Patrick Rutabanzibwa: UKWELI ni upi?

Patrick Rutabanzibwa: UKWELI ni upi?

Tiba

Nijuavyo mimi (and I stand to be corrected) Ukuu wa wilaya ni kazi ya kisiasa na kazi za kisiasa kiuhalisia hazina kitu kinachoitwa KUSTAAFU. Utendaji wa serikalini ndio una kitu kiitwacho kustaafu. Ukuu wa wilaya, mkoa au hata uwaziri ni swala la maamuzi ya mtu mmoja kuamua akuteue au akuache kwa mapenzi yake. Na ni swala la wewe kukubali au kukataa lakini sio KUSTAAFU.

Kuna mama mmoja Mwanza alikuwa anateuliwa kila wakati na Che Nkapa katika nafasi za ukuu wa wilaya lakini alikuwa haendi sababu alikuwa anafanya kazi ya maana Unicef iliyokuwa ikimpa mapesa mengi. Nadhani na naamini kazi za kisiasa (ukiondoa urais kwa sababu baada ya kuchaguliwa hubadilika kuwa kama mtendaji na mwajiri mkuu wa watumishi wote wa serikali) huwa hazina KUSTAAFU kwa sababu hazina hata umri wa mwisho kuziomba hata ukiwa na miaka 90 unaweza kuteuliwa ama kuchaguliwa na wapigakura.

Nachelea kukubali kuwa Jenerali Ulimwengu ALISTAAFU Ukuu wa wilaya. Nadhani usahihi ni kuwa alikataa kupokea mabadiliko ya kuhamishwa ama uteuzi aliopewa na hivyo kuachana na siasa.

As I've said earlier, I stand to be corrected!

Mkuu bibikuku, kimsingi nakubaliana na maelezo yako. Basi tuseme Ulimwengu alijiuzulu nafasi ya ukuu wa Wilaya.

Tiba
 
Hapa hii habari inanichanganya.
Kuna report niliisoma juu ya hiyo IPTL saga, ambapo inasisitiza kuwa Patrick ndio alimfuata na kumshauri Mkapa kwa kumwambia waachane na IPTL then watafute alternative nyingine other than IPTL, na kam hiyo alternative nyingine inge-fail then yeye Patrick ali-offer kujiuzulu, ila Mkapa alikataa.
Sasa sijui which is which.
Anyways, hii mikanganyiko inanifanya ni-dive deep hata ktk ile issue ya Richmond-Dowans-Symbion..........nikijumlisha moja jumlisha moja napata 2, meaning hata huyo Lowassa nakuwa-convinced kuwa hakuwa na kosa lolote.
Kama Lowassa ana kosa kwenye Simbion basi hata Barrack Obama anakosa.

Nchi mambo yake yanashangaza sana,mfano hiyo richmond lowasa anasema"hakuna hata jambo moja tulilolifanya bila kumpatia rais taarifa,kuanzia hatua ya mwanzo kabisa...."rais naye anasema"mimi binafsi hiyo richmond siijui kabisa wala sina taarifa ya chochote kilichotokea..." baadaye akihutubia wazee wa dsm dimond jubilee rais aliendelea"lowasa hakuwa na kosa lolote bali alijiuluzu kwa sababu za kisiasa..."sasa nani mkweli hapa?
 
Mengi ndiye aliyekuwa OWNER wa gazeti la Mwanahalisi

hivyo alikuwa ni bosi wake Kubenea

Je mengi huyo huyo ndiye owner wa hili gazeti jipya la Kubenea?
 
The Boss wakati mwingine matumizi ya neno Fisadi huwa hayaeleweki. Fisadi kwako kwa mwingine anaweza kuwa ni mchapakazi anayezitolea jasho pesa zake kwa njia ya halali. Hivi una habari nchi hii kila mtu anayepita akiendesha gari hata kama ni la serikali anaitwa na baadhi ya watu kuwa ni fisadi? Na kama mhusika hana ushahidi wa kuthibitisha ufisadi wa mtuhumiwa anaishia kusema ndio walewale tu!! Inawezekana kabisa hata wewe the Boss kuna maeneo wanakuita Fisadi tu.
 
Nchi mambo yake yanashangaza sana,mfano hiyo richmond lowasa anasema"hakuna hata jambo moja tulilolifanya bila kumpatia rais taarifa,kuanzia hatua ya mwanzo kabisa...."rais naye anasema"mimi binafsi hiyo richmond siijui kabisa wala sina taarifa ya chochote kilichotokea..." baadaye akihutubia wazee wa dsm dimond jubilee rais aliendelea"lowasa hakuwa na kosa lolote bali alijiuluzu kwa sababu za kisiasa..."sasa nani mkweli hapa?

hapo wote wakweli
 
Katili huyu jamaa sana hakika ni mtusi
Unaposema Katili una maana gani ndugu? Fafanua ni ukatili gani aliokufanyia wewe au mtu mwingine unayemjua na ikiwezekana weka ushahidi hapa tuutafakari. Vinginevyo itauwa ni maneno ya vijiweni tu.

Kingine nakushauri kama msomi uache "stereotyping" au "generalization" kwa maana ya kuhukumu jamii nzima kwa kutumia kosa au tabia za mtu mmoja mmoja toka kwenye jamii husika. Hapa unataka kutuaminisha kuwa Mtusi yeyote ni mtu katili bila kutoa ushahidi wowote kuthibitisha hilo. Je akitokea mtu wa nje ya nchi akasema watanzania wote ni punda wa kubeba madawa ya kulevya kwa sababu tu kuna baadhi ya watu wamekamatwa nje atakuwa sahihi?
 
Katika jambo ambalo wanasiasa (wa chama tawala na wapinzani wao) wamefanikiwa sana nchi hii ni kulifanya suala la ufisadi kuwa ni dhana tu ya kisiasa. Hivi sasa haijulikani wanapoongelea ufisadi wanamaanisha nini hasa na mafisadi ndio akina nani kwani kwa sasa hili neno linatumika kama silaha ya mwanasiasa ya kuwashambulia wapinzani wake. Matokeo yake hakuna mtu anayeweza kutiwa hatiani kwa kutumia hii dhana ya kisiasa ya ufisadi. Kwa bahati mbaya zaidi hata waandishi wa habari wametekwa na hilo wimbi la kufanya ufisadi kuwa ni dhana tu ya kisiasa.
 
Kutokusikia kwako kusifanye hiyo ndiyo iwe ukweli halisia kwa kila Mtanzania. Kwanza kutokusikia kwako kunategemea na angle ya maisha yako ilipo. Jaribu kufanya research kwanza kutafuta ukweli kuliko kusubili kusikia.

Kuna watu vile vile hawakuwahi kumsikia 'Yesu au Mtume Muhammad (S.A.W)' mpaka wamekufa lakini haina maana kuwa hawa jamaa hawakuwahi kuwepo hapa duniani kama ilivyobainishwa na research na maandiko ya kale.

Unajua kukubali kukosolewa nako ni dalili ya uanaume, haya nimekubali kukosolewa ndugu yangu
 
Ukiongea na watu wengi aliofanya nao kazi ama wanaomjua kwa ukaribu watakueleza kuwa Patrick is one of the brilliant technocrats in this country. Additionally, I've been told that he's hard working, fearless, highly ethical and a tough cookie.
Inakuwa ni ngumu kuamini which is which.
 
Unajua kukubali kukosolewa nako ni dalili ya uanaume, haya nimekubali kukosolewa ndugu yangu
Ndugu yangu heshima mbele.

Angalizo lako siyo 'uanaume' au 'uanamke' peke yake bali pia ni mzizi wa falsafa ya kujifunza na katika kufanya hivyo, ndiyo hatua moja mbele kimaendeleo hupatikana.

Hata mimi ukinisoma sehemu ukagundua kuwa nimepungukiwa uelewa fulani, basi nitashukuru sana ukinigusa sikioni na kuniambia mapungufu yangu.

Tuko wote.
 
Hapa hii habari inanichanganya.
Kuna report niliisoma juu ya hiyo IPTL saga, ambapo inasisitiza kuwa Patrick ndio alimfuata na kumshauri Mkapa kwa kumwambia waachane na IPTL then watafute alternative nyingine other than IPTL, na kam hiyo alternative nyingine inge-fail then yeye Patrick ali-offer kujiuzulu, ila Mkapa alikataa.
Sasa sijui which is which.
Anyways, hii mikanganyiko inanifanya ni-dive deep hata ktk ile issue ya Richmond-Dowans-Symbion..........nikijumlisha moja jumlisha moja napata 2, meaning hata huyo Lowassa nakuwa-convinced kuwa hakuwa na kosa lolote.
Kama Lowassa ana kosa kwenye Simbion basi hata Barrack Obama anakosa.

Du na Obama tena kweli wewe unataka tugeuzwe Libya, bwana tusiwasemeseme wamarekani tuwaache waje kujichimbia zao mafuta na kuvuna gesi
 
Toka huko kwenye makabila ujadili hoja. Wenzio huko tulitoka kitambo. Ukitoka hapo utasema ni dini. Ovyoo!
 
Du na Obama tena kweli wewe unataka tugeuzwe Libya, bwana tusiwasemeseme wamarekani tuwaache waje kujichimbia zao mafuta na kuvuna gesi
Sasa kama hii mitambo ingekuwa ina ufisadi wowote Hillary Clinton wala si Obama asingethubutu kwenda Ubungo na kuipa baraka zake. Hii ni pasua kichwa na sioni jawabu. Richmond-Dowans-now Symbion-Obama
 
Ukiongea na watu wengi aliofanya nao kazi ama wanaomjua kwa ukaribu watakueleza kuwa Patrick is one of the brilliant technocrats in this country. Additionally, I've been told that he's hard working, fearless, highly ethical and a tough cookie.
Inakuwa ni ngumu kuamini which is which.

Nakubaliana na wewe mkuu...binafsi kuna mambo alinifanyia mazuri sana tena bado nikiwa kijana mwanachuo.
 
Back
Top Bottom