Pata matatizo uwajue ndugu na marafiki wako

ugalila

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
652
599
Kuna jamaa yangu alikuwa ni mtu wa bata sana na alikuwa na marafiki wengi sana na ndugu walikuwa wakimkubali sana na kumpigia simu kila kukicha, ila sasa maisha haya hayana mwenyewe yamemgeukia jamaa katimuliwa kazini , biashara zake zimeyumba, madeni anayo kila mahali, na ugonjwa juu.

Naona anafarijiwa na mama yake tu na anasema hakuna ndugu wala rafiki anayekuja kumcheki na wote wana taarifa ya matatizo yake, wanaomsaidia ni watu ambao hata hakuwa nao kipindi cha bata, hadi yeye anajishangaa mwenyewe.

Nimejifunza kuchagua marafiki wa kweli ni vizuri zaidi maana haya maisha ukiambiwa nyuma geuka wa mwsho anakuwa wa kwanza na wa kwanza anakuwa wa mwisho.
 
Nilikuwa na rafiki kila weekend yupo kwangu, anajimwaga anavyopenda, tunakunywa wine, nyamachoma, anakaa Friday mpaka Sunday. Khe siku nimekuja kumpa shida yangu nilipata tatizo, aliniambia hawezi kunisaidia, kilichokera Zaidi, jamaa wakawa wananipigia simu kuniuliza kama ni kweli yaliyonisibu. Inamaana aliitangaza ile shida. Du, niliumia kama miezi miwili kwakuwa ni mtu alikuwa karibu sana na mimi nilidhani ndiyo best friend.

Nilikata na sasa ni karibu mwaka ninaishi kwa amani, hajui maisha yangu sijui ya kwake.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa n mtu wa bata sana na alikuwa na marafiki wengi sana na ndugu walkuwa wakimkubali sana na kumpgia smu kila kukicha, ila sasa maisha haya hayana mwenyewe yamemgeukia jamaa katimuliwa kazini , biashara zake zimeyumba, madeni anayo kila mahali, na ugonjwa juu, naona anafarijiwa na mama yake tu na anasema hakuna ndugu wala rafiki anayekuja kumcheki na wote wana taarifa ya ya matatizo yake, wanaomsaidia ni watu ambao hata hakuwa nao kipindi cha bata, hadi yeye anajishangaa mwenyewe

nimejifunza kuchagua marafiki wa kweli n vizuri zaidi maana haya maisha ukiambiwa nyuma geuka wa mwsho anakuwa wa kwanza , wa kwanza anakuwa wa mwisho,
Kweli kabisa. Ukitaka kumfaham adui yako subiri wakati wa neema. Ukitaka kumfaham rafiki yako subiri wakati wa taabu.
 
Nilikuwa na rafiki kila weekend yupo kwangu, anajimwaga anavyopenda, tunakunywa wine, nyamachoma, anakaa Friday mpaka Sunday. Khe siku nimekuja kumpa shida yangu nilipata tatizo, aliniambia hawezi kunisaidia, kilichokera Zaidi, jamaa wakawa wananipigia simu kuniuliza kama ni kweli yaliyonisibu. Inamaana aliitangaza ile shida. Du, niliumia kama miezi miwili kwakuwa ni mtu alikuwa karibu sana na mimi nididhani ndiyo best friend.

Nilikata na sasa ni karibu mwaka ninaishi kwa amani, hajui maisha yangu sijui ya kwake.
ninadhani ulilewa sana na vicheko vyake vya kinafiki na wewe ulishindwa kusoma alama za nyakati. masiko na macho vinapokea, vidole na mdomo vinaropoka. ndio watu walivyo siku zote. rafiki wa kweli ni wazazi wako na Mungu tu basi.
 
ninadhani ulilewa sana na vicheko vyake vya kinafiki na wewe ulishindwa kusoma alama za nyakati. masiko na macho vinapokea, vidole na mdomo vinaropoka. ndio watu walivyo siku zote. rafiki wa kweli ni wazazi wako na Mungu tu basi.

Si unajua wanafiki wavyokuwaga na kicheko, kuna mtu alinitonya kuwa yanayotokea nyumbani kwako weekend yote yako barabarani, nilimuuliza akaja juu, mimi ninasema kwa nani, tumuite tumuulize. Basi reality ilivyotokea sikumuuliza nilikata tu.
 
Back
Top Bottom