Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Kikwete hakuanzisha mchakato wa katiba kama mwenyekiti wa CCM, bali alianzisha kama raisi, hivyo alipaswa kupongezwa kama raisi. CDM wameshasema siku zote wanaheshimu sheria zilizopo zinazomtambua Kikwete kuwa raisi. Hata hivyo wanapinga uhalali wa sheria hizo, hence uhalali wa raisi.
Heshima kwako Tuko,
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Jakaya Mrisho kikwete aliongoza kikao cha CC na kuafiki Dowwans ilipwe.Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT aliongoza kikao cha wabunge wa CCM na kuamuru malipo ya Dowans yasilipwe.Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT kwenye sherehe za kutimiza miaka 34 hairuka Dowans asema hawajui wala hana hisa pia hajawahi kukutana nao.
Mifano yote mitatu inamzungumzia mtu mmoja mwenye kofia mbili ,Kikwete ni rais na ni mwenyekiti wa CCM .Mtu huyu Kikwete anaweza kutambulishwa kwa kofia mojawapo kutegemea na shughuli anayoifanya inaegemea wapi lakini bado hawezi kuikana au kuidharau kofia nyingine.
Mheshimiwa Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM alipohutubia sherehe za miaka 34 Dodoma kofia ya uenyekiti wa CCM ilikuwa ikitajwa zaid kuliko Rais wa JMT kwakuwa alikuwa kwenye sherehe zinazowahusu CCM zaidi.Tunaweza kusema alikuwa kichama zaidi.Mheshimiwa Rais Kikwete anapompokea mgeni eg balozi wa nchi nyingine anakuwa kiserekali ziadi hivyo kofia ya Urais inachukua nafasi yake.
Mheshimiwa Freeman Mbowe alikuwa katika nafasi nzuri sana kumpongeza Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM kwa kukubali kuandaa mchakato wa mabadiliko ya katiba ingawa CCM hawakuliweka kwenye ilani yao ya uchaguzi.Ipo point moja muhimu sana hapa CHADEMA waliweka kwenye ilani yao mchakato wa kubadili katiba.
[1] CCM wamechukua baadhi ya mambo mazuri kutoka CHADEMA.
[2] CCM haiwezi kufanya hivyo bila ridhaa ya mwenyekiti wake ambae ni Kikwete,sasa kulikuwa na shida gani KUB kumaddress kama Mwenyekiti.
[3] Kwakuwa CHADEMA hawamtambui Kikwete kama Rais wa JMT,je ipo kanuni ya bunge inayowalazimisha kumaddress kikwete kama Rais ?.kama haipo ni kwanini CHADEMA wanatuzuga kwamba hawamtabui ?.
[4] Ifike mahali CHADEMA iache kuzungusha zungusha watuambie ukweli bila kificho wakifanya hivyo watakuwa huru.Hawatakuwa na sababu za kutoa maelezo kitendo cha mwenyekiti wao kupeana mikono na Rais Kikwete na tabasamu la nguvu.