FMES,
Kuwa mwanafunzi wa mtu haina maana kuwa utaiga au kufuata aliyokufundisha. Binadamu ndivyo tulivyo. Mwinyi alijiita kichuguu kwa kulinganishwa na Mwalimu lakini akawa wa kwanza kulizika azimio la Arusha na kutuletea azimio la Zanzibar. Na juzi tu katwambia kuwa azimio la Arusha lilikuwa ndoto. Huyu wa sasa anasema ukizungumzia azimio la arusha leo watakuona chizi. Ni kweli kulikuwepo na rushwa wakati wa utawala wa Mwalimu lakini kulikuwa pia na hofu ya kuogopa kugunduliwa na authorities na subsequent consequences. Lakini wakati wa Mwinyi lilikuwa jambo la fahari kuonekana unakula na wakubwa, wafanyibiashara etc. etc. Na huyu wa awamu ya tatu ndiyo kabisa akatumbukia kwenye limbwi la uozo wa rushwa na matokeo yake ndiyo hayo ya akina Zombe, Mahita na kukumbatiwa kwa mafisadi.
hatuna haja ya maelezo marefu, mfano mshaonyeshwa huko thailand.....!!
Zakumi,
Mkuu Azimio la Arusha lilikuwa kweli chini ya chama kimoja lakini hata hilo la Zanzibar.. maamuzi ya Azimio hilo yamependekezwa na kupitishwa na viongozi wale wale wa chama kimoja kabla hatujaunda vyama vingi..Kumbuka kuwa Miwnyi ndiye alikuwa rais wakati linapitishwa.
Pili, Azimio la Zanzibar halipotoshi ama kupingana na Azimio la Arusha kulingana na maelezo ya mwinyi, kama unakumbuka Mwinyi alisema haya alipokuwa akiliwakilisha isipokuwa ni MAREKEBISHO toka Azimio la Arusha ktk kipengele cha viongozi. Ni sawa na Agano jpya la Yesu kutopingana na lile la kale isipokuwa ni marekebisho ya baadhi ya Aya na nyongeza za yale yaliyokuwa yamekosekana mwanzoni ili waumini wapate kufanya ibada kwa ufasaha zaidi.
Mkuu ni muhimu sana uelewe tunapozungumzia viongozi ujue ni viongozi wapi tunaowasema...Hawa ni wale waliochaguliwa kushika madaraka ktk serikali inayoongoza - Toka rais mwenyewe hadi watu wote atakao WATEUA kushika nyadhifa ndani ya serikali yake, ndio watu wasioruhusiwa kuwa na biashara pembeni kwani majukumu waliyopewa yanawahitaji muda wote 24/7...
Azimio la Zanzibar liliwapa uhuru watu hawa kufanya biashara hivyo kuleta conflict of interest... na matokeo yake ndio haya ya kina Yona na Mramba, bado unatetea wafanyabiashara kuwa viongozi mkuu!
Hii ni Principal ya uongozi ktk serikali zote iwe ya Kibepari au ya Kisoshalist!... kwa hiyo usije danganyika kuwa Azimio la Zanzibar ni muhimu ktk kuendesha serikali ndani ya Ubepari..
Na ndio maana Kikwete ameondoa Azimio hilo ktk Uongozi wa awamu yake.. Ni moja ya sifa kubwa ninazompa hadi sasa hivi ingawa bado uetekelezaji wake haujakaa sawa.
Kwa mujibu wa Azimio la Zanzibar angeweza kupangisha nyumba yake ya mbavu za mbwa iliyopo Ukonga na kwenda kuishi Ikulu. Kwa kuipangisha nyumba yake angeweza kumsaidia mtanzania mwenzake. Hilo ndilo Azimio la Zanzibar.
hatuna haja ya maelezo marefu, mfano mshaonyeshwa huko thailand.....!!
Hata Azimio la Arusha liliruhusu viongozi kuwa na hisa japo kwa makampuni mawili, hivyo kumiliki mali kwa kiasi na si ulafi ilikuwa ni ruksa.
Sasa Azimio la Zanzibar likasema nyumba moja ya kupanga haitoshi, shurti Kiongozi awe na nyumba 7 kama za babu yake Nyani (Yohana wa Makopo)! Ndipo ulafi, uroho na umelo ukaanza!
Rev.Kishoka said:Hata Azimio la Arusha liliruhusu viongozi kuwa na hisa japo kwa makampuni mawili, hivyo kumiliki mali kwa kiasi na si ulafi ilikuwa ni ruksa.
Kishoka,
..Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili, na kuwa na hisa ktk makampuni ya kibepari.
..kuna watumishi wa serikali walifunga miradi yao ya kufuga kuku wa biashara ili kuzingatia miiko ya uongozi ya Azimio la Arusha.
..cha msingi hapa ni kuiboresha sheria ya maadili ya viongozi na watumishi wa serikali. hata sheria zetu za makosa ya jinai zinatosha kukabiliana na uhalifu uliotokea na unaoendelea.
NB:
..Azimio la Arusha na siasa za Ujamaa lilisababisha nidhamu ya kazi na productivity kushuka kwa kiwango cha kutisha.
Kishoka,
..Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili, na kuwa na hisa ktk makampuni ya kibepari.
..kuna watumishi wa serikali walifunga miradi yao ya kufuga kuku wa biashara ili kuzingatia miiko ya uongozi ya Azimio la Arusha.
..cha msingi hapa ni kuiboresha sheria ya maadili ya viongozi na watumishi wa serikali. hata sheria zetu za makosa ya jinai zinatosha kukabiliana na uhalifu uliotokea na unaoendelea.
NB:
..Azimio la Arusha na siasa za Ujamaa lilisababisha nidhamu ya kazi na productivity kushuka kwa kiwango cha kutisha.
Nakiri nilinukuu vibaya Azimio. Viongozi ndiyo waliopewa miiko na si wananchi wa kawaida. Sababu ya Viongozi kuwekewa masharti magumu ilikuw ani ili kuondokana na Viongozi kutumia vibaya madaraka yao na kujipatia ziada kwa misuli ya vyeo vyao.
Azimio la Zanzibar, badala ya kuweka japo vipingamizi fulani ili kuratibu huu mwanya wa kujipatia, limefungulia mlango na kila mtu sasa anakuwa nyang'au na kula kupita kiasi!
Nakiri nilinukuu vibaya Azimio. Viongozi ndiyo waliopewa miiko na si wananchi wa kawaida. Sababu ya Viongozi kuwekewa masharti magumu ilikuw ani ili kuondokana na Viongozi kutumia vibaya madaraka yao na kujipatia ziada kwa misuli ya vyeo vyao.
Azimio la Zanzibar, badala ya kuweka japo vipingamizi fulani ili kuratibu huu mwanya wa kujipatia, limefungulia mlango na kila mtu sasa anakuwa nyang'au na kula kupita kiasi!
Tatizo la manyang'au ni pale mzoga unapokwisha, wanaanza kutafunana wao kwa wao. Naona ndio wameanza na huyo ole wake atakayepona, tunamsubiri - sisi wananchi tuliochoka na ulafi wao - kwa ari na shauku. Twendeleze libeneke.
Zakumi,
Mkuu ebu kasisikilize upya Hotuba ya Mwinyi...naona kama unapotosha!
Ni kweli Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili na bado mimi naunga mkono kabisa jambo hilo.. Hisa ktk mashirika ruksa lakini sio mishahara unless mnayo tafsiri tofauti ya mshahara, ambayo nielewavyo mimi ni malipo ya mwezi kwa kazi uliyoifanya...
Halafu swala la Kupangisha nyumba ni bomu kabisa..haiwezekani kila mtu apangishe nyumba lazia kuwepo na utaratibu wa kupangisha ili kodi za mapato ya kupangishwa ziweze kukusanywa... Serikali inatakiwa kuweka maazimio yenye manufaa kwa Taifa na sio kutazama mtu mmoja mmoja, hapa nikiwa na maana kuwa unaporuhusu kupangisha nyumba lengo lkake linakuwa kutunisha mfuko wa serikali ktk pato la kodi za upangishaji, hivyo ni lazima iwekwe taratibu ambazo zitahakikisha kwamba wapangishaji wanafuata masharti ya kupangisha, sio swala la kumsaidia mtu mahala pa kuishi..
Kifupi mkuu wangu Azimioa la zanzibar ni bomu, viongozi hawatakiwi kabisa kujihusisha na biashara wala nyumba za kupangisha kutokana na madaraka waliyopewa..Ni ktk kutumia madaraka hayo ndio tunaona wakijenga hoja za mji mpya Kigamboni ambako wao wenyewe kwa kutumia madaraka yao hupewa nafasi ya kwanza kuchukua viwanja hivyo kujenga hizo nyumba za kupangisha...
Kisha hata siku moja tusifikirie kwamba kiongozi anaweza kuvua joho lake la uongozi kufuata utaratibu ambao unamweka yeye sawa na raia wa kawaida.. Hata siku moja hawezi kupanga msitari kupanda daladala mkuu wangu usijechanganya vitu hivi na ukweli unasimama peke yake...
Tunawalipa kodi zetu, mishahara mikubwa, magari majumba na kadhalika kuliko hata viongozi wa nchi za Ulaya tena hata baada ya kustaafu bado wanapokea ruzuku kubwa kuliko daktari wa Muhimbili, hivyo hakuna sababu kabisa ya viongozi hawa kujihusisha na biashara...
..Unachozungumzia ni Ethics au miiko ya uongozi katika Azimio la Arusha. Miiko ya uongozi ni sehemu tu ya Azimio la Arusha
Halafu swala la Kupangisha nyumba ni bomu kabisa..haiwezekani kila mtu apangishe nyumba lazia kuwepo na utaratibu wa kupangisha ili kodi za mapato ya kupangishwa ziweze kukusanywa... Serikali inatakiwa kuweka maazimio yenye manufaa kwa Taifa na sio kutazama mtu mmoja mmoja, hapa nikiwa na maana kuwa unaporuhusu kupangisha nyumba lengo lkake linakuwa kutunisha mfuko wa serikali ktk pato la kodi za upangishaji, hivyo ni lazima iwekwe taratibu ambazo zitahakikisha kwamba wapangishaji wanafuata masharti ya kupangisha, sio swala la kumsaidia mtu mahala pa kuishi.....