Paul Christian Makonda anafaa kuwa Waziri

Ichwampaka

Senior Member
Nov 19, 2018
135
109
Paul Makonda alipewa nafasi ya ukuu wa wilaya na Rais JK akafanya vyema sana, Rais JPM baadaye akampa ukuu wa mkoa Dar. Hapa pia amefanya vizuri sana inategemea mzani unaotumia kumpima (sisi tunampima kwa ilani ya CCM).

Ngazi hii pia anapaswa kuivuka, msukumo wa kuhamia ngazi nyingine unapaswa kutoka kwa mtu mwenyewe. Makonda kachukua fomu ya kugombea ubunge Kigamboni (huu ni msukumo wa ndani wa kwake mwenyewe).

Ukiwa mbunge, unaweza kuwa waziri na ukiwa waziri una nafasi kubwa ya kuwa waziri mkuu na hata baadaye inakupa mpenyo mzuri wa kugombea urais. Makonda angeweza kusubiri uteuzi wa viti vile kumi, lakini kama kawaida yetu maneno yangejaa kuwa amebebwa. Kaamua kujitosa bado maneno kibaooo.

Akili inaniambia huyu jamaa anapigwa vita asifikie ile destination yake. Usisubiri mtu akuamulie destiny yako, pambana. Hata Mungu hutenda muujiza katika kile ulicho nacho, Makonda shika ubunge kisha tuone huko mbele ya safari mambo yatakavyo unfold.

Wewe ni binadamu, hakuna binadamu asiye na mapungufu, ila mapungufu yako ni machache sana sana na yanavumilika na bado una nafasi ya kuendelea kujifunza na kubadilika. Karibu mbunge mtarajiwa wa Kigamboni tupo tayari kwenda na wewe. Tunasubiri maamuzi ya chama chetu.
 
Makonda ni janga kwa Tanzania yetu. Huyu ndie alimuambia jei pii emu "Mzee niruhusu mimi niwashughulikie, wewe uendelee na kazi zako". Huyu ndiyo mchana kweupe tulimwona anatinga Mawingu na mabunduki etc. Hafai hafai hafai. Huyu mpaka kesho vyeti vyake vina utata.
 
Makonda ni janga kwa Tanzania yetu. Huyu ndie alimuambia jei pii emu " Mzee niruhusu mimi niwashughulikie, wewe uendelee na kazi zako". Huyu ndiyo mchana kweupe tulimwona anatinga Mawingu na mabunduki etc. Hafai hafai hafai. Huyu mpaka kesho vyeti vyake vina utata.
Makonda atakuwa waziri ili anyooshe wajinga kama wewe!
 
Makonda ni mpambanaji kwenye kutimiza ndoto zake hili sina ubishi nalo na sina wivu wowote kwake. Na nampongeza.

Lakini sio kiongozi mzuri. Nadhani ni mtu wa kawaida saana aliyena akili za kawaida- average. Anatakiwa atawaliwe na sio kutawala. Ana uwezo mdogo.

Tuna matatizo mengi saana kama nchi. Kututoa kwenye changamoto tulizonazo tunahitaji watu smart. Lakini kama nikupeana uongozi pasipo kuzingatia hali ya watanzania ili uwafurahishe marafiki na watu wa karibu anafaa saana.

Mfano unampa uwaziri mkuu Makondo what do you expect?
 
huyu mwingine kalipwa kusifu na kutukuza Makonda yule dogo Robert Heriel kapata msaidizi! kweli uongozi raha si kwa kutafutwa huku! Makonda ni zero brain, vyeti feki, mtu hana akili na hana elimu analazimisha kwa rushwa na hongo kuteuliwa kuongoza raia!
 
Pumbavu sana,marekani ni mbinguni?au ndo kuna oxygen?
Marekani sio mbinguni, lakini ndiko wanasema ukweli - Makonda alikuwa akiwanyim watu haki ya uhai. Unajua maana yake? Alikua anaua watu. Sasa tuanze na hapo. Nani anataka kiongozi mwenye hatia ya damu kwa ajili tu ya mambo ya siasa? Yaani uue watu halafu useme unaomba kura zao, wai! UKiwa Mbunge watu wako wakakukosoa si utawaua kama huko nyuma ulivyoona ni halali kuua watu wanaokosoa!

Na wakimpitisha tutamuuliza juu ya hili suala. TUnamsubiri kwa hamu. Siku hiyo hata BBC, CNN tutawakaribisha, Makonda akiulizw swali juu ya kunyima watu haki ya kuishi.
 
NI MWIKO, MWIKO KABISA KUINGIA KWENYE KICHWA CHA MWENYEKITI NA KUJIPANGIA KAZI. MKILA VYA WATU MTAVILIPA.
NAKUMBUKA NENO. MTAVITOA KUPITIA TUNDU LOLOTE LA MWILI!
 
Hizo Chuki zenu binafsi tu Kwa Comred Makonda sisi tunamuona anasifa zote na anafaa kuwa Mbunge wa Kigamboni.
 
Paul Makonda alipewa nafasi ya ukuu wa wilaya na Rais JK akafanya vyema sana, Rais JPM baadaye akampa ukuu wa mkoa Dar. Hapa pia amefanya vizuri sana inategemea mzani unaotumia kumpima (sisi tunampima kwa ilani ya CCM).

Ngazi hii pia anapaswa kuivuka, msukumo wa kuhamia ngazi nyingine unapaswa kutoka kwa mtu mwenyewe. Makonda kachukua fomu ya kugombea ubunge Kigamboni (huu ni msukumo wa ndani wa kwake mwenyewe).

Ukiwa mbunge, unaweza kuwa waziri na ukiwa waziri una nafasi kubwa ya kuwa waziri mkuu na hata baadaye inakupa mpenyo mzuri wa kugombea urais. Makonda angeweza kusubiri uteuzi wa viti vile kumi, lakini kama kawaida yetu maneno yangejaa kuwa amebebwa. Kaamua kujitosa bado maneno kibaooo.

Akili inaniambia huyu jamaa anapigwa vita asifikie ile destination yake. Usisubiri mtu akuamulie destiny yako, pambana. Hata Mungu hutenda muujiza katika kile ulicho nacho, Makonda shika ubunge kisha tuone huko mbele ya safari mambo yatakavyo unfold.

Wewe ni binadamu, hakuna binadamu asiye na mapungufu, ila mapungufu yako ni machache sana sana na yanavumilika na bado una nafasi ya kuendelea kujifunza na kubadilika. Karibu mbunge mtarajiwa wa Kigamboni tupo tayari kwenda na wewe. Tunasubiri maamuzi ya chama chetu.
Alimpiga Mzee Warioba!!
1595234730459.png
 
Back
Top Bottom