PreGE2025 Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hao umeona wanapinga msimamo wa chama wa REFORMS? Wako kimya kwahiyo watulie hivo hivo
 
Sure mkuu huyu katibu anapaswa apate promosheni..
Kwa ngazi ya tawi na barua ya level hiyo pongezi kwake.
 
Kama nje ni madikteta hivi kwenye hicho kikao ndo angepewa uhuru wa kutoa maoni?
Sielewi principles za vikao vyao kama kunakuminya maoni ya wajumbe.

Lakini je, nje waneonesha udikteta gani kwa wanachana ama viongozi wake?

Tuje upande 'B' je Ccm unaweza kuchongoroa mdomo wa kutoa maoni kipinzani nje ya utaratibu wa vikao wakakuacha?
 
Kwani hayahamia CHAUMA huyu?
 
Misingi ya demokrasia kuifuata yote ni kazi ngumu mno.maana demokrasia inataka hata wachache,wenye mawazo tofauti na ya wengi,nao waheshimiwe!
Mawazo yao wapeleke kwenye vikao na sio kuanzisha nje ya chama kwa kivuli cha CDM

Kabla ya vyama vingi kila mtu alikuwa CCM lkn leo kuna vyama kibao

Kama wana itkadi zao waanzishe vyama vyao

Kuitwa chama cha demokrasia haimaanishi demokrasia ni haki ya chadema peke yake.
 
Sidhani kama kuwafukuza chama ni busara.
Mkuu hivi ukimfumania live mkeo anatafunwa na jirani yako ukimpa talaka ni kukosa busara? Hao watu wanatumika na CCM kuihujuma Chadema wazi wazi, wamediriki hata kufungua kesi mahakamani Chadema isimamishwe kufanya shughuli za kisiasa na mratibu wa hujuma hiyo ni Ofisi ya Msajili wa vyama kwa maelekezo ya CCM.
 
Misingi ya demokrasia kuifuata yote ni kazi ngumu mno.maana demokrasia inataka hata wachache,wenye mawazo tofauti na ya wengi,nao waheshimiwe!
Ni sawa ila maazimio yakishafikiwa na vikao vya juu, kinachofuata ni utekelezaji wala si kuwa kinyume....
 
Then hii ni hatari....niliadhani wana mashiko. Wanapotaka chadema ifungiwe shughuli za kisiasa watafaitikaje sasa?
 
Hivi Tawi la Chama linaweza kumfuta mwanachama wa chamq cha siasa uanachama?
 
Acha uvivu soma baru hapo juu alafu sema kama kuna kanuni/sheria haijafuatwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…