his government, and his own
profligate public administration expenditure that he lacks moral authority
to take on donors.

The other reason is that his regime lives off this coalition of mutual
deceit with donors that both are fighting to eradicate poverty in uganda .
Kagame, however, is able to act boldly because he occupies a moral high
ground in fighting corruption, has ensured fiscal frugality and also
because his government pursues strategies of survival - not necessarily
dependant on donor approval.

In rwanda , ministers and other high ranking public officials resign and or
are fired by the week because of allegations of corruption. From the lowest
clerk in a government office to the most powerful minister or military or
security chief, no one is immune to jail when they steal; none close to the
president, none distant from him. You steal, you get jailed.

If there is some prima facie case that you stole, but there isn't not
enough evidence to convict you in a court of law, then you are asked to
resign or get fired. What a tough guy this kagame man is!!

[font=&quot] [/font]







woooooowwwww...that's awesome...awesome...bravo kagame...show 'em wat you are made up!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Good ni kweli huyu Kagame kwenye mambo ya kusafisha serikali yake ni no.1 Afrika vilevile Kigali ni mji msafi hivi sasa...Sisi hapa Tz longolongo nyingi badala yake JK kaagiza BMW mpya sijui ngapi wakati zile benz na landcruiser za mwanzo bado zipo. Mawaziri wetu wako radhi tule majani lakini rais anunuliwe ndege 'what a rubbish'.

hivi ni kwa nini hawa mawaziri / viongozi hawapewi Rav4 au Vitara ambazo cost zake ni theluthi ya haya mashangingi wanayotumia sasa...vilevile ni nafuu kwenye service.

JK na Mizengo angalieni wenzenu wanavofanya nasi tuige mazuri, achaneni na hanasa zisizo na tija huku mnadhidi kuomba misaada kila kukicha...

tatizo Kagame ni kwenye demokrasi inaonekana hataki upinzani maana kwatai ndani wapinzani wake na inasemekana uhuru wa habari Rwanda unarudi nyuma. Hata kwenye ufanisi wa serikali na kuwanyoosha viongozi yuko bomba...

Maybe huyu bwana ndie atakaefaa EA federation kama kweli hiyo ndoto itatimia...yetu macho.
 
Copy and Paste za hivi zinasound kabisa!
Mimi mwenyewe nimeisoma huku napata burudani mwilini na rohoni!
Ni article moja saaafi sana, kama ni ukweli!

Rwanda wanaenda kwa kasi sana kimaendeleo, soon and very soon watakuwa mbali sana kutuzidi!

Vita juu ya corruption ni inevitable kwa nchi yoyote inayolenga kujenga heshima, ndio maana huko China wanapiga risasi mafisadi!!

Ukipiga vita corruption bila kutazama sura ya mtu unaongeza sana matumaini ya wananchi kwa serikali yao..hakuna mwananchi asiyeumizwa na ufisadi, hivyo mwisho wa siku unakuta taifa zima linaona(physically) matokeo ya kazi hiyo njema!

Hongera sana Kagame!.....Tanzania tumelalia Masikio!!...Concetration ya serikali ni 2010 rally...basi!
 
Copy and Paste za hivi zinasound kabisa!
Mimi mwenyewe nimeisoma huku napata burudani mwilini na rohoni!
Ni article moja saaafi sana, kama ni ukweli!

Rwanda wanaenda kwa kasi sana kimaendeleo, soon and very soon watakuwa mbali sana kutuzidi!

Vita juu ya corruption ni inevitable kwa nchi yoyote inayolenga kujenga heshima, ndio maana huko China wanapiga risasi mafisadi!!

Ukipiga vita corruption bila kutazama sura ya mtu unaongeza sana matumaini ya wananchi kwa serikali yao..hakuna mwananchi asiyeumizwa na ufisadi, hivyo mwisho wa siku unakuta taifa zima linaona(physically) matokeo ya kazi hiyo njema!

Hongera sana Kagame!.....Tanzania tumelalia Masikio!!...Concetration ya serikali ni 2010 rally...basi!

Kuna watu humu ukimtaja tu Kagame basi watakushukia kama tai vile, sijui kwanini huwa hatupendi kusikia mazuri ya watu. Jamaa kwa kweli anajitahidi sana, na ana uchungu sana na nchi yake, ni mzalendo wa kweli. Sasa rudi bongo halafu mthaminishe muungwana ... ni vituko vitupu! na bado anataka aongezewe term ya pili!! .... ajabu sana!!

Kuna huyu bwa'mdogo mwingine naye wa hapa DRC, anajitahidi sana. DRC nayo serikalini ilikuwa inanuka kwa rushwa kama bongo, lakini huyu kijana anajitahidi sana kusafisha, sasa hivi anaijenga nchi yake kwa kasi sana na sitoshangaa baada ya miaka 5 itajayo tukawa tumeachwa mbali. Bado yuko kwenye vita huko pembezoni mwa nchi yake, lkn ukiangalia highways anazojenga hapa Kinshasa (wenyewe wanaita boulevards) zina tia moyo, ni 6 lanes hata Dar hakuna. Wananchi wake wanampenda sana, sasa hivi anawapiga chini kiana wa-belgiji na wafaransa na tenda zote karibu za ujenzi anawapa wachina, hata ukifika hapa kinshasa utaona population ya china inaanza kuongezeka.
Jamaa hana majisifu kabisa kama muungwana, nina wiki 2 hapa kinshasa lakini sijawahi kusikia sauti yake kwenye media; .... bongo kazi tunayo .. lol!
 
Back
Top Bottom