Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya Hon Mbowe

Status
Not open for further replies.
Mkuu Pasco.Heshima mbele.

Nimeamua kuanzisha thread hii kwa makusudi kabisa ila kuondoa upotoshaji ambao umeufanya hasa kwa wale ambao hawajatazama Bunge. Kuna watu wengi tu hawajatazama Bunge na hawatapata muda wa kutazama hivyo ukisema kuwa CHADEMA tumekubali yaishe na kumtambua Rais si kweli. Kwanza napenda ieleweke kuwa kumpongeza mtu ni tamaduni ya kawaida kabisa na pale mtu anapostahili pongezi basi hana budi kupongezwa.

Alichokisema Mbowe ni kumpongeza Rais kwa kukubali kuandaa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya pamoja na kwamba suala hili halikuwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hayo mengine ya kumtambua hajasema. Kuongeza ni suala la kawaida sana. Na amesisitiza kuwa atapongeza kila zuri litakapofanywa iwe kwa chama au kwa serikali. Hansard ikitoka nitaweka hapa.

Naomba uiondoe thread yako. Ili usipotoshe na wengine pia.

Kutoka Mjengoni
Aluta Continua.
Ni heri angempongeza kama mwenyekiti wa chama chake cha ccm,sasa kama amempongeza kama rais,then ni sawa na kumtambua tu.Mngemshauri mwenyekiti wenu aseme kuwa anampongeza mwenyekiti wa ccm kwa kuamua kuitumia hoja ya cdm kwa manufaa ya Taifa.
Labda shida iko hapo Pasco aliposema cdm "Wamekubali yaishe"
Binafsi sikutazama bunge,so Pasco atuwekee vithibitisho vya kauli yake hiyo kama anaweza.Akifanya hivyo sioni sababu ya kuomba msamaha,certainly hana sababu ya kuomba msamaha kuhusu mwenyekiti wenu kumtambua JK kama Rais.
 
Kumbe na wewe umeliona enh........? mie nilidhani peke yangu ndio sina macho na akili ya kusoma na kukijua kilichoandikwa hapo. Ama kweli Siasa ni mchezo unaohitaji kipawa cha kuweza kumshawishi mtu aamini unayoyasema hata kama ni uongo!
 
Asante Mh. regia kwa kumtaka pasco ajitokeze na kuondoa oungo wake.

Pamoja na shukurani zangi, Mh. nina concern moja ambayo wewe na Wah. wabunge wa CDM kama mnaweza kutufafanulia;
inakuwaje mnakubali kupoteza kodi za wapiga kura wenu kwa kutumia siku tano (5) !!!! kujadili hotuba ya JK ?? Kwa faida gani kwa nchi hii!!
Nilitegemea mngeonyesha mfano kwa kulitolea swala hili your dissatisfaction kama chama , badala ya kuungana na hao ccm kulijadili wholesale bila kuonyesha kukerwa na matumizi mabaya ya muda wa bunge, and hence pesa za wapiga kura. (of course kuhoji kwenu kusingebadilisha mjadala, lakini tungeona kwamba mmeonyesha ni yepi maswala muhimu ya kujadili)

Duh hilo swala litakuwa gumu sana kwa maana aaah mpango mzima wa posho unadhani utakaaje? Mie nasema na narudia kusema tusikubali haya maigizo sijui ya CCM, CDM sijui CUF na NCCR hawa wanasiasa ni wasanii wanangalia kwanza maslahi yao yetu yanakuja baadae wewe fikiria hawamtambui Rais halafu wanachangia hotuba ya Rais unaelewa kweli mie naona maruweruwe tu..................
 
Ni heri angempongeza kama mwenyekiti wa chama chake cha ccm,sasa kama amempongeza kama rais,then ni sawa na kumtambua tu.Mngemshauri mwenyekiti wenu aseme kuwa anampongeza mwenyekiti wa ccm kwa kuamua kuitumia hoja ya cdm kwa manufaa ya Taifa.
Labda shida iko hapo Pasco aliposema cdm "Wamekubali yaishe"
Binafsi sikutazama bunge,so Pasco atuwekee vithibitisho vya kauli yake hiyo kama anaweza.Akifanya hivyo sioni sababu ya kuomba msamaha,certainly hana sababu ya kuomba msamaha kuhusu mwenyekiti wenu kumtambua JK kama Rais.

Heshima kwako Jmushi1.

Mkuu tuko pamoja KUB mheshimiwa F Mbowe alitakiwa ampongeze JK kama mwenyekiti wa CCM na akwepe kabisa kutaja cheo cha rais ningekuwa mtu wa kwanza kumshikia bango Pasco lakini kwa hili hastahili kabisa kuomba radhi.
 
Hansard ndiyo msema kweli: hata sisi ambao hatukuangalia Bunge itabidi tuifatilie kwa kina ili tujirizishe.
 
Pasco anapoteza credibility taratibu. Kwanza alianza na pesa mpya kutoka BOT. Akaja na la Lema...kumkashifu hapa kwa kumwita waziri mkuu mwongo. Na sasa hili?....
 
Hili BwaBwa Pasco halijaomba radhi tu?

Mkuu Pasco.Heshima mbele.

Nimeamua kuanzisha thread hii kwa makusudi kabisa ila kuondoa upotoshaji ambao umeufanya hasa kwa wale ambao hawajatazama Bunge. Kuna watu wengi tu hawajatazama Bunge na hawatapata muda wa kutazama hivyo ukisema kuwa CHADEMA tumekubali yaishe na kumtambua Rais si kweli. Kwanza napenda ieleweke kuwa kumpongeza mtu ni tamaduni ya kawaida kabisa na pale mtu anapostahili pongezi basi hana budi kupongezwa.

Alichokisema Mbowe ni kumpongeza Rais kwa kukubali kuandaa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya pamoja na kwamba suala hili halikuwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hayo mengine ya kumtambua hajasema. Kuongeza ni suala la kawaida sana. Na amesisitiza kuwa atapongeza kila zuri litakapofanywa iwe kwa chama au kwa serikali. Hansard ikitoka nitaweka hapa.

Naomba uiondoe thread yako. Ili usipotoshe na wengine pia.

Kutoka Mjengoni
Aluta Continua.

Mkuu soma kwenye hiyo nyekundu halafu tueleze uhalali wa Pasco kuwaomba radhi CDM na sisi kwa kutuletea habari za uongo! Nadhani kuna tatizo sisi wenyewe pengine ni vipofu au uelewa wetu umeenda arijojo na uchizi unapoiga jaramba
 
Heshima kwako Jmushi1.

Mkuu tuko pamoja KUB mheshimiwa F Mbowe alitakiwa ampongeze JK kama mwenyekiti wa CCM na akwepe kabisa kutaja cheo cha rais ningekuwa mtu wa kwanza kumshikia bango Pasco lakini kwa hili hastahili kabisa kuomba radhi.

Kikwete hakuanzisha mchakato wa katiba kama mwenyekiti wa CCM, bali alianzisha kama raisi, hivyo alipaswa kupongezwa kama raisi. CDM wameshasema siku zote wanaheshimu sheria zilizopo zinazomtambua Kikwete kuwa raisi. Hata hivyo wanapinga uhalali wa sheria hizo, hence uhalali wa raisi.
 
Heshima kwako Jmushi1.

Mkuu tuko pamoja KUB mheshimiwa F Mbowe alitakiwa ampongeze JK kama mwenyekiti wa CCM na akwepe kabisa kutaja cheo cha rais ningekuwa mtu wa kwanza kumshikia bango Pasco lakini kwa hili hastahili kabisa kuomba radhi.

wewe na CDM tabu sana!! Ubunge Arusha subiri 2015 bana
 
Asante RM sasa tunamsubiri Pasco aje atupe vizuri ufanunuzi wa thread yake ni wapi alipoyatoa hayo aliyoyaeleza.
 
Alichosema Mh. Mbowe mjengoni leo, angalia video clip hii hapa.

Video kwa hisani ya MICHUZI Blog
 
Last edited by a moderator:
Ni heri angempongeza kama mwenyekiti wa chama chake cha ccm,sasa kama amempongeza kama rais,then ni sawa na kumtambua tu.Mngemshauri mwenyekiti wenu aseme kuwa anampongeza mwenyekiti wa ccm kwa kuamua kuitumia hoja ya cdm kwa manufaa ya Taifa.
Labda shida iko hapo Pasco aliposema cdm "Wamekubali yaishe"
Binafsi sikutazama bunge,so Pasco atuwekee vithibitisho vya kauli yake hiyo kama anaweza.Akifanya hivyo sioni sababu ya kuomba msamaha,certainly hana sababu ya kuomba msamaha kuhusu mwenyekiti wenu kumtambua JK kama Rais.

Heshima kwako Jmushi1.

Mkuu tuko pamoja KUB mheshimiwa F Mbowe alitakiwa ampongeze JK kama mwenyekiti wa CCM na akwepe kabisa kutaja cheo cha rais ningekuwa mtu wa kwanza kumshikia bango Pasco lakini kwa hili hastahili kabisa kuomba radhi.
Mkuu Ngongo,
kama hukupata kusoma haya na kama hutokuwa mvivu naomba ugonge hapa
 
Ifike wakati mfanye kama hivi pale mnapoona upotoshwaji unafanyika kwa vyama vingine hii itawasaidia kuonekana mnasimamia haki na nidhamu ya JF. Siku zote huwa nasisitiza umuhimu wa kuheshimiana na kutokuzuliana maneno. Jana kina HR na Kafulila walizuliwa kuwa wameangushwa kwenye kugombea uenyekiti wa PAC na POC, Sijakusikia wewe Regina wana Mkumbo kuwarekebisha watu na kuwaeleza ikweli mlinyamaza kimya. Ila mkiguswa nyie mtaanzisha thread za kuomba msamehewe. Uungwana ni kufanya yasio wachukiza wengine sio kuacha kufanywa yanayokuchukiza wewe tu.

Ahibal nasi matuhibul nafsik penda nafsi ya mwenzako kama unavyoipenda nafsi yako.

Shukran.

Mh. Regia sio mbunge wa cuf wala nccr mageuzi na Dr. Mkumbo si msemaji wa cuf wala nccr mageuzi.

Kama unadhani Hamadi rashid na kafulila hawaijui jf ama hawawezi kujitokeza jf kukanusha hizo taarifa za uongo dhidi yao basi ni vizuri ukaendelea kuwa advocate wao kama unavyofanya mara zote.
Anzisha thread ya kuwasemea au kuonyesha uongo ulioletwa kwenye forum, sio kila kitu unataka utafuniwe tuuu unasubiri kumeza.
Mh. Regia na Dr. Mkumbo ni wanaforum kama walivyo wengine, wanatoa mawazo yao kadri wanavyoona inafaa, sasa wewe kuja kuwapangia waseme nini hilo sio jukumu lako, ifike mahala uwe na heshima na adabu kwa wenzio hata kama hamkubaliani kiitikadi.

Vinginevyo, we wahi tu lushoto ukalime mapeasi kama ulivyosema mwenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom