Pastor Huruma Nkone, Dr Chris Mauki na Dr Kinyondo kuwafunda vijana

Ngambako

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
315
263
Salaam wana JF

Kwa karne hii, jamii ya vijana imekuwa ikikumbwa sana na changamoto mbalimbali, vijana wengi wamekuwa wakihusisha changamoto kama vile za Mahusiano, Ajira na Masomo ni moja kati ya changamoto zinazowakumba vijana wengi hapa nchini

kwa mantiki hiyo, jumuiya ya kanisa la Victoria christian Center Tabenacle (VCCT) linaloongozwa na Mchungaji kiongozi Pastor Dr Huruma Nkone kwa kushirikiana na wataalamu katika fani za elimu na saikolojia Dr Kinyondo,Muhadhiri chuo kikuu cha Dar es Salaam na Mkurugenzi wa idara ya utafiti pale REPOA kwa kushirikiana na Dr Chris Mauki wa wamewaandalia vijana wa Dar es Salaam semina ya usiku mzima kwa siku ya kesho ijumaa kuanzia saa 3 usiku mpaka 11 alfajiri. semina hii itafanyika eneo la Mbezi Beach A Mtaa wa kilimani kupitia mwai kibaki road.

Semina hiyo itaongozwa na Mziki kutoka kwa waimbaji wazuri kama vile Godlucky Gozbert, Ipyana Kibona na kundi la Hyper Squad, pamoja na nyimbo kutakuwa na Maigizo na Ngonjera nzuri kutoka kwa wataalamu wa fani hiyo.

Semina hiyo itaongozwa na Mtangazaji mashuhuri na MC makini ndugu Sam Ssasali kutoka clouds TV.

Semina hiyo itakuwa ni bure kabisa

Nyote mnakaribishwa
 

Attachments

  • Vcct.jpg
    Vcct.jpg
    55.7 KB · Views: 62
Hapo ndipo panaponishinda....

..."Semina hiyo itaongozwa na Mziki kutoka kwa waimbaji wazuri kama vile Godlucky Gozbert, Ipyana Kibona na kundi la Hyper Squad, pamoja na nyimbo kutakuwa na Maigizo na Ngonjera nzuri kutoka kwa wataalamu wa fani hiyo"....

....."Semina hiyo itaongozwa na Mtangazaji mashuhuri na MC makini ndugu Sam Ssasali kutoka clouds TV".....
 
Back
Top Bottom