kabila01
JF-Expert Member
- Apr 21, 2009
- 4,235
- 4,949
Nitumie nafasi hii kuwakaribisha wapambanaji wenzangu tusiokata tamaa katika kilimo. Bonde hili lipo KM 10 tu kutoka Iringa Mjini usafiri wa daladala na nauli ni sh 500 tu. Unaweza kukaa Iringa Mjini asubuhi unaenda shamba jioni unarudi.
Ukiamua kukaa kule poa mazingira mazuri umeme upo na nyuma za kupanga zipo kodi ni kama elfu 20 kwa mwezi chumba chenye umeme.
Bonde hili linaenda sambamba na Mto Ruaha, serikali imejenga Scheme za umwagiliaji maji yanapatikana kwa wingi mwaka mzima na wala hutumii machine kumwagilia. Scheme ya umwagiliaji ni kubwa sana inapita vijiji kama 7 unaanzia Kalenga mpaka Kigara karibia na Pawaga.
Mashamba yanakodishwa kwa shilingi laki moja na nusu kwa msimu na unalipia elfu 25 gharama ya maji kwa msimu mzima.
Mazao yanayolimwa ni vitunguu, nyanya, hoho, nyanya chungu, mahindi gobo, green beans nk.
Wapambanaji karibuni.