Passive Income Haiwezi kukutajirisha - Wanakudanganya.

Smart Finance

Member
Joined
Apr 10, 2025
Posts
35
Reaction score
114
Imeandaliwa na Smart Finance SW

Siku hizi, watu wengi wanapenda kusikia kuhusu habari za passive income. Wanavutiwa na njia za kutengeneza pesa kupitia mfumo huu. Kama hujui passive income ni nini, nitaeleza kwa ufupi lakini unaweza pia kufanya utafiti wako binafsi.

Passive income ni kipato kinachopatikana bila kufanya kazi ya kila siku. Kwa mfano, umejenga nyumba na kuzipangisha unapokea kodi kila mwezi. Ile kodi ni passive income. Au umenunua hisa, na kila mwaka unapokea gawio; lile gawio nalo ni passive income.

Mimi ni muumini mkubwa wa passive income na nafanya kazi kwa bidii, naumiza kichwa kutengeneza platform imara itakayoniingizia kipato cha aina hii. Lakini ukweli ni kwamba huwezi kuwa tajiri kwa kutegemea passive income pekee, hasa ukiwa bado kijana.

Kwa nini?

Kwa sababu, ili upate pesa kutoka kwenye passive income, ni lazima kwanza ufanye kazi inayokupa active income. Ili ulipwe kodi, ni lazima kwanza ujenge nyumba. Na ili ujenge nyumba, ni lazima kwanza ufanye kazi au biashara inayozalisha faida.

Sasa tumeona kwa uwazi kabisa ni kwa jinsi gani ambavyo passive income inategemea active income katika utengenezwaji wake. Haya tuendelee

Tuseme umejenga nyumba ya kupangisha yenye units tatu na unapokea kodi ya laki moja kwa kila Unit. Amini usiamini, hiyo laki tatu kwa mwezi itakusaidia kula, kunywa, kuvaa, na kugharamia mambo madogo madogo tu. Haitoshi kukuwezesha kuendesha maisha yako kwa mafanikio makubwa kama utategemea kodi pekee.

Mimi naipenda passive income kwa sababu naitumia kama njia ya kulinda kile nilichopata kupitia active income. Unajua, kupata pesa si kazi sana ila kuitunza na kuizalisha ndio changamoto inapoanzia. Kupitia passive income, naweza kuitunza pesa yangu, na kuiwekeza ili izae taratibu. Ingawa matokeo yake ni madogo madogo kwa mara moja, kadri muda unavyoenda faida pia inaonekana.

Kama wewe ni kijana, nakushauri ujifunze kuhusu passive income, lakini utumie muda wako mwingi kwenye active income. Katika kila pesa unayopata, tumia asilimia 30 pekee kwa ajili ya kujenga msingi wa passive income. Isizidi 30%.

Lakini kama umri wako umeenda, basi wekeza nguvu na muda wako zaidi kwenye passive income, na ikiwezelana tumia zaidi ya asilimia 70 ya mapato yako huko.

Kwa nini nasema haya, ilhali mimi ni muumini wa passive income? Kwa sababu mapato ya aina hii huwa madogo ukilinganisha na active income. Na kwa nini madogo? Kwa sababu risk yake ni ndogo pia.

Kumbuka: muda haumsubiri mtu. Ukiwa kijana una nguvu na muda wa kutosha. Ni busara kuzitumia rasilimali hizi (Muda na Nguvu) kujenga msingi wa maisha yako ya baadaye, na kutengeneza faida kubwa katika kile unachokifanya.... ili ukifikia uzeeni, uvune kile ulichopanda ujanani.

Wanasema: "Ujana wako ndiyo utaamua uzeeni ucheze draft au golf."

Share ujumbe huu kwa ndugu, jamaa na marfiki na wao waweze kujifunza. Lakini pia unaweza jiunga kwenye WhatsApp Channel yetu kupitia link hapo chini ili tujifunze kwa pamoja.

NB: Mafunzo yote hutolewa bure.

Follow the Smart Finance - SW channel on WhatsApp: Smart Finance - SW | WhatsApp Channel
 
Unamfahami Warren Buffett? Huyo kazi yake ni kupata gawio ana hisa Coca cola ,Apple na makampuni kibao na ni tajiri mkubwa duniani.Rudia Tena kufanya utafiti wako

Usiyoyajua kuhusu huyo mzee ni kwamba hayo magawio unayoyaona ya coca, apple na kampuni zengine alizowekeza ni hatua za mwisho kabisa za safari yake ya mafanikio.

Ngoja nikuulize ndugu yangu. Wewe unafikiri mpaka kufikia kulipwa zaidi ya $700m (Trilioni 1.795 TZS) kama gawio kwa mwaka, huyu mtu amewekeza kiasi gani? Hizo pesa alizitoa wapi?

Funguka na usibaki gizani, Warren Buffet enzi za utoto wake akiwa na miaka 6 tu alikuwa muuza magazeti na chupa za soda, hiyo ni active income.

Hakuishia hapo aliuza mpaka vifaa vya michezo, nenda ufanye research utaona huyu mzee hustling kaanza kitambo. Unazijua ping pong? Buffet ameziuza sana na faida aliyokuwa akipata alinunua hisa kidogo kidogo.

1956 Warren Buffet alifungua kampuni yake mwenyewe na iliitwa "Buffet Partneship Ltd" nenda katafute hii ni homework nakupa. Warren Buffet kauza mpaka nguo, faida aliyokuwa akipata kwenye biashara zake alikuwa akinunua maduka ya nguo pesa nyengine ananunua hisa.

Alafu gawio la hisa ananunua tena hisa zengine na faida za kwenye biashara zake sehemu kubwa alikuwa alikuwa akinunua hisa na kupanua biashara zake. Amefanya mikutano kibao na semina kibao na zote hizo alikuwa akilipwa pesa nyingi tu.

Ngoja nikwambie kitu bwana Girland, huyo mzee unaemzungumzia utajiri wake umechangiwa kwa kiasi kikubwq sana na active incomes. Ila alikuwa mjanja, pesa alizokuwa akipata huko aliwekeza vyema kwenye assets zinazomletea passive income ambazo ndo hizo umeziona wewe.

Sasa wewe ruka moja kwa moja kwenye passive income uone kama huvai shera msibani.
 
Hakutuma na ya kutolea
 
Unauwezo wa kufanya passive income sources zako kuwa sources za active income yako.

Kumbuka return ya kwenye investments, say nyumba (au real estate in general) sio kodi pekee. Ni wewe kujua jinsi ya kuishi nayo ikutengenezee pesa. Wengi wetu tunajua ni kodi pekee.
 
Uko sahihi... na utakubaliana nami kwamba ukitegemea passive income peke yake HUTOBOI
 
Mkuu forex na fursa zinazoendana na forex (betting)
unaziweka katika kundi gani active au passive
 
Hiyo ni high risk na haipaswi kuhesabiwa kama chanzo cha kipato bali sehemu ya kujifurahisha tu kwa pesa za ziada sana
 
Unamfahami Warren Buffett? Huyo kazi yake ni kupata gawio ana hisa Coca cola ,Apple na makampuni kibao na ni tajiri mkubwa duniani.Rudia Tena kufanya utafiti wako
Duh! Mababu kwa hiyo wewe ndio unamjua Warren Buffett?
 
Imeandaliwa na Smart Finance SW

Siku hizi, watu wengi wanapenda kusikia kuhusu habari za passive income. Wanavutiwa na njia za kutengeneza pesa kupitia mfumo huu. Kama hujui passive income ni nini, nitaeleza kwa ufupi lakini unaweza pia kufanya utafiti wako binafsi.

Passive income ni kipato kinachopatikana bila kufanya kazi ya kila siku. Kwa mfano, umejenga nyumba na kuzipangisha unapokea kodi kila mwezi. Ile kodi ni passive income. Au umenunua hisa, na kila mwaka unapokea gawio; lile gawio nalo ni passive income.

Mimi ni muumini mkubwa wa passive income na nafanya kazi kwa bidii, naumiza kichwa kutengeneza platform imara itakayoniingizia kipato cha aina hii. Lakini ukweli ni kwamba huwezi kuwa tajiri kwa kutegemea passive income pekee, hasa ukiwa bado kijana.

Kwa nini?

Kwa sababu, ili upate pesa kutoka kwenye passive income, ni lazima kwanza ufanye kazi inayokupa active income. Ili ulipwe kodi, ni lazima kwanza ujenge nyumba. Na ili ujenge nyumba, ni lazima kwanza ufanye kazi au biashara inayozalisha faida.

Sasa tumeona kwa uwazi kabisa ni kwa jinsi gani ambavyo passive income inategemea active income katika utengenezwaji wake. Haya tuendelee

Tuseme umejenga nyumba ya kupangisha yenye units tatu na unapokea kodi ya laki moja kwa kila Unit. Amini usiamini, hiyo laki tatu kwa mwezi itakusaidia kula, kunywa, kuvaa, na kugharamia mambo madogo madogo tu. Haitoshi kukuwezesha kuendesha maisha yako kwa mafanikio makubwa kama utategemea kodi pekee.

Mimi naipenda passive income kwa sababu naitumia kama njia ya kulinda kile nilichopata kupitia active income. Unajua, kupata pesa si kazi sana ila kuitunza na kuizalisha ndio changamoto inapoanzia. Kupitia passive income, naweza kuitunza pesa yangu, na kuiwekeza ili izae taratibu. Ingawa matokeo yake ni madogo madogo kwa mara moja, kadri muda unavyoenda faida pia inaonekana.

Kama wewe ni kijana, nakushauri ujifunze kuhusu passive income, lakini utumie muda wako mwingi kwenye active income. Katika kila pesa unayopata, tumia asilimia 30 pekee kwa ajili ya kujenga msingi wa passive income. Isizidi 30%.

Lakini kama umri wako umeenda, basi wekeza nguvu na muda wako zaidi kwenye passive income, na ikiwezelana tumia zaidi ya asilimia 70 ya mapato yako huko.

Kwa nini nasema haya, ilhali mimi ni muumini wa passive income? Kwa sababu mapato ya aina hii huwa madogo ukilinganisha na active income. Na kwa nini madogo? Kwa sababu risk yake ni ndogo pia.

Kumbuka: muda haumsubiri mtu. Ukiwa kijana una nguvu na muda wa kutosha. Ni busara kuzitumia rasilimali hizi (Muda na Nguvu) kujenga msingi wa maisha yako ya baadaye, na kutengeneza faida kubwa katika kile unachokifanya.... ili ukifikia uzeeni, uvune kile ulichopanda ujanani.

Wanasema: "Ujana wako ndiyo utaamua uzeeni ucheze draft au golf."

Share ujumbe huu kwa ndugu, jamaa na marfiki na wao waweze kujifunza. Lakini pia unaweza jiunga kwenye WhatsApp Channel yetu kupitia link hapo chini ili tujifunze kwa pamoja.

NB: Mafunzo yote hutolewa bure.

Follow the Smart Finance - SW channel on WhatsApp: Smart Finance - SW | WhatsApp Channel
asante sana kwa ujumbe mzuri " Ujana wako ndio utaamua uzeeni ucheze draft au golf"
 
Sijaelewa jibu lako.
Akili kisoda huwezi kuelewa. Ngoja nikufafanulie, hivyo vilivyotajwa hapo mambo ya kucheza betting havitakiwi kuchukuliwa kama chanzo cha kipato kwani vinaweza kukufanya maskini wa kupindukia
 
Akili bia unaelewa au unalewa? Mantiki ya swali langu sio dhihaka ni kutaka kujua na kuelewa kwa upana zaidi aina ya hizo passive na active income na sio vinginevyo.
 
Usiyoyajua kuhusu huyo mzee ni kwamba hayo magawio unayoyaona ya coca, apple na kampuni zengine alizowekeza ni hatua za mwisho kabisa za safari yake ya mafanikio.

Ngoja nikuulize ndugu yangu. Wewe unafikiri mpaka kufikia kulipwa zaidi ya $700m (Trilioni 1.795 TZS) kama gawio kwa mwaka, huyu mtu amewekeza kiasi gani? Hizo pesa alizitoa wapi?

Funguka na usibaki gizani, Warren Buffet enzi za utoto wake akiwa na miaka 6 tu alikuwa muuza magazeti na chupa za soda, hiyo ni active income.

Hakuishia hapo aliuza mpaka vifaa vya michezo, nenda ufanye research utaona huyu mzee hustling kaanza kitambo. Unazijua ping pong? Buffet ameziuza sana na faida aliyokuwa akipata alinunua hisa kidogo kidogo.

1956 Warren Buffet alifungua kampuni yake mwenyewe na iliitwa "Buffet Partneship Ltd" nenda katafute hii ni homework nakupa. Warren Buffet kauza mpaka nguo, faida aliyokuwa akipata kwenye biashara zake alikuwa akinunua maduka ya nguo pesa nyengine ananunua hisa.

Alafu gawio la hisa ananunua tena hisa zengine na faida za kwenye biashara zake sehemu kubwa alikuwa alikuwa akinunua hisa na kupanua biashara zake. Amefanya mikutano kibao na semina kibao na zote hizo alikuwa akilipwa pesa nyingi tu.

Ngoja nikwambie kitu bwana Girland, huyo mzee unaemzungumzia utajiri wake umechangiwa kwa kiasi kikubwq sana na active incomes. Ila alikuwa mjanja, pesa alizokuwa akipata huko aliwekeza vyema kwenye assets zinazomletea passive income ambazo ndo hizo umeziona wewe.

Sasa wewe ruka moja kwa moja kwenye passive income uone kama huvai shera msibani.
😁😁😁🙌

Last paragraph
 
Mkuu forex na fursa zinazoendana na forex (betting)
unaziweka katika kundi gani active au passive
Forex trading ni active income kwasababu inahitaji ushiriki wako wa moja kwa moja. Lazima utumie muda kulisoma soko kila siku, kufanya maamuzi ya haraka, kusoma graphs yaani kwa kifupi ili uwe forex trader mzuri na mwenye mafanikio lazima uhusike moja kwa moja na tradings zako.

Ila kuna baadhi ya fursa zinazoendana na forex zenyewe ni passive income. Kwa mfano unaanda kozi kuhusu kitu fulani kuhusu forex. Hiyo kozi inaweza kuwq labda video kisha unaipakia youtube. Hio ni passive income kwasababu video hio itaendelea kukuletea kipato bila kufa ushiriki wako wa moja kwa moja. Au tuseme unaandika kitabu alafu ukiuze amazon hio ni passive.

Pia kuhusu betting kama umeifanya ni chanzo chako cha mapato hio itaangukia kwenye active income kwasababu lazima kila siku uingie sokoni kuandaa mkeka. Hata kama ukatengeneza treni la mwaka mzima hio bado ni active income kwakuwa hutoweza kupata pesa mpaka mechi ziishe, na uki cash out bado utaingia tena sokoni kwaajili ya kutengeneza mkeka mwengine.

NAtumai umenielewa ndugu yangu
 
Back
Top Bottom