Paul Kagame: An African role model?

Kwa sehemu kubwa nakubaliana na uchambuzi wako mkuu Masanja.Ila nahisi unapoteza consistency pale unaposema kuwa "hakuna mahakama iliyosema kuwa Kagame ni guilty...".Nakumbuka siku mkuu Dsm alisema kitu kama hicho kuhusu RA na ulimshukia kwa very strong points.Sasa leo nawe unatokea kulekule.Jamani "tumeanza kumwangalia nyani usoni?".Pls tutumie kipimo kilekile.
 

Mkuu inawezekana kupoteza concistency. Unajua, kuna watu hapa wanataka jamaa aonenekane muuaji tuu..hata yale mazuri ambayo ameyafanya kwa wananchi wake..yafukiwe. Kagame amekuwa villified na public opinions. Kama amefanya makosa basi ashitakiwe just like any other person. Siyo kuleta hizi verdict za UN and Co..kuvillify watu hapa...UN haina credibility kutwambia nani muuaji..wakati walikuwa na nafasi ya kuyaepusha haya mauaji....wakashindwa..just like US has no credibility ya kutwambia eti Iraq kuna democrasia..Its hot air!

Ukweli ni kwamba Muuaji ni muuajai tuu..Kama Kagame aliua basi vyombo husika vimchukulie hatua. Two wrongs dont make it right. Tatizo just like most of the things..this world is full of injustice. Nani anakupeleka mahakamani?

I have to be honest: I dont like French policies in Africa. Leo wanampa silaha Idrisa Deby.. Chad..wakati ndo hao hao wanawapa silaha rebels wanaompinga....Ndo nchi inakumbatia madikteta hapa Africa..guess what France said abaout Madagcasar?..kwamba hawatabadilisha foreign policy yao..ingawa AU, UN nk wameshapigfa kelele mpaka wengine kama US kukata misaada..France yeye..anaona sawa tuu..kwa sababu..maslahi yake yako intact...Its high time..we say no to countries like France...Usipokuwa mfuatiliaji wa hawa jamaa wa magharibi....unaenda na bandwagon..ya CNN na BBC..I tell you..uko kwenye matatizo. Go deep and find out....Its high time..Africa we get our own Aljazeera.

Harafu kikubwa ninachokiona..waswahili wengi...tunaona aibu...nchi ndogo ambayo tumewatunzia wakimbizi thousands and thousands..leo inapiga hatua kubwa..tusiogope challenge. We can do better with right atitude and determination.
 
- Mkuu kuna facts zaidi za kuthibitisha haya, au hizi ni dataz umezitoa huko?

FMES!

Mkuu FMES,

Nimesoma tena na tena post yangu, sikuona mahali ambapo nimeandika jambo ambalo nahitaji kutoa ushahidi kuthibitisha niliyoyaandika. Nimejaribu kuwashirikisha yale ambayo niliyapata wakati mimi na jamaa zangu tulipopata nafasi ya kupunga upepo na kupooza koo, huku tukijadili hili na lile. Nimeomba kueleweshwa. Kama ningekuwa na hizo data, wala nisingejaribu kuuliza haya mambo. Lakini pia nimeendelea kusema kuwa itakuwa vizuri kujadili bila kuangalia upande mmoja tu. Yaani tusifanye kazi ya kumpamba Kagame au kueleza mabaya yake tu. Ningependa tupate picha ya hali halisi ili angalau tujue ukweli wa mambo kuhusiana na huyu jamaa. Hii ni kwa sababu wapo watu wanamwona kama mtu anayetenda mambo ya nguvu katika kuwaletea watu wake maendeleo. Labda tunweza kupata moja au mawili ya kujifunza!

Tayari wewe ni shahidi kuwa watu wametoa michango ambayo binafsi nimefaidika sana katika kumjua jamaa na pia kujua jinsi Rwanda ilivyopiga hatua pamoja na matatizo ya mauaji ya 1994. Jambo la msingi ambalo tunatakiwa kukumbuka ni kuwa wajibu wa kiongozi ni kuleta maendeleo ya watu wake na si kwa majirani. Kwa hiyo kama Kagame anafanya mambo ya maana kwa watu wake apewe sifa. Pia kama anafanya mauaji nje na ndani ya nchi alaaniwe na vyombo vinavyohusika vichukue hatua. Mbona rais wa Sudan anatakiwa The Hague? Baada ya 1994, nadhani nchi kama Rwanda inahitaji Dikteta na kama Kagame anafanya mambo ya maana ninamuunga mkono. Longo longo nyingi ndo mwanzo wa kuleta Somalia nyingine. Hakuna anayehitaji huo upuuzi. Na katika hali kama hiyo lazima watu wengine waumie na hata kufa!
 
Pamoja na kuwa Kagame alishiriki kuua warwanda lakini tuangalie baada ya kuingia madarakani amefanya nini.Africa tunahitaji Raisi mwenye msimamo kama KAGAME
Kama udikteta Moi,M7,Gadafi,Mugabe na wengine wengi nao ni madikteta
 

Masanja,

..nimesema Rwanda hatulingani nao. vilevile there are better role models when it comes to economic turn arounds than Rwanda.

..chukulia Mozambique: watu zaidi ya millioni 1 walikufa; wakimbizi wa ndani zaidi ya millioni 4; mfumo wa elimu, afya, viwanda, na kilimo uliharibiwa kabisa kabisa; tatizo la mabomu ya ardhini liliendelea kuwepo.

..Tanzania tuna matatizo mengi sana na karibu yote tunaweza kuyatatua ikiwa tutapata uongozi makini. pamoja na kusema hayo sidhani kama Tanzania tunahitaji kiongozi kama Kagame ambaye ana damu ya wananchi millioni 3 wa DRC.

NB:

..vurugu za Kagame dhidi ya wananchi wa DRC zimetuletea wakimbizi wa-Tanzania.

..mkoa wa Kigoma umeathirika sana na vita ya DRC. ujambazi umeongezeka, mazingira yameharibiwa, shughuli za uchumi zimezorota.

..kwamba kuna wa-Tanzania hapa wanamuenzi Paul Kagame ina maana hawajali maisha na usalama wananchi wenzetu wa mipakani kama Kigoma.
 


Nimesoma posts zote kwenye hii thread, sijaona hata mtu mmoja anamuenzi Kagame. Labda utusaidie kututajia mtu anayemuenzi Kagame.

Kwa maoni yangu, watu wamejaribu kuelezea ni mazuri kiasi gani amewafanyia Wanyarwanda na mabaya pia. Kama kuna mtu yuko subjective hayo ni matatizo yake. Mimi naona watu wamechangia objectively. Kwamba Kagame ameua watu DRC haina maana kwamba hajawafanyia mazuri Wanyarwanda. Tumesema sana kuhusu hilo kwenye michango yetu ya nyuma. Kwa hiyo unaweza wewe kujikita kwenye kutuelimisha kuhusu mabaya yake (his dark side) bila kuwatuhumu wale wanaochangia upande wa mazuri yake. Hatuwezi kuwa sawa kwa jinsi tunavyoona mambo. Hata hivyo,hicho hakiwezi kuwa kigezo cha kuonana wabaya (to give names to each other). Namna hiyo tunazuia mchakato kwa kuelimishana!!
 
Bado Data zilizopo hazituonyeshi kuwa Rwanda au hata Msumbiji wanafanya vema kuliko Tz!

Life expectancy, per capital income, uhuru wa vyombo vya habari na kutoa maoni Tz ni kubwa zaidi kuliko hizi nchi mbili!

Sasa mnaposema Rwanda wanafanya vema ni vigezo gani mnatumia? May be wingi wa akina mama ktk Bunge na kupiga vita ufisadi?

Rwanda ni nchi ndogo sana kwa enoe huwezi kulinganisha na Tz! Ni kama tu mkoa wa Kagera au zaidi kidogo!
 

Mkuu,

Hapa nakubaliana na wewe partly.

Mimi nimekaa Kigoma for close to eight years. Ni ukweli usiopingika kwamba Kigoma imesahaulika kabisa katika mipango ya serikali yetu. Social services are just pathetic and at times non existent.

Ndo hapa nawaambia wananchi wenzangu..tujaribu kufanya independent study zetu pale tunapoweza. Kwa kiasi kikubwa Wana Kigoma walisaidiwa na wakimbizi wa hiyo hiyo DRC unayoibeza. Watu tumefanya biashara na DRC..nguo na mazagazaga mengine tumekuwa tukichukua Congo. Maana kipindi hicho hata bia ya Tanzania haifiki Kigoma...tulikuwa tunakunywa Primus za Burundi....Yes, wakimbizi walifanya uharibifu wa mazingira..lakini..hao hao ujio wao ulitoa ajira kiasi...wananchi wakafaidika.. si haba..

Tusiangalie tuu..kauli za wanasiasa..Its easy..kwa Chiligati au Masha kama waziri wa mambo ya ndani kusimama bungeni na kutoa mlolongo wa athari hasi za wakimbizi..lakini huyo huyo anasahau kwamba isingekuwa Wakimbizi..Kigoma auu Ngara..hata zisingesikika...maana I can assure you these places zimetengwa mno..

All in all, Mimi naweza kusema kwamba athari za wakimbizi zimekuwa mixed. Positive na negative. Sema tatizo kubwa la nchi zetu ni kutumia fursa kama hizo..Kigoma..sijui kama itaendelea kama imeshindwa kusonga mbele wakati wakimbizi wakiwepo na mzunguko wa pesa ukiwa Mkubwa..so is Ngara...
 
Ni kweli, Kagame is doing very well.

(a) Kuna mama mmoja wa Kinyarwanda tulikuwa tunafanya naye kazi hapa Marekani, ameamua kurudi kwao ambako amepokelewa kwa mikono miwili na analipwa karibu sawa na alivyokuwa akilipwa hapa ukiachilia mbali unafuu wa maisha ya huko.

(b) Infrastructure ya Rwanda kwa sasa hivi ni nzuri sana kuliko nchi nyingi za Afrika ya Mashariki na ya kati, na zinazidi kuimarika.

(c) Kwa sasa hivi Rwanda wana jeshi imara kuliko nchi zote za Afrika ya Mashariki ya kati, hata rafiki yake wa zamani M7 anaogopa jeshi la Rwanda, lakini waswahili tunajifanya tuko mbele huku tukitumia silaha za miaka ya 40!!
 

Mkuu,

hizo data nani katoa? Jamani..umasikini na maisha tunaishi sisi..harafu wanaokuja kutupimia hali ya maisha yetu ni watu wanaoishi Paris na Washington..wapi na wapi?


Wengi walioandika humu..wameshapita Rwanda....sasa mkuu..utakataa kwamba Kigali si safi..simply because "data hazisemi hivyo" hata kama umetembelea Kigali ukajionea? Au utasema kwamba watanzania ni matajiri simply because statistics za IMF zinasema hivyo hata kama...kijiji kizima hakuna zahanati wala maji ya bomba?

Jamani .....Masikini ana wakati mugumu sana..yaani hakuna anachoweza kufanya kikakubalika..as long ni masikini..duh! Yaani hata umasikini wetu hatuujui? mpaka tuambiwe/tupewe dataz? Kazi tunayo..ila kitaeleweka tuu...
 
Masanja,

..inaelekea damu ya watu waliouawa na Kagame haina thamani kwako. "mema" aliyoyafanya yanafunika kabisa kuhusika kwake na vifo zaidi ya millioni 3.

..kwa msingi huo tutakuwa hatujakosea kujadili rekodi ya Habyarimana na Interahamwe na ikiwezekana tupate role models humo na tuwaenzi.

..je, uliwahi kufika Rwanda wakati wa Habyarimana? Wanyarwanda walikuwa wanaishi maisha ya namna gani wakati na baada ya utawala wa Habyarimana?

..je, infrastructure za Rwanda ziliharibiwa kiasi gani na civil war, pamoja na genocide iliyofuatia?

..SIKUTAKA TUFIKISHANE HAPA. KWAMBA SASA WAAFRIKA TUNAJADILI WAUWAJI. WAAFRIKA SASA HATUJALI MAISHA YA WENZETU AND WE FIND ROLE MODELS IN MURDERERS.

Kichuguu,

..Rwanda wamejenga barabara za lami za urefu gani tangu Kagame aingie madarakani?

..how many clean water, rural electrification,... projects have been completed since he came into power?

..Jeshi la Rwanda linaweza kuwa most efficient katika kuuwa kuliko majeshi yote ya Afrika Mashariki. lakini sidhani kama Jeshi hilo ni efficient ktk shughuli za uokoaji na huduma za jamii, ulinzi wa amani, au uzalishaji mali mfano kama kilimo etc.

..economic and social transformation iliyotokea Mozambique baada ya civil war inaizidi kabisa hayo yaliyofanywa na Kagame. vilevile transformation hiyo imeongozwa na watu ambao hawajachuka kwa damu kama Kagame. kwanini hatutaki kuwaenzi hawa wa Msumbiji tunangangania Kagame tu?
 
- Wewe bwana waulize wa-Ganda, under Idd Amini maisha yalikuwa bora sana kiuchumi kuliko Obote, sasa kwa hii mantiki naona Idd Amini naye awekwe kwenye kundi la Kagame yaani Role Model, au?

FMES!
 
Nimesikia jana kwenye vyombo vya habari Rwanda imejitoa kuwa host wa SULIVAN meeting mwaka kesho kwa sababu wana mipango iliyo na manufaa zaidi kwa taifa lao. Tanzania sisi tuliingia kichwakichwa kuwa host wa SULIVAN meeting bila kuwa na priority!! Mkutano ule haukuwa na manufaa yoyote kwa taifa letu na watu wake, hata wale wa machinga/wajasiriamali waliokwenda pale walipata hasra tupu. Kwa uamuzi huu wa kuachana na kuwa host wa SULIVAN meeting namuona Kagame kkuwa anaweka maslahi ya nchi yake nma watu wake mbele, siyo role model kwa sasa kutokana na kuingia madarakani kiutata utata ila ana sifa za kuingia kwenye role model wa viongozi wa Afrika.
 
DarkCity said:
Nimesoma posts zote kwenye hii thread, sijaona hata mtu mmoja anamuenzi Kagame. Labda utusaidie kututajia mtu anayemuenzi Kagame.

DarkCity,

..mtoa hoja ameuliza kama Kagame ni role model. sasa ukikubaliana na hilo, basi ni sawasawa kabisa na kumuenzi.


FMES said:
- Wewe bwana waulize wa-Ganda, under Idd Amini maisha yalikuwa bora sana kiuchumi kuliko Obote, sasa kwa hii mantiki naona Idd Amini naye awekwe kwenye kundi la Kagame yaani Role Model, au?

FMES,

..umenikumbusha kuna wa-Tanzania waliamua kumsomea hitma Iddi Amini.

..hata wakati wa Hitler Ujerumani ilikuwa na maguvu ya ajabu. they almost concurred the world. labda wa-Tanzania tumfanye Hitler role model.
 

JK

Hitler hawezi kuwa role model wetu Kwa sababu ameshakuwa villified na dunia. Hivi nikuulize..ingekuwa vipi..kama Hitler angeshinda ile vita ya pili ya Dunia? Unafikiri watu wangekataa kuji-associate naye? Leo Hitler angekuwa ni shujaa sana. LAKINI kwa vile alishindwa vita ndo hapo..yote unayasikia...Hata wajerumani hawataki kumskia..Ingawa Hitler ni kiongozi aliyekuwa na mvuto mkubwa sana na wajerumani walimpa support ya kufa na kupona...GBush alienda Iraq 2003..support ya wananchi ilikuwa over 80%...wengi watakudanganya..ohh..aliudanganya umma..ohh..visingizio kibao..lakini ukweli wengi walijua Sadam hana silaha.....mambo yaliharibika waliposhindwa vita..Unadhani Bush angeshinda ile vita kama walivyotegemea..nani angemuona Bush muongo? Jiulize mbona 2004 alichaguliwa..wakati wanajua silaha za maangamizi hazikuwepo..jamaa alidanganya? Its simple..the guy lost the war! Ndo maana wananchi wakamgekua...But before they new kwamba hakuna cha silaha wala nini..ni maslahi ya taifa mbele...

Same applies...Leo Israel katika kujilinda anajikuta anauwa wapalestina kibao..lakini kwa vile wakubwa wako upande wake..no body makes noise..hata hapa JF..we dont complain..tunaishia kusema Israeli ina haki ya kujilinda..we dont question conventional wisdom....hawa wapalestina hawana haki ya kuishi kama taifa huru?.. Kama US na wenzake wangekuwa against Israel, I can bet myself....wote hapa tungekuwa tunaicondemn Israel.

Binadamu especially waafrika..hatuna independent source of information..ndo maana..ni mara chache kama zipo..umeshawahi kuona wasomi hata hapa JF wanarefer dataz za waafrika..kila mtu kujenga hoja ana-rely kwenye takwimu za magharibi. Ndo maana hata kama kitu kiko Kenya au Burundi..hata gazeti la TANZANIA wata nukuu BBC au CNN..ingawa hawa CNN etc..wako miles away. Thats the way things work bro. If you dont attempt to think outside the box..utadhani things are fine..lakini..wazungu wametulemaza sana..uwezo wetu wa kufikiri umekuwa affected sana..tena sana.

TATIZO LETU WAAFRIKA NI KUBWA MNO THAN MEETS THE EYE. HATA BONGO ZETU ZIMESHAATHIRIKA..IT WILL TAKE AGES TO MAKE A COMEBACK-IF WE EVER WILL.
 
Tumpe muda JK ili afanye nini hicho cha maana au ili asafiri zaidi? Shame on us kwa kweli hivi kwa miaka mi3 tumefanya nn zaidi ya kusafiri na porojo? Three years hata timu ya kazi imekuwa ngumu kuitengeneza!! Hivi kosa gani kubwa tulifanya kwa Mungu mpaka akachukia hivyo na kutuadhibu kwa kutunyima uongozi? Inatia uchungu kwa kweli wakati wenzetu wanasonga mbele kwa speed ss tunabackslide kwa speed pia. Ooh Tanzania pole utajiri wote ulionao lakini unaongoza kwa umasikini pia.
 
=JokaKuu;417961]
DarkCity,

..mtoa hoja ameuliza kama Kagame ni role model. sasa ukikubaliana na hilo, basi ni sawasawa kabisa na kumuenzi.

Joka, ni vizuri kwamba umeona kuwa mtoa hoja ameleta swali kwetu ili tujadili. Sidhani kama kuna mjadala wowote unaoweza kuitwa mjadala kwa kuangalia upande mmoja tu wa shilingi. Lazima tuangalie pande zote mbili ili wafuatiliaji wenyewe wafikie mahali waamue (to make an informed decision in their minds) kuwa kweli jamaa ni role model au la. Labda niongeze swali jingine hapa, kwani mtu anaweza kuwa role model kwa baadhi ya vitu na hapo hapo akawa bad model kwa mengine? Yaani Kagame anaweza kuwa role model kwa kuendeleza na kujali maslahi ya nchi yake na hapo hapo akawa mfano mbaya wa viongozi wanaosujudu mauaji ya raia wasio na hatia?


FMES,

..umenikumbusha kuna wa-Tanzania waliamua kumsomea hitma Iddi Amini.

..hata wakati wa Hitler Ujerumani ilikuwa na maguvu ya ajabu. they almost concurred the world. labda wa-Tanzania tumfanye Hitler role model.

Binafsi sioni kama wana makosa endapo walifaidi sana wakati wa utawala wake. Pia sidhani kama walivunja sheria kwa kufanya jambo hilo. Lakini pia wanaweza wakawa walimsamehe na kama ni watu wa dini basi hawana sababu ya kutomsomea dua.
 
Last edited:
- Wewe bwana waulize wa-Ganda, under Idd Amini maisha yalikuwa bora sana kiuchumi kuliko Obote, sasa kwa hii mantiki naona Idd Amini naye awekwe kwenye kundi la Kagame yaani Role Model, au?

FMES!

FMES, tukipata jibu la swali lako na lile la mtoa mda mjadala utakuwa umeisha. Na kwa vile hatujapata jibu ambalo wafuatiliaji wengi tunakubaliana nalo basi tunaendelea na mjadala huku tukielimishana.

Binafsi nawafahamu jamaa wa Uganda ambao walikuwa wanamlaumu sana Nyeyere kwa kumuondoa madarakani Idd Amini. Kuna mambo mengi sana ambayo alikuwa anayafanya na wananchi waliridhika naye. Mfano ni suala la kutokuwa na huruma na watu wazembe pamoja na mafisadi. Pia suala la kuwafukuza Wahindi ni jambo ambalo Waganda wengi walilifurahia. Kwa hiyo, wapo watu wengi waliompenda Amini. Hayo ni maoni yao. Binafsi sikumpenda Amini na siwezi kumwona kama kiongozi bora wa kuigwa. Pia sina mapenzi yoyote na Kagame. Nilichosema ni kuwa, kuna taarifa kuwa anafanya mambo ya maana sana na yenye kuwaletea maendeleo wananchi wake. Hili ni suala la msingi sana. Rais jukumu lake ni ustawi wa nchi yake kwanza. Wachangiaji wengine wametoa mifano mingi tu, ukiwemo wa Marekani na G.W Bush. Kwa hiyo kama mtu ana data zinazoonesha jinsi jamaa alivyo muuaji na anavyoshindwa kuendesha nchi yake basi atupe. Hata tukikosa data siyo kwamba kuna mtu atamtangaza Kagame kuwa role model kwani hili swali si lazima lipate jibu la ndiyo au hapana. Binafsi naendelea kupata shule.
 
Mi nadhani Kagame is a dictator, but a benevolent and enlightened one. Idd Amin was also a dictator but less enlightened. Museveni nae ni kadictator lakini he is somehow benevolent and enlightened. Moi also is made of similar stuff.

Common denominator ya madictator wote ni kwamba ukipinga ideas zake waziwazi they wont take it kindly. Hii ndo weakness yao.

Otherwise, critical mass ya sisi Waafrika, ambao hatuwezi ku-analyse issues, tunahitaji kutawaliwa by benevolent and enlightened dictators kama Kagame. Kagame anasema Africa is not ready for western-style democracy. Mission yake ni "kuwa-andaa" Wanyarwanda ili waweze kujiongoza kwa demokrasia wanayoona itawafaa wao hapo baadae. Anawaelimisha na kuwajengea miundombinu bora.

Nakubaliana nae in principle ndomaana nafikiri he should be a role model for African leaders/rulers. Also watu kama Gaddafi na Mugabe are in this league. I support them.
 
You know, I would rather fan on Kagame who knows how to attract real investment than looking for an opportunity to meet Shaq, Jay Z, 50 Cent or Michael Jordan!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…