Nafikiri kuwa ili kuondoa non-sense zinazoendelea ktk nchi nyingi za Afrika, mtazamo wa Kagame ni sahihi kabisa. Tunahitaji maendeleo, na dikteta ambaye atatusaidia kuyapata hayo maendeleo ni bora kuliko kuendelea kukaa na 'uswahili" usiokwisha na maneno tele bila maendeleo.
Namsifu Kagame kwa kuweza kutumia strength yake ya kupanga mikakati ya kijeshi kuhakikisha Rwanda inaendelea kusonga mbele kimaendeleo tena kwa mkono wa chuma.Hataki kulea rushwa na wapinga maendeleo kwa kigezo cha demokrasia.Mbona hata Putin anafanya hivyo na Rusia imeweza kurudi taratibu pale inapotaka kuwa?
Nchi yetu hii tunapenda wapiga hadithi kuliko watekelezaji sasa tumekwama.Mambo hayaendi.Kila siku sound nyingi bila utekelezaji.
Pengine sijaifahamu vizuri Rwanda, lakini nahisi tuna utajiri mkubwa kuliko wao. Sidhani kama wana mali nyingi tulizonazo kama dhahabu, gas asilia, vito, bandari etc? Mara nyingine ili mambo yaende tunahitaji mtu kama Kagame.Demokrasia inayodhidi kutupeleka kwenye umaskini haitatusaidia mana tutaishia kupigana bila sababu.Imetuzalia ufisadi na rushwa isiyokwisha.
Lakini hata JK ni askari..tumpe muda atumie uzoefu wa kupanga mikakati ya kijeshi kutuletea maendeleo. Tatizo ni mpaka lini tutamsubiri?
Kazi kwelikweli
Hali ya Rwanda ni tofauti sana na watu wanavyoiona kwa nje, na Kagame sio role model kama watu wanavyofikiria. Tatizo la Africa ni kuwa lile suala la kufanya kazi au kuitumikia nchi kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote hakuna. Nyerere tu ndio alikuwa na mtazamo wa namna hiyo. Ukiona kiongozi ana onyesha kuwa mkali na kuonyesha kuwa analinda maslahi ya nchi basi ujue ni kwa ajili ya wachache. Rwanda kuna rushwa nyingi na michezo michafu mingi sana. Ila wanaoruhusiwa kuifanya ni wachache waliokaribu na utawala, na wanaotoka kabila fulani. Wengine hata uhuru wa kufanya maombo yao na kutoa maoni yao hawana. Mchezo mchafu alioufanya DRC Congo na anaoendelea kuufanya ni kielelezo tosha cha jinsi Kagame alivyo.
Bado Kagame hajaweza kuwa role model wa Africa, bado sana.